Usaili Jeshi la Polisi

kiye

Senior Member
Apr 28, 2012
117
24
Habari wana JF, hivi kuna mtu anajua tetesi zozote kuhusu usahili wa nafasi za kwenda polisi zilizotangazwa mwezi wa saba? Maana niliona tangazo kwa ajili ya form six na four wakiitwa kwenye usahili vp kuhusu watu wa vyuo, wamepotezea ama bado tu?
 
Mmh! Unajua tatizo nn, wapo kimya mnoo! Kama wameamua kutu delete ni bora waseme watu waangalie utaratibu mwingine bhana! Maana hii ngoja ngoja inaumiza matumbo!
 
Wanachukua toka jkt this time,kama unataka nafasi hizo anzia jkt ndugu yangu
 
Habari wana JF, hivi kuna mtu anajua tetesi zozote kuhusu usahili wa nafasi za kwenda polisi zilizotangazwa mwezi wa saba? Maana niliona tangazo kwa ajili ya form six na four wakiitwa kwenye usahili vp kuhusu watu wa vyuo, wamepotezea ama bado tu?

kwema! vuta subra bado wanafanya usahili wa six na four kwa awamu ya pili ile ya kwanza ilifanywa na makamanda wa mikoa wale waliopenya wanafanyiwa usahili wa pili na maofsa toka makao makuu ya jeshi la polisi na zoezi linaendelea mikoani toka wiki yote hii, wakimaliza ndo wanakuja kwenu graduate.
 
kwema! vuta subra bado wanafanya usahili wa six na four kwa awamu ya pili ile ya kwanza ilifanywa na makamanda wa mikoa wale waliopenya wanafanyiwa usahili wa pili na maofsa toka makao makuu ya jeshi la polisi na zoezi linaendelea mikoani toka wiki yote hii, wakimaliza ndo wanakuja kwenu graduate.

Huo usail unafanyika kwa taratibu zipi kaka , tuibie maujuzi kidogo bhasi
 
Wanachukua toka jkt this time,kama unataka nafasi hizo anzia jkt ndugu yangu

Kaka bajeti ilipangwa wew na wizara mda mrefu tu ina mana hao jkt hawakuiona hadi wizara ikatangaza nafasi awamu ya kwanza form 4 na 6 na usaili unaendelea, pia awamu ya graduate , ina mana wamewafanya watz matoy au wew una mana gan ? Think before bana
 
Kama nilivyokwisha kusema kwenye uzi mwingine kama huu. Usiponde wala kubishana kwa kile ulichoambiwa, chamsingi kichukue icho ulichosikia kwa asilimia kadhaa na usikatishwe tamaa chamsingi nikuendelea kuvuta subira maana michakato inaendelea kwa 4 na 6! Vyombo vya ulinzi na usalama uwa vinakua na uitaji wa askari wajuzi na wasio wajuzi kwa kipindi husika na michakato wakati mwingine ua inaanzia jkt na kufuatia mtaani, au wanaweza pia kuchukua mtaani moja kwa moja au wakachukua jkt peke yake! Hivyo kama wameitaji watu kutoka mtaani basi kaeni mkijua wao si wajinga, tusikariri kwamba ni lazima kupita jkt!
 
Asante wakuu, nafikiri tuendelee kuwa na subira maana kuna maelezo kuwa form 6 n 4 hawajamalizana nao. Nakubaliana na jamaa aliyesema mpaka nafasi imetangazwa ina maanisha wizara husika ilitengewa bajeti kwa sula husika.

Natamani niingie kwenye kundi hili maana wananch wana malalamiko mengi kuhusu jeshi la polisi kwamba limekosa weredi na ubinadam kwa wananchi, naamini kwa kuongeza idadi ya wasomi
katika jeshi hili kutaongeza ufanisi mkubwa na kupunguza malalamiko kwa wananchi ingawa penye ulazima wa kutumia nguvu lazima zitumike hata kama baadhi watalaum lakini kama jeshi lazima liangalie maslahi ya wengi na muongozo wa utawala wa sheria!!
 
Lakin tukiwa tunasubiri interview ya form 4 na form 6 imalizike naona wangetoa majina ya waliochaguliwa kufanyiwa interview ili watu wasikate tamaa kusubiri
 
kwema! vuta subra bado wanafanya usahili wa six na four kwa awamu ya pili ile ya kwanza ilifanywa na makamanda wa mikoa wale waliopenya wanafanyiwa usahili wa pili na maofsa toka makao makuu ya jeshi la polisi na zoezi linaendelea mikoani toka wiki yote hii, wakimaliza ndo wanakuja kwenu graduate.

Asante kwa maelezo mazuri mkuu, wacha tuwe na subira!
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
(Jeshi la Magereza)


TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA

Jeshi la Magereza Tanzania Bara linatangaza nafasi za Mafunzo ya Awali ya Askari Magereza yatakayoendeshwa Chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Mbeya. Waombaji wa nafasi hizo wanatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-

MASHARTI YA KUAJIRIWA:

1. JINSI:​Mvulana au Msichana ambaye hajawahi kuoa
au kuolewa na asiwe na mtoto

2. URAIA:​Awe Raia wa Tanzania Bara

3. UMRI:
(a) Wahitimu wa Shahada:​Awe na umri wa kati ya miaka 18 na 28
(b) Wasio na Shahada:​Awe na umri wa kati ya miaka 18 na 24

4. UREFU:

(a)​ Wavulana:​ Wawe na urefu usiopungua Sentimeta 170.2 au Futi
​ 5 na inchi 7
(b) Wasichana: Wawe na urefu usiopungua Sentimeta 167.64 au
Futi 5 na inchi 4
​
5. SIFA NYINGINEZO:
i) Awe amehitimu Elimu yake kati ya Mwaka 2012 na 2014
ii) Awe na Afya nzuri iliyothibitishwa na Daktari anayetambuliwa na Serikali
iii) Awe hajawahi kushtakiwa wala kupatikana kwa kosa lolote la jinai
iiii) Awe na tabia na mwenendo mzuri
v) Awe hajawahi kuajiriwa mahali popote Serikalini

7. ELIMU:

(a)​Wenye Shahada katika Fani au Taaluma zifuatazo:
(i) Shahada ya Sheria (Laws)
(ii) Utekelezaji wa Sheria (Law Enforcement)
(iii) Takwimu (Applied Statistics)
(iiii) Uchumi na Mipango (Economic Planning)
(v) Mazingira (Environmental Science and Management or Geography and Environment Studies)
(vi) Usanifu Majengo (Architecture)
(vii) Ukadiriaji Majengo (Building Economics)
(viii) Mipango na Usimamizi Miradi (Project Planning and Management)
(ix) Uhandisi wa Umeme (Electrical Engineering)
(x) Uhandisi wa Mitambo ya Kilimo (Agricultural Engineering)
(xi) Tiba ya Mifugo (Veterinary Medicine)
(xii) Misitu (Forestry)
(xiii) Uchumi Kilimo (Agronomy)
(xiiii) Bima (Insurance)
(xv) Uhasibu na Usimamizi wa Vyama Ushirika (Cooperative Management and Accountancy)
(xvi) (Project Planning and Management)
(xvii) Uhandisi Mazingira (Environmental Engineering)
(xviii) Sayansi ya Kompyuta (Computer Science)
(xix) Udaktari wa Binadamu (Doctor
of Medicine)
(xx) Ualimu wa Masomo ya Sayansi kama Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati
(xxi) Ualimu wa Masomo ya Biashara na Kifaransa (Commercial Subjects, Economics and French)
(xxii) Ukutubi (Library and Information Studies)
(xxiii) Mahusiano (Public Relations)
(xxiiii) Biashara na Masoko (Commerce in Marketing)

(b)​WASIO NA SHAHADA
1.1: Wenye Stashahada (Diploma) toka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali katika Fani/Taaluma zifuatazo:-
(i) Ukutubi (Library)
(ii) Uchumi na Mipango (Economic Planning)
(iii) Bima (Insurance)
(iiii) Uhasibu na Usimamizi wa Vyama Ushirika (Co-operative Management and Accountancy)
(v) Mipango na Usimamizi Miradi (Project Planning and Management)
(vi) Utabibu (Clinical Medicine)
(vii) Uuguzi (Nursing)
(viii) Maabara (Laboratory Technician)
(ix) Mazoezi ya viungo (Physiotherapy)
(x) Uandishi wa Habari (Journalism)
(xi) Ufundi Magari (Automobile Technician)
(xii) Ujenzi (Civil Engineering)
(ix) ​Umwagiliaji (Irrigation)
(x) Mitambo ya Kilimo (Agro-Mechanics)
(xi) Umeme (Electrical Engineering)
(xii) Usanifu Majengo (Architecture)
(xiii) Ushauri Nasaha (Counseling and Guidance)
(xiiii) Uhandisi Mitambo (Mechanical Engineering)
(xv) Sanaa na Muziki (Fine and Performing Arts)
(xvi) Ualimu wa masomo ya Biashara, Uchumi na Kifaransa

1.2:​Wenye Astashahada/ Cheti cha Majaribio ya Ufundi katika Fani/Taaluma zifuatazo:-
(i) Uhandisi Maji (Water Engineering)
(ii) Ujenzi (Masonry)
(iii) Ufundi Magari (Motor Vehicle Mechanics)
(iiii) Umeme wa Magari (Auto-Electrical Engineering)
(v) Waunganishaji Nondo (Steel Fixing)
(vi) Useremala (Carpentry and Joinery)
(vii) Bomba (Plumbing and Pipe Fitting)
(viii) Rangi (Spray and Painting)
(ix) Ushonaji (Tailoring)
(x) Utengenezaji Sabuni (Soap Making)
(xi) Ufumaji (Embroidery)
(xii) Kutengeneza viatu (Shoe-Making)
(xiii) Maabara (Laboratory Technician)
(xiiii) Uhitasi (Secretarial Studies with Computer Knowledge)
(xv) Muziki na Utamaduni (Performing Arts and Music)
(xvi) Uuguzi na Ukunga (Nursing and Midwife)
(xvii) Utabibu Usaidizi (Clinic
al Assistant)

ZINGATIO:
Waombaji wa nafasi hizi wahakikishe wanazingatia masharti yote yaliyotajwa hapo juu. Upungufu au udanganyifu wowote utakaojitokeza kwa kutotimiza masharti yaliyotajwa hapo juu utasababisha maombi kutopokelewa na ikigundulika baada ya ajira mhusika atasitishwa mafunzo, kuachishwa kazi na kufikishwa Mahakamani.

8. NAMNA YA KUTUMA MAOMBI:

Waombaji wote watume maombi yao moja kwa moja kwa:-

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA,
MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA,
S.L.P 9190,
DAR ES SALAAM.

a) Barua zote za maombi ziambatane na nakala za vyeti vyote vya elimu, ujuzi, Cheti cha kuzaliwa mwombaji na picha ndogo ya hivi karibuni ya mwombaji (Passport size photograph). Vyeti halisi na halali vitatakiwa kuoneshwa wakati wa usaili. Hati za matokeo ya mitihani (Results Slip/ Statement) hazitakubaliwa isipokuwa kwa wahitimu ambao vyeti vyao halisi havijatolewa na Vyuo husika pekee.

b) Watakaofanikiwa kuitwa kwenye usaili watajulishwa kupitia katika Tovuti ya Jeshi la Magereza (www.magereza.go.tz), Magazeti na katika Mbao za matangazo zilizopo kwenye Ofizi za Wakuu wa Magereza wa Mikoa na Bwalo Kuu la Maafisa wa Magereza lililopo Ukonga Dar es salaam.

c) Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15 Oktoba, 2014........(ZINGINE HIZI HAPA,KAZI KWENU SASA)



J. C. Minja
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA
19 SEPTEMBA, 2014
 
Back
Top Bottom