Usafiri wa bus mbezi_morogoro rd

mfwakwa

Member
May 31, 2010
40
0
Nimeshangazwa na usafiri wa mbezi. Nilikuwa nasafiri kutoka posta mpya kuelekea mbezi kwa msuguli, nilishangaa nilipofika kituo cha posta majira ya saa 11.30 nilikuta watu wamefurika sana; bahati nzuri akatokea abiri mmoja akanishauri nihame nikapandie bus kituo cha akiba then nirudi posta halafu mbezi; nilikubali nikaondoka naye hadi akiba; pale pia kulikuwa na abiria wengi sana; nikaamua kupanda bus ya ubungo inayoingia kwanza posta; nililipa 250/= then posta nikalipa tena 250/= hadi ubungo. nilipofika ubungo nilishangaa zaidi bus nyigi zinazoanzia ubungo zinaishia kimara. ok niliingia kwenye bus ya ubungo-msata nilitoa 1000 nikamweleze konda naelekea mbezi; alifoka na kuniambia gari ya shamba hii ila inaenda kulala inaisha kimara; nikamwambia well kama itaendelea nitaendelea kama itaishia kimara sawa, alichukua 250/= tulipofika kimara pale napo watu walikuwa wengi sana alifika pale akashusha watu wote then akaaza safari upya uzuri na mimi nilifanikiwa kuingia nikalipa tena 250/ kutoka pale ile gari ilienda hadi mbezi tuliposhuka akachukua tena watu pale kuelekea kibamba kwa 200/ SAFARI KUTOKA POSTA HADI KIBAMBA 250AKIBA+250UBUNGO+250KIMARA+250MBEZI+200KIBAMBA=1200/= anayepand bus ni mshahara wa kima cha chini; KWELI ATAFIKA?:confused2:
 
Maisha bora kwa kila mtanzania ndo hayo Mfwakwa..........................
 
Sasa kweli kasi mpya, Mtu wa Kima cha chini aweze wapi maisha haya bila kuwa na cha pembeni? Hata hiyo pikipiki yenyewe inahitaji mafuta ambayo kwa sasa yamesimama kwenye 1700 ukitumia lita mbili kwa siku, ni sawa na lita 44 kwa siku 22 za kazi ona sasa mshahara usivyotosha. TUCTA fanyeni mabo hapo hapajatulia.
 
mfwakwa,

hayo maisha mbona tumeyazoea sasa :

Kutoka Posta hadi Mbagala Rangi Tatu - unapanda mabasi manne (250 x 4)
Kutoka Posta hadi Bunju - Magari matatu (au Mawili kama utapanda ya Bagamoyo = 300 +1600)
Kutoka Posta hadi Gongo la Mboto - Magari manne au matano (250 x 4/5)
Kutoka Posta hadi Tabata (Mawenzi/Chang'ombe/Kinyerezi/Segerea) - Magari manne (250 x 4)

List inaendelea

Hayo maeneo niliyokutajia ni "one-way" kwahiyo ukitaka kupata gharama halisi zidisha mara mbili kwa siku mara idadi ya tegemezi (dependants)!
 
...kuna mengi yanayochangia katika hili lakini nadhani kubwa ni hili la kumruhusu kila mwenye basi lake kuwa msafirishaji wa abiria jijini. Mwanzisha thread amesema kuwa 'Kondakta akafoka', hii ni kutokana na hili ninalolisema. Usafirishaji wa jiji kama la Dar ulitakiwa ume ni Kampuni rasmi kwa Mfano UDA, kama watu wasingeihomola. Ingesaidia sana kupunguza matatizo ya Wahuni wanaokatisha ruti na wafanyakazi wasiokuwa na adabu kwa watu wanaowapa kula yao! kibaya zaidi ni kuwa hao hao wenye mamlaka ya kuondoa uozo huu ndio hao haowenye kumiliki hayo mabasi yanayokatisha ruti. Ni a vicious circle. Poor We!
 
Nimeshangazwa na usafiri wa mbezi. Nilikuwa nasafiri kutoka posta mpya kuelekea mbezi kwa msuguli, nilishangaa nilipofika kituo cha posta majira ya saa 11.30 nilikuta watu wamefurika sana; bahati nzuri akatokea abiri mmoja akanishauri nihame nikapandie bus kituo cha akiba then nirudi posta halafu mbezi; nilikubali nikaondoka naye hadi akiba; pale pia kulikuwa na abiria wengi sana; nikaamua kupanda bus ya ubungo inayoingia kwanza posta; nililipa 250/= then posta nikalipa tena 250/= hadi ubungo. nilipofika ubungo nilishangaa zaidi bus nyigi zinazoanzia ubungo zinaishia kimara. ok niliingia kwenye bus ya ubungo-msata nilitoa 1000 nikamweleze konda naelekea mbezi; alifoka na kuniambia gari ya shamba hii ila inaenda kulala inaisha kimara; nikamwambia well kama itaendelea nitaendelea kama itaishia kimara sawa, alichukua 250/= tulipofika kimara pale napo watu walikuwa wengi sana alifika pale akashusha watu wote then akaaza safari upya uzuri na mimi nilifanikiwa kuingia nikalipa tena 250/ kutoka pale ile gari ilienda hadi mbezi tuliposhuka akachukua tena watu pale kuelekea kibamba kwa 200/ SAFARI KUTOKA POSTA HADI KIBAMBA 250AKIBA+250UBUNGO+250KIMARA+250MBEZI+200KIBAMBA=1200/= anayepand bus ni mshahara wa kima cha chini; KWELI ATAFIKA?:confused2:
hahaha!kumbe mfwaka unakaa mbezi eeh!?
sasa tukutane pale SUN-SET jioni ya ijumaa tuyajadili haya matatizo huku tukizitiririsha
 
Tatizo la usafiri wa Tz hasa Dar ni biashara huru iliyokaa mfumo wa kiholela mnoo
 
Back
Top Bottom