Usafiri wa reli ya kati hatarini kusimama

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234




KAMPUNI ya Reli Tanzania (TRL), imesema kuna uwezekano wa kusitisha huduma za kusafirisha wa abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma, katika siku za usoni na kwamba hatua hiyo inatokana na kukosekana kwa mabehewa.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam, na Meneja Biashara wa TRL, Hassan Shaaban, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema tatizo la kukosekana kwa mabehewa ya abiria, ni kubwa katika kampuni hiyo na kwamba kuna uwezekano wa kuathiri utoaji wa huduma za usafiri wa treni kati ya Dar es Salaam na Kigoma.

Alisema tatizo hilo linatokana na kuharibika kwa mabewa kunakochangiwa na uzito wa mizigo ya abiria.

"Utaratibu ni kwamba abiria wa daraja la tatu wanastahili kuwa na mizigo isiyozidi kilo 20 kwa kila mmoja, na daraja la pili kilo 40 wakati wale wa daraja la kwanza, wanaruhusiwa kuingia na mizigo isiyozidi kilo 70 ambayo hailipiwi," alisema Shabaan.

"Hata hivyo unaweza kukuta abiria mmoja amezidisha uzito wa mzigo hadi kufikia kilo 100, jambo linalosababisha mabehewa kuzidiwa uwezo,"alisema.

Alisema pia kumekuwa na tatizo la kuzidi kwa idadi ya abiria kwenye mabehewa, jambo linalochangia kuyafanya yachakae kwa haraka.

"Kwa mfano,behewa la daraja la tatu linabeba zaidi ya abiria 160 badala ya 80 wanaoruhusiwa na kampuni. Hali hii ikiendelea inaweza kusababisha ajali mbaya na watu kupoteza maisha," alisema.

Alisema hali pia inasababisha hasara isiyokuwa ya lazima katika matengenezo ya mabehewa..

Alisema inaonekana abiria wanaozidi, wanapandia katika stesheni kama ya Pugu, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, ambako hakuna udhibiti kama ilivyo katika makao makuu ya kampuni hiyo.

"Hapa makao makuu tunawadhibiti kwa kuwa kuna geti ambalo abiria hupita, asiye na tiketi hapiti, lakini kwenye vituo vya njiani hakuna geti, abiria anaingia kwenye gari moshi bila kizuizi huku akiwa na mizigo mikubwa lakini akiwa hana tiketi," alisema.

Meneja huyo alisema kisheria, abiria anapopanda kwenye gari moshi akiwa hana tiketi, hawezi kushushwa kwenye kituo chochote, bali analipa nauli na faini, kiasi hicho cha fedha.

Alisema hata hivyo kiasi hicho bado ni kidogo ikilinganishwa na bei zinazotozwa kwenye mabasi.

"Kwa hiyo wanaona bora wavunje sheria na kutozwa faini kwani gharama zitakuwa ndogo zikilinganishwa na zinazotozwa kwenye mabasi ya abiria, haya yote yanatokea kutokana na TRL kuwa na safari moja ya abiria kila wiki, hivyo watu wengi kuhitaji usafiri," alisema.

Kutokana na hali hiyo, uongozi wa kampuni hiyo umeamua kuanzia wiki ijayo, kuwa mizigo yote itakayozidi kwa mujibu wa viwango vilivyowekwa haitasafiri kwenye mabehewa ya abiria.

Kwa mujibu wa meneje huyo, badala yake, mizigo itakayozidi itapelekwa kwenye ofisi ya vifurushi ambako itapimwa na kulipiwa, kisha kusafirishwa kwenda inakokusudiwa na mabehewa ya mizigo.


Chanzo: Mwananchi.

My Take;
Hili swala JK kasha lizungumzia katika kampeni zake akiwa Kigoma, au alilikacha kwa kutokuwa na maelezo? Ningemwomba Dr Slaa akiwa katika kampeni ya maeneo husika (kandokando mwa reli ya kati) Dodoma, Tabora, Manyoni, Urambo, etc awaambie wananchi kwa nini wanataabika na usafiri kutokana na ufisadi wa viongozi wa CCM. Aingie kwa undani zaidi katika kashfa hiyo ya TRL – ambayo bila sdhaka yoyote ni kubwa kuliko zote zilizowahi kutokea katika historia ya nchi hii. Na asichoke kulielezea akiwa katika kile eneo.
 
Wana JF,

JK ana ahidi kujenga viwanja vya ndege huku Reli ya kati, kwenda Arusha hadi tanga zote zime simama sasa hapo kweli twapoteza mwelekeo jamani au Reli ya kati iliuliwa makusudi ili wannchi wasimfuate mjomba Dar???
 
Si anawajengea uwanja wandege na ata ifanya kigoma kuwa dubai? Sasa wasiwasiwa nini?

Waendelee kusubiri upembuzi yakinifu uanze awamu hii then awamu ya lowasa watatafuta mkandarasi then awamu ya rostam watajenga.
 
Si anawajengea uwanja wandege na ata ifanya kigoma kuwa dubai? Sasa wasiwasiwa nini?

Waendelee kusubiri upembuzi yakinifu uanze awamu hii then awamu ya lowasa watatafuta mkandarasi then awamu ya rostam watajenga.

.....Na Manji ndiyo atakayefungua miradi miradi hiyo?
 
Back
Top Bottom