USA Vs China

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,601
8,741
Marekani na China wanapigania Tanzania kwa sasa kwani wanaamini Tanzania itakuwa super power ya East and Central Africa. Marekani pamoja na kuweka balozi wao mwanajeshi msaafu wako kwenye harakati za kufungua base ambayo itaanza kama kituo cha kirafiki cha mafunzo ya kijeshi. Kila mwaka meli za kimarekani zinakuja Tanzania kwenye mafunzo ya kirafiki lakini hii ni kujenga uhusiano mzuri baina ya Tanzania na Marekani. Marekani ni utaratibu wao kutawala kwa marafiki kwa mfano Asia marekani ana base Japan, Korea na urafiki wa karibu wa Taiwan hivyo china hawezi kumzidi kule. Vilevile huko ulaya Marekani wana German na uhusiano wa karibu na UK na nchi nyingi tu.
China wameligundua hilo na leo hii wametuma kiongozi wa kijeshi Tanzania na wanajaribu kuweka urafiki wa karibu lakini bado watu wengi hawaamini Wachina. Vilevile vifaa vya kichina vinaaribu jina la china sana Tanzania na Watanzania wengi hasa wafanya biashara wanafikiri China inataka kuwapeleka wafanyabiashara wao Tanzania kufungua masoko kwa China.
Marekani zamani ilikuwa inamtumia Japan lakini sasa wameamua kufanya vitu wenyewe.
Baadae nitaeleza kwa kwanini hasa Tanzania ni muhimu kwa hizi nchi
 
Tatizo huwezi jua nia ya hizi nchi linapo kuja swala la Tanzania. Kila nchi ina serve interest zake na kila nchi haswa hizi kubwa, kwao urafiki ni wa convenience tu. Swali ni kwamba je Tanzania ita faidikaje au kutumiwaje katika huu uhusiano na hizi nchi?
 
Mwanaf!
Wenzetu wana long range vision. Sisi hatuna. Wenzetu walishaona mbali. Sisi tunaona kutembelewa na Bush na kukaribishwa White House na Obama inatosha. Lakini naomba kuwakumbusha kauli ya Mwalimu Nyerere. Alisema mkishawakaribisha Wamarekani na kuwapa kituo cha kijeshi hawaondoki.
 
Watanzania hatuna utaratibu wa kuwa na malengo ya muda mrefu. Ukitupa malengo ya muda mrefu harafu kukatokea msukosuko kidogo happ katikati basi tutakualaumu kama nini. Viongozi nao wako madarakanai bila kuwa na vision yoyote ya nchi hivyo hawana plan yoyote ya muda mrefu. Ndiyo maana ukiwapa zawadi ya gari la kifahari au trip ya kwenda nje na kukaa 5-star hoteli kwa siku nne basi utapata mkataba wa kuikomoa nchi bila kuamini macho yako. Vile vile huko vijijini ukiwapa T-Shirt, kanga, baseball hat na pilau umemaliza. Watakuambia wewe chukua kila unachotaka hata kama majirani wakipiga kelele usiwasikilize.
 
Mwanaf!
Wenzetu wana long range vision. Sisi hatuna. Wenzetu walishaona mbali. Sisi tunaona kutembelewa na Bush na kukaribishwa White House na Obama inatosha. Lakini naomba kuwakumbusha kauli ya Mwalimu Nyerere. Alisema mkishawakaribisha Wamarekani na kuwapa kituo cha kijeshi hawaondoki.

You are right mkuu we are very simplistic. We never look past today. Matokeo yake tuna rithisha watoto na wajukuu nchi ile ile tuliyo ikuta sisi.
 
Back
Top Bottom