Usajili wa meli ulifanywa kwa njia ya mtandao (online) bila ya meli kwanza kukaguliwa

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Leo gazeti la Kulikoni limetoa mwanga kuhusu usajili wa utata wa meli za mafuta uliofanywa na serikali ya Zanzibar (SMZ), meli zinazodaiwa kumilikiwa na kampuni za Iran.


Tanzania imekabiliwa na vitisho vya vikwazo kutoka Marekani na EU iwapo itathibitika meli zilizosajiliwa ni za Iran na iwapo usajili huo hautafutwa m,ara moja.

Kuikoni limeandika kwamba ZMA hufanya usajili wa meli hizo (na nyinginezo) kupitia kampuni ya wakala wakala wake Philtex ya Dubai na kwamba usajili huo hufanywa kwa njia ya mtandao (online) bila ya meli zenyewe kukaguliwa na ZMA. Hivyo usajili hufanywa kutokana na taarifa/nyaraka zisizo sahihi kuhusu meli husika kwani kampuni hiyo husukumwa na masilahi yake Zaidi kuliko kitu kingine.

 
Sioni serikali itachomoka vipi hapa. Membe jana aliomba Marekani na EU wafanye uchunguzi iwapo meli ni za Iran, hivi ZMA haikufanya uchunguzi kwanza?

Kuna harufu ya ufisadi hapa na dili hii imewezeshwa na fisadi fulani, you know who! hakuna mwingine! Viongozi wetu wa serikali kila mara wanajikuta wanaendeshwa na yeye kwa pua.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom