Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usaili kipimo tosha kwa waomba kazi?

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by kilimasera, Jun 28, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,071
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  MIAKA nenda rudi, usaili umekuwa utaratibu maalum unaotumiwa kupima uwezo wa taaluma na utaalamu wa watu wanaoomba kazi.
  Pamoja na mfumo huu kuonekana kuwa kama kero kwa baadhi ya watu, usaili bado utaendelea kuwa njia muhimu ya kuchuja waomba ajira.
  Huu ukiwa uhalisia wa mambo, baadhi ya watu wanauliza, je usaili hasa ule wa mahojiano unatosha kuwa kipimo pekee kwa waomba ajira?

  Kipimo cha kazi
  Je usaili unapima uwezo wa taaluma na ujuzi wa kazi wa wahusika? Kuna wanaodai kuwa muda mchache unaotumiwa katika kuwafanyia usaili waombaji wa kazi hauwezi kuwa kipimo tosha cha kung’amua uwezo wa waomba kazi.
  Swalehe Abdurabi ni mhitimu wa Shahada ya Elimu ya Jamii kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anayesema usaili sio njia sahihi ya kupima uwezo wa mtu kiutendaji kwa lengo la kumpa ajira.
  Anasema tangu amalize chuo mwaka 2009, ameshafanya usaili zaidi ya mara 20 katika taasisi mbalimbali na kugundua kuwa njia hiyo haizingatii yale aliyosoma mtu chuoni na wakati mwingine maswali yanayoulizwa hayaendani na kazi anayoomba mhusika.
  “Kwanza ni kuna bias (upendeleo), na wanaangalia vigezo ambavyo siyo muhimu. Kwa mfano mtu anaenda kuomba kazi ya Ukandarasi wanataka uvae suti, kigezo ambacho hakitaweza kuonyesha uwezo wako wa kazi,” anaeleza na kuongeza:
  “Wewe unakuta kuna nafasi moja ya kazi, mnaitwa zaidi ya watu 500 kufanyiwa usaili na wakati huo wengine mnatoka mikoa ya mbali. Unakuja huku unafanyiwa usaili kwa dakika tano, hivi kweli kuna haki hapo, na wakati huo wanajua kabisa kuna kuna mtu wao wamemuandaa kuchukua nafasi hiyo.’’
  Abdurabi anaungwa mkono na Mary Ngelula. Mfanyakazi katika kampuni ya mafuta ya EOC iliyopo Tabata jijini Dar es Salaama anayesema ubora wa mwajiriwa hauwezi kupimwa kwa usaili hasa ule wa mazungumzo kama ilivyozoeleka.
  “Siwezi kukubaliana na mtu anayesema usaili ni kipimo tosha maana sifa kubwa ya mfanyakazi lazima awe na nidhamu, sasa utamtambuaje kwa mahojiano? Kwa mtu anayetafuta kazi anaweza kuwa mnyenyekevu wa hali ya juu katika usaili ,lakini baadaye anaweza kubadilika,’’ anaeleza.

  Kwa mtazamo wake, Ngelula anasema njia bora ya kumpima mtu ni ile ya kumpa kazi kwa vitendo kwa muda usiopungua miezi mitatu.Ana wasiwasi kuwa mtu anaweza kufanya vizuri katika usaili, lakini akashindwa kuhimili vishindo vya kazi.

  Lakini wapo wanaotetea usaili kama kipimo cha kuwachuja waomba kazi akiwemo Ofisa Utawala wa kampuni ya EOC ,Magdalene Emmanuel anayeeleza kuwa usaili ni njia bora ya
  kumtathmini mtu na kuelewa uwezo wake katika utendaji.

  Hata hivyo ana shaka na matumizi ya lugha za kigeni hususan Kiingereza katika matukio mengi ya usaili akisema kuwa lugha hiyo imekuwa kikwazo kwa waomba kazi hata wale wenye uwezo na ujuzi stahiki katika kazi wanazoomba.

  “Naamini kwamba usaili ni muhimu sana. Kuna mtu mwingine hawezi kuongea, lakini ni mtendaji mzuri wa kazi na mwingine ana uwezo wa kuongea, lakini si mtendaji mzuri….”anasema.

  Aidha uzoefu unaonyesha usaili umekuwa ukitumika kama njia ya kubaini maarifa uwezo, uzoefu wa waomba kazi. Lakini pia kujua kama anayeomba kazi ana sifa zinazorandana na mahitaji ya wale wanaomfanyia usaili.

  Usaili na wahitimu wa Tanzania
  Kwa waombaji kazi wengi wa Kitanzania hasa wahitimu, lugha na mbinu za ufanyaji usaili vimekuwa vikiwapiga chenga.Hii ni kwa sababu mfumo wa elimu wanaopitia hauwaandai kikamilifu kuhimili misukosuko ya soko la ajira ikiwemo namna ya kujiandaa na usaili wanapomaliza masomo.
  “Katika interview (usaili), lugha ni ya kigeni, haitoshi pale panahitaji ufundi wa kukabiliana na maswali. Kuna mambo kama jinsi ya kukaa, kuzungumza. Je, haya yapo katika mitalaa? ,” anasema Bakari Athumani ambaye ni mwalimu mstaafu anayeishi Boko jijini Dar es Salaam.
  Bakari anaongeza kusema kwa kuhoji: “Tuweke kando mitalaa, vipi shule zetu zinawafundisha wanafunzi masuala ya usaili, kujiamini na mambo mengine muhimu katika maisha? Mambo mengine sio lazima yawepo katika mtalaa, kwani mtalaa si jalala la kuweka kila kitu.
  “ Walimu shuleni wanaweza kabisa kuendesha sessions (vipindi) hata mara chache kwa mwaka, wakawaeleza wanafunzi wao mambo mbalimbali ya kimaisha na jinsi ya kuyakabili……Usaili nao ni sehemu ya maisha, wanafunzi wafundishwe jinsi ya kufaulu katika usaili kwani ndicho kipimo cha kupata kazi.’’
   
 2. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 9,834
  Likes Received: 517
  Trophy Points: 280
  kazi kweli kweli.
   
 3. pomo

  pomo JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 265
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  dah,ndo naingia kwenye jf kwa mara ya kwanza mkuu, usaili ni kweli kipimo tosha ila ndo hivyo huwa wanachukuliwa kamlete. kama wakichukuliwa clean kwenye usaili ni kipimo kizuri si kuna miezi ya probation?
   
 4. pomo

  pomo JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 265
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  dah,ndo naingia kwenye jf kwa mara ya kwanza mkuu, usaili ni kweli kipimo tosha ila ndo hivyo huwa wanachukuliwa kamlete. kama wakichukuliwa clean kwenye usaili ni kipimo kizuri si kuna miezi ya probation?<BR>
   
 5. pomo

  pomo JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 265
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sina cha kuongezea mkuu
   
 6. A

  Agrodealer Senior Member

  #6
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 108
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwa kweli usail ni uzushi mtupu, kwani wanaohitimu hasa wanaotoka katika familia duni hasa za vijijini wamekua wakitumia gharama nyingi kwenye usaili bila mafanikio kitu ambacho kinawpelekea kukata tamaa na kuona elimu si kitu zaidi ya kuwa na mareferee sehemu unayoomba kazi
  vilevile mtu analazimika kujiingiza kwenye utoaji rushwa wakati wa usaili ilimradi tu apate kazi
   
 7. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 15,388
  Likes Received: 1,601
  Trophy Points: 280
  Hukua na haja ya kukopi thread yote kama ilivyo kisha ukakiweka ki-comment uchwara kiivyo,unatuongezea mzigo wa ku-scroll down wakat ulichoandika hakina mashiko kivile
   
 8. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 9,834
  Likes Received: 517
  Trophy Points: 280
  jinyonge basi..
   
 9. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,846
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Ukiomba kazi ambayo si fani/field yako ndg yangu kila utakachokuwa unaulizwa utakiona ni kigeni lakini kama utaomba kwenye fani/field yako(uliyosomea) ndg yangu utapeta tu. Siyo we ni umesomea Mahusiano kazini(industrial relations) unaenda kuomba kazi ya Uhandisi wa Viwanda(industrial engineering) utachekwa ndugu.
   
 10. R

  Renald Member

  #10
  Jun 29, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  usaili unaweza ukawa sahihi kama wakizingatia taaluma ya m2 husika.mfano kama m2 ni mkandarasi apewe usaili kwenye mazingira yake ya kazi na apewe kaz ya kikandarasi
   
 11. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 9,834
  Likes Received: 517
  Trophy Points: 280
  inategemea na kichwa cha m2 mkuu,niliwah kushuhudia interview flan,kazi ilyotangazwa ilikua ni uhasibu,dogo m1 frm chuo flani cha hapa nchini ambaye ana degree ya uhasibu kaulizwa swali rahisi 2 la fan yake,kaanza kujiuma uma,thn kaja dogo mwingne kasoma kilimo kaulzwa swali lile lile akaweza kujbu,so mwajiri hakua na la kufanya zaid ya kumchukua yule wa kilimo na kumpa job training na maisha yakaendelea.
   
 12. LUSAJO L.M.

  LUSAJO L.M. JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 207
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wanajamii,Hapa nadhani katika mada hii kuna vitu viwili vimechanganywa ambavyo laiti kama vingetenganishwa tungekuwa na mada moja ya maana sana ambayo ingepata michango mingi yenye manufaa kwa wengi. Ni vitu ambavyo vinaenda sambamba lakini haviwezi kukaa pamoja. Kuna watu wamechangia wakisema kwamba usaili hauna maana na so kigezo cha muhimu katika kuajiri mtu na wakati huo huo tumejumuisha na kusema kwamba usaili mara nyingi ni kama geresha kwani kwa kiasi kikubwa mtu anaetarajiwa kuchukua kazi husika anakuwa ameshapangwa na kwamba usaili wote unafanyika kama kukamilisha 'ratiba' tu na sio kwa ajili ya kuchagua yule anaefaa katika wazuri walioomba nafasi ya kazi. Mada hizo mbili ni "Umuhimu wa Usaili katika kupata kazi" na "Mfumo wa kuajili kwa upendeleo bila kujali uwezo wa watu."Usaili ni hatua ambayo inatumika kutathaminisha uwezo wa msailiwa na mwajiri kabla ya kupewa ajira anayotarajiwa katika kampuni au taasisi. Katika hatua ya usaili mwajiri anatarajiwa kuamua kama msailiwa anafaa kwa ile kazi ambayo ameomba. Hii ni hatua ambayo inatangulia maamuzi ya kuajiri na inatumika kuwatathmini walioomba kuajiriwa katika nafasi husika. Usaili umekuwa sio njia ya kuaminika sana kumpata mtu muafaka kwa ajili ya kazi lakini ni moja kati ya zana muhimu sana katika kutathmini na kuchagua mtu anaefaa kwa ajilia ya kazi fulani katika kampuni, shirika au taasisi.Katika maandalizi ya kuajiri mtu kwa ajili ya kazi fulani usaili hauanzii na pale msaili na msailiwa wanapokutana kwa dakika tano, kumi au saa moja kuulizana maswali bali huanzia pale mtu unapowakilisha maombi yako ya kazi kwa ajili ya nafasi husika. Na moja ya kazi ya usaili ni kujaribu kujua kama yale uliyowakilisha katika maombi yako ya kazi ndio ambayo unayamaanisha hata katika maongezi ya ana kwa ana. Pia ukiachana na uwezo wa mtu na uzoefu katika kazi husika, usaili pia unatumika kujaribu kuangalia namna ambapo msailiwa anaweza akafanya kazi katika mazingira ya kampuni au shirika husika, pia namna ambavyo anashirikiana na wenzake sehemu za kazi na nje, kwani ikumbukwe kwamba mtu unapoajiriwa na kuanza kazi mpya utakutana na watu tofauti wenye huka tofauti kwa hiyo ni muhimu sana kujua ni jinsi gani unaweza kuyamudu mazingira hayo huku ukitilia mkazo zaidi ustawi wa kampuni, shirika au taasisi husika.Kuna mengi ya kuandika katika hii mada lakini naomba kumaliza tu kwa kusema usaili pekee sio kipimo tosha kwa waomba kazi kupewa kazi lakini wakati huo huo naomba ifahamike kwamba usaili (interview) ni sehemu ndogo sana ambayo maafisa wa rasilimali watu/waajiri wanaitumia katika kuchagua na kuamua ni nani ndio anafaa kupewa kazi ambayo imetangazwa. Pia usaili ni njia ambayo mwombaji wa kazi anaweza jua mengi husiana na kazi aliyoomba na shirika/Taasisi ambayo ameomba kazi. Hatua nzima ya kuajiri mtu inaanzia na haja ya kuajiri mpaka mwisho kwenye kuajiri baada ya kufanya uchaguzi wa yule bora zaidi kati ya walio bora.
   
Loading...