Elimu ya Kinywa: Usafi wa meno na kinywa kwa ujumla, sababu, kinga na tiba za harufu mbaya

Listerine mara nyingi. Hasa nikifululiza ndo inakuwa shida

Huwa nasoma maelezo

Mouthwashes zipo za aina mbalimbali.

Zipo za watu wenye sensitive gums, sensitive teeth, zilizo less intense na kadhalika.

Jaribu kutafuta iliyo less intense na mahsusi kwa hilo tatizo lako.

Zipo. Ni kujua wapi tu zinapatikana.
 
Mouthwashes zipo za aina mbalimbali.

Zipo za watu wenye sensitive gums, sensitive teeth, zilizo less intense na kadhalika.

Jaribu kutafuta iliyo less intense na mahsusi kwa hilo tatizo lako.

Zipo. Ni kujua wapi tu zinapatikana.
Listerine cool mint iko intense sana. Nitajaribu kutafuta ambazo kidogo zipo less intense, kama unavyosema, nadhani ndizo zinazonifaa.

Asante kwa maelezo ya kina.
 
Listerine cool mint iko intense sana. Nitajaribu kutafuta ambazo kidogo zipo less intense, kama unavyosema, nadhani ndizo zinazonifaa.

Asante kwa maelezo ya kina.

Kwa mfano, kuna Listerine Zero ambayo haina alcohol na ipo less intense.

77848%20ZERO.png


Pia unaweza kutumia zile za watoto...nazo ziko vizuri. Haziunguzi mdomo.

Crest_Pro_Health_Jr_Star_Wars_Mouthwash_Details.png
 
Nashukuru sana kwa uzi huu...nimengoa jino langu 1 gego kwa uzembe jino limetobokaaa ni mekaa nalo hadi kwenda kwa Dr kuziba alifai tena..root canal dr alisema pia halifaiiii coz wadudu walikula .yan ukiona kutoboka kwenyewe ni kishimo kifogo pemben ya jino..ila maumivu na mateso niliyoyapata jaman tunzeni...tutunze sana meno yetu kama ushauri ulivyotolewa hapo juu na wadau mbalimbali
 
Nashukuru sana kwa uzi huu...nimengoa jino langu 1 gego kwa uzembe jino limetobokaaa ni mekaa nalo hadi kwenda kwa Dr kuziba alifai tena..root canal dr alisema pia halifaiiii coz wadudu walikula .yan ukiona kutoboka kwenyewe ni kishimo kifogo pemben ya jino..ila maumivu na mateso niliyoyapata jaman tunzeni...tutunze sana meno yetu kama ushauri ulivyotolewa hapo juu na wadau mbalimbali
Nami nikushukuru kwa kuuona umuhimu wa huu uzi.
 
Nna jino langu nshaziba mara 2 af risasi inabomoka, natamani kuling'oa ila sipendi, na root canal pia siitaki, nishauri
 
UTAKUWA ulisha wahi sikia mambo mengi mbalimbali yenye imani ya kutisha kuhusiana na afya ya kinywa na meno ,nimeandaa baadhi ya mambo na ukweli wake naomba uongeze za kwako ambazo ulisha wahi sikia sehemu,kuhusia na afya ya kinywa na meno tusharee.

IMANI POTOFU KUHUSU KUHUSU AFYA YA KINYWA NA MENO.

1.IMANI POTOFU;

KUKATA KIMEO (TRADITIONAL OVULECTOMY)

UKWELI ;Kimeo (ovula)hakikatwi ,ila huwa na maambukizi ya bacteria hivyo mgonjwa anatakiwa kutibiwa kwa dawa ,

2.IMANI POTOFU

MENO YA PLASTIC HUTOLEWA KWA IMANI ZA KIMILA

UKWELI; meno ya plastic kwenye mwili wa binadamu , neonatal teeth ( mtoto anazaliwa na meno ) mara chache mtoto kuzaliwa na meno na hayana madhara isipokuwa kama yana muumiza mama ,hutolewa hospitali.

3.IMANI POTOFU

MAMA MJAA MZITO HATAKIWI KUTIBIWA MENO

UKWELI ;ni kwamba mama mjamzito anatakiwa kupata matibabu yote ya meno kulingana na ushauri wa dactari atakavyo ona.

4.IMANI POTOFU

HUTAKIWI KULA CHOCHOTE KABLA YA KUNG’OA MENO na HAITAKIWI KUNG’OA meno mchana

UKWELI,tunashauri mtu awe amekula na kushiba wakati anakuja kung’oa meno na meno yana naweza ng’olewa muda wowote.

5.IMANI POTOFU

DAWA YA JINO NI KUNG’OA

UKWELI ,ni kwamba kuna aina nyingi za matibabu ya meno ikiwemo kuziba ama kujaza ; matibabu ya mzizi wa jino root cannal treatment na kukuta mizizi ya jino yaani APICECTOMY.

IMEANDALIWA NA

DR.MBOBOYU …….076221006 .THE DENTAL SURGEON(DDS)
Mi jino inakatika vipande vipande.
Umebak mziz,
Unauuma.

Kuna utovu wa mti unaitwa mkuyu eti ukieka kwe jino linatoka,

Ikiwekwa vbaya yanang'oka yooote.
 
Mkuu nina jino lina rangi nyeusi
Vipi inawezekana likawa jeupe mkuu maana wanasena tumerithi vp kuna ukweli wowote hapo...
 
inaletwa na Fortunata Cornel DDS 4

Kinywa ni sehemu muhimu sana katika mwili wa mtoto kwasababu ya kazi mbalimbali ambazo zinafanywa na kiungo hichi ikiwemo kula,kuzungumza,kuonyesha hisia kama kucheka au kulia na pia ni sehemu ambayo mtoto hutumia kwa kujiliwaza kwa mfano kunyonya vidole kung’ata kucha na kadhalika.

Pia watoto hupenda kuweka kila kitu wanachokutana nacho mdomoni ,ni muhimu kujua jinsi ya kutunza vinywa vyao ili kuepuka magonjwa mbalimbali yanayoweza kuadhiri afya zao.

Magonjwa ya kinywa na meno yanayowapata watoto wengi mara nyingi ni magonjwa ya fizi(periodontal diseases) pamoja na kutoboka kwa meno(dental caries).Magonjwa haya yanweza kuadhiri afya ya mtoto kwa namna nyingi sana;

  • Kutoboka kwa meno kunaweza kusababisha maumivu ambayo humafanya mtoto kushindwa kula vizuri.Hii hali humfanya mtoto kushindwa kupata viritubisho sahihi kwenye mlo wake.
  • Kutoboka kwa meno kunaweza kusababisha mtoto wako kupata maambukizi sehemu zingine za usoni na shingoni(dental abscess)ambayo husababisha uvimbe kutunga usaha,maumivu makali na homa.
  • Ajali kama kuanguka kunapelekea meno kung’oka kabla ya mda wake na hivyo inaweza kumpelekea mtoto kuchelewa kuota meno ya utu uzima na hivyo akapata shida hasa wenzie wakimcheka kuwa ana mapengo,hii pia inaweza kupelekea mpangilio mbaya wa meno ya ukubwani(malocclusion)
  • Magonjwa ya fizi huweza kusababisha mtoto kuwa na harufu mbaya mdomoni na hii humfanya akose amani na hata kujitenga na wenzake .Mtoto anapokosa kucheza na kukaa na wenzake (interaction) huathiri ukuwaji wake na huweza ata kumfanya mtoto achelewe kuongea.
  • Muonekano wa mtoto pia huharibika pale ambapo meno yake yanapotoboka sana(rampant caries).Hii inaweza kumfanya mtoto kukosa kujiamini na pia kushindwa kuongea au kucheka vizuri na hata wengine hukataa kwenda shule na hivyo kuhatarisha ukuwaji wao.
 
Back
Top Bottom