Usajili wa magari kufanyika mara mbili kwa mwaka

This is just another example of a "leader", who is out of touch. Tanzania hakuna msongamano wa magari, infact Tanzania kuna upungufu wa magari na vyombo vya usafiri kwa ujumla. Kilichokuwepa Dar es Salaam and only in Dar es Salaam ni upungufu wa barabara. Kungekuwa na msongamano wa magari watu wasingegombania daladala posta kila siku mpaka akidamama na heshima zao wanalazimika kuruka madirisha! Ofcourse mtu anayeendeshwa na DFP hawezi kujua haya and unfortunately yeye ndiye anayepewa jukumu la kutatua the seemingly msongamano!!!
Kuzungumzia magari ya miaka mitano tu kupewa leseni ni vitimbi kama sio kejeli.
 
Kwani hatuna chombo maalumu (NGO or otherwise) cha kupigania HAKI za wananchi? Maana serikali ya CCM imeacha kabisa kujali maisha yetu.

Chombo kama kipo basi kiende mahakamani kipate restraining order dhidi ya Kombe na hao waliomtuma. Maana katumwa huyo, sio hivi hivi.

Hii njia ya kupigania haki kupitia mahakama inafanya kazi wakati mwingine. Nakumbuka kuna kipindi serikali ilitoa amri mabasi ya Dar Express yasimamishe huduma zake (baada ya ajali mbili). Kwa vile mkuu wa hayo mabasi si mtu wa mzaha, alikwenda mahakamani na akaweza kulazimisha serikali isiyasimamishe mabasi yake.

Hawa wabaya wetu wananunua magari kwa kutumia fedha za umma, na wanabadilishiwa mengine baada ya miaka michache tu. Sasa wanadhani hata sisi tunaotegemea fedha za jasho letu wenyewe tunaweza kufanya hivyo?

Ieleweke hivi: Sehemu kubwa ya sisi Watanzania, hata wale ambao tumefuta ujinga, haijawahi kuendesha gari lenye umri huo mnaotaka wa chini ya miaka 5. Si kwamba hatupendi, ni hatuwezi. Sasa na hiki kidogo tulichonacho mnataka kutunyima?

Ni rahisi kwa wale waliovimbisha matumbo kwa kutafuna fedha za umma kufungua vinywa vyao (in between eating and drinking), na kusema SASA TUENDESHE MAGARI YENYE CHINI YA MIAKA 5 TU. Kilichobaki ni sisi kupigania haki zetu mahakamani. Au tuendelee na kawaida ya "kuwaomba watuonee huruma"?

Mkuu wala usiwe na wasi wasi, haya ni maneno tu na sidhani kama kuna litakalotekelezwa. hapo Juu KJ alishasema kuwa alianza kuyasikia haya tangu 1995, hadi leo utekelezaji ZERO
 
Back
Top Bottom