Usajili wa Namba za Simu - Unachotakiwa Kujua

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Hizi ni habari njema sana lakini pamoja na haya kuna vitu watu wanatakiwa wajue .

Ukiwa unashida yoyote kwenye masuala ya usajili wa namba au kifaa chako cha mawasiliano onana na kuto cha mtoa huduma wa mawasiliano yako kama wao wanashindwa kukusaidia wasiliana na msimamizi mkuu wa masuala ya mawasiliano tanznaia www.tcra.go.tz na pia kuna chama cha watumiaji wa huduma za mawasiliano sijui anuani yao unaweza kuwatafuta kwa ufafanuzi zaidi .

Ni vizuri ukaenda kusajili simu mwenyewe na usimtume mtu wala kwenda kusajili namba za simu za wengine kwa sababu endapo chochote kikitokea huko mbeleni unaweza kuwajibika wewe moja kwa moja kuna masuala ya uhalifu , wahalifu wengine wanaficha sura zao na kutuma ndugu na jamaa zao kwenda kuwasajilia , wengine ni watu waliofariki dunia lakini walikuwa na vitambulisho vya kupiga kura kuna wahalifu wanatumia vitambulisho hivi kwenda kusajili taarifa ambazo sio sahihi .

Lakini pia kumetokea shida ya usajili haswa kwa wale wanaotumia namba za mitandao mengine ya nchi tofauti ambazo labda hazina utaratibu wa kusajili na mambo kama hayo haswa kwa wale ambao wanakuja nchini kwa siku moja au 2 na kuondoka na kuna wengine wanaoishi maeneo ya mipakani wanaofanya kazi upande mmoja na mwingine hizi zote ni changamoto za kufanyia kazi sasa hata huko mbeleni .

Njia ya Karibu zaidi ya Kumfikia mwananchi Mapema zaidi na haraka akiwa popote Tanzania kwa sasa ni njia ya simu , labda kwa kumpigia , kumtumia ujumbe mfupi kama yuko sehemu ambayo mtandao unapatikana kwa shida basi akisogea sehemu yenye mtandao mzuri anaweza kupokea ujumbe mfupi sms .

Ujumbe huu mfupi unaweza kutumika sio kwenye shuguli za biashara na masoko kama kampuni nyingi za simu zinavyofanya kwa wateja wao hata kwenye shuguli zingine za kijamii mfano mbunge wenu anakuja kutembelea eneo lenu siku fulani badala ya kuchafua miti kwa matangazo na gharama zingine za kutangaza kwa gari anaweza kutumia namba zetu za simu zilizosajiliwa kwa ajili ya kuwapelekea ujumbe na taarifa mkaipata wote sio mbunge tu kuna mengi yanatokea ambapo wananchi wanatakiwa kushirikishwa lakini wengi wanashindwa kutekeleza hivyo kutokana na kutowajua watu wao na taarifa zao zingine .

Kuna masuala ya takwimu yanayofanywa na taasisi kadhaa huko nyuma yamewahi kuwa tabu kidogo kutokana na huduma za mawasiliano usajili huu unaweza kusaidia sana masuala ya takwimu kuanzia serikalini , taasisi zingine za kijamii , kampuni za simu na wale wengine wanaotaka kutoa huduma zingine kwa jamii zingine nchini .

Na mwisho kuna watu ambao wanaogopa kuhusu kufuatiliwa masuala yao ya mawasiliano kama simu na mengine nadhani kama huna kosa na hufanyi hujuma yoyote hakuna atakayekufuatilia haswa vyombo vya usalama lakini taarifa zako zinaweza kutumika kwenye shuguli zingine za masoko kwa kampuni za mawasiliano na labda kama kampuni hizo zikiamua kutoa namba zako kwa kampuni zingine ili kuweza kutuma matangazo yao kwako hayo ni makubaliano yako na kampuni hizo za simu na kama hukuwahi kufanya makubaliano hayo ni vizuri ukawasiliana na huduma kwa wateja na taasisi zingine nilizoeleza hapo juu .

Ni haki yako wewe mteja kujua kama taarifa ulizoweka kwenye usajili wa simu kama zimehifadhiwa kwa usahihi na sehemu salama na zimepotumika vinginevyo pia ni haki yako kutumia vyombo vya sheria vilivyopo kuweza kushitaki na kulipwa fidia .

Nakutakia mchana mwema na mafanikio katika usajili wa simu mtumie ujumbe huu na mwenzako pia .

KWA KAMPUNI ZA SIMU NI KUCHAGUA BIASHARA ZAO AU USALAMA WA WATEJA KAMA ZINAONA HAZIWEZI KUENDELEA NA UTARATIBU HUU KWA KUPOTEZA WATEJA ETC WATAFUTE NCHI WANAZOWEZA KUWEKEZA BILA ULINZI NA USALAMA KWA WANANCHI WA MAENEO HAYO HAPA KWETU NI MWIKO

HAYA NI MAONI YANGU

YONA F MARO
KILIMANJARO , TANZANIA
WWW.WANABIDII.NET
 
mzee uishaahidi KUACHA KABISA JF!...
naona siku zinavyozidi kwenda unaendelea kupingana na kauli ako
 
Ndugu, website ya TCRA Ipo kwa lugha ya kiingereza, itawasaidia vipi watanzania wengi ambao kiingereza kwao ni msamiati?
 
Njia ya rahisi zaidi ni kuwasiliana na huduma kwa wateja kwenye mtandao wako wa simu nadhani mitandao yote kwa Tanzania ni 100 au tembelea kwenye maduka yao na vituo vyao vingine kama ofisi ukishindwa huko ndio sasa unaweza kuwasiliana na TCRA lakini pia kuna shirikisho la watumiaji wa huduma za mawasiliano anuani yao sijui mpaka sasa hivi ila hilo nalo lingekuwa zuri sana
 
Shy na Usajili wa SIMU:

- TCRA walisema hawaongezi tena muda baada ya 30th June 2010: Waziri kutoka Bungeni kaongeza wiki Mbili (Shy unalisemaje hili?)

- TCRA hawana kitengo maalumu cha huduma kwa wateja: Piga simu pale kama una matatizo na usajili: hawana majibu hata!

- Makampuni ya simu vicheckesho: Vodacoma(piga: *106# jibu: ndugu mteja...hautaji kutupigia simu!) Zain(piga:*106# jibu: Your request could not be processed) e.t.c

- ni mambo ovyoovyo tu
 
- TCRA walisema hawaongezi tena muda baada ya 30th June 2010: Waziri kutoka Bungeni kaongeza wiki Mbili (Shy unalisemaje hili?)
Huyo waziri ndio msimamizi mkuu wa shuguli zote zinazohusu mawasiliano na teknologia nchini na wakati anatoa tamko hilo pale bungeni mkuu wa tcra alikwepo , costech na wakuu wengine wa masuala ya mawasiliano na teknologia wa vyuo na idara zingine za kiserikali - hata hivyo kwa kufanya hivyo imeonyesha kuna shida moja nayo ni kwa wananchi wenyewe kutokupokea suala la usajili wa namba zao kwa umakini na kuwekea umuhimu labda kutokana na elimu na masuala mengine ya mawasiliano na kampuni za simu ziliona zitapoteza wateja kiasi fulani endapo hizo line kweli zingefugwa siku hiyo

- TCRA hawana kitengo maalumu cha huduma kwa wateja: Piga simu pale kama una matatizo na usajili: hawana majibu hata!
Njia ya kwanza ni kuwasiliana na mtoa huduma wako kwa namba 100 watakupa huduma zote unazotaka au unaweza kutembelea maduka yao au ofisi zao ziliokaribu na eneo ulilopo kama unapata tabu basi ndio kuna tume ya mawasiliano hiyo au kuna ushirika wa watumiaji wa huduma za mawasiliano ambao anuani zao sina kwa sasa

- Makampuni ya simu vicheckesho: Vodacoma(piga: *106# jibu: ndugu mteja...hautaji kutupigia simu!) Zain(piga:*106# jibu: Your request could not be processed) e.t.c
Kwa sasa kampuni karibu zote unaweza kupata huduma ya kudhibitisha sema tatizo ni kwamba kuna baadhi ya watu waliosajiliwa hawajawekwa kwenye kumbukumbu za mitandao ya simu hizi kwahiyo inakuwa tabu kwa wao kuweza kuthibitishwa na hii nimeona haswa maeneo ya vijijini yaliyo mbali na miji ambapo msajili huenda mara 1 tu kwa wiki kwa ajili ya usajili

- ni mambo ovyoovyo tu
 
Back
Top Bottom