Acha kuukana uraia wa nchi yako. Njaa itakuua.
Afrika ilitawaliwa na wageni kwa sababu watu wake hawakuweza/taka kutoka nje.
leo tushajifunza historia na kuona hili bado kuna watu wanang'ang'ania kujifungia Afrika tu? Hata katika zama hizi za telecommuting, dual nationalities na mobile banking?
Nawashangaa sana watu ambao mpaka leo wana mawazo mgando kama haya,inaonyesha kabisa jinsi wasivyojua maana ya Diaspora,labda niulize tu,hawahawa mnaowapinga wakiamua kujenga wanajenga wapi kama sio kwao,na inakuwaje kila mara tunapowapigia simu wimbo wenu wa Taifa ni umasikini na kuomba mtumiwe hela.Acheni unafiki,hata hao walioendelea kiuchumi wameendelea baada ya kutoka na kufanya biashara na mataifa mengine,sasa ndugu zangu mnakalia utanzania mnaficha nini huko mpaka msitoke au mnafuga fisi?Watazame jirani zetu Warundi awalivyokuwa wanajidai kutojua nchi nyingine walipofikia?Twende mbele turudi nyuma ili tuendelee tunahitaji changamoto toka katika mataifa yaliyoendelea na sio kwa kuwasubiri waje nyumbani kwani wakija wao wanakuja kuvuna,ni kwa wenye nafasi kuwafuata hukohuko kwao na kuchukua kilichopo kurudisha nyumbani.Mwisho nikuulize tu,hivi leo hii ukipewa Green Card utaikataa..
Nitaikataa. Nje sawa na ndani kuwa Mzalendo.
Uko sahihi kaka,hapa inatubidi tusichoke kulilia dual nationality kwani hata kama mtu ukiwa na uraia wa nchi nyingine haimaanishi kuwa uzalendo huna.Huwa napata hasira sana hasa pale ninapotaka kwenda nyumbani ambako nimejenga na kununua mashamba na nina vitegauchumi vyangu,kisha kajinga tu ka ubalozini kananiambia tumekunyima viza,shit...
Ulishwahi kunyimwa visa ya kuingia Tanzania?kutokea nchi gani mkuu?kama una gamba tayari visa za bongo unaweza chukulia airport bongo ukishafika,kwenda ubalozi si lazima sana,unless wawe wamebadili utaraibu ama depending na hapo ulipo.
Uchumi gani huu unaotaka mtu afungwe kamba nyumbani kwake kama mbuzi wa hitima?
Uchumi wa dunia hii ya teknolojia au wa mwaka 1947?
Nani sasa ataendeleza huo uchumi kama nyinyi mmeshakimbilia nchi za watu kwenda kuwa watumwa? Mnataka wengine watengeneze halafu nyie ndiyo mrudi? Ovyooo.
Bado hujaelewa somo.
Kila mtu ana karama yake, wengine wana karama ya kuendeleza uchumi kutoka ndani ya nchi, wengine wana karama ya kuendeleza uchumi kutoka nje ya nchi. Nchi inatuhitaji wote, na kama umesoma uchumi hata wa kuanzia tu utajua it is all about the allocation and utilization of resources in the best and most efficient way. This is as basic as Adam Smith.
Sasa kama Mtanzania anaweza kuwa CEO wa Standard Chartered kwa kufanya kazi nje ya Tanzania, na hizi corporations ndizo zinakuja kuwa hegemons katika uchumi mpya, kwa nini Mtanzania huyu asikae nje akaendeleza karama yake na in the process kuisaidia Tanzania?
Hizi habari za kufikiri kwamba ili ku participate katika uchumi wa Tanzania ni lazima uwe Tanzania ni function ya kutoelewa uchumi wa dunia unavyoenda leo na trend ya future. Hata baada ya resources na tools zote za leo (unaweza kupiga simu kutoka Tanzania kuja US cheaper kuliko US kuja Tanzania siku hizi) bado unafikiri kwamba ni lazima kila mtu alundikane Tanzania.
Hata hao wajasiliamali wa Tanzania walio nyumbani watahitaji Watanzania wenzao walio nje ili wapate habari kamili za nje, wote tukirudi nyumbani nani atatoa michongo?
Tanzania inahitaji watu wengi zaidi kutoka nje, sio habari za uzalendo pofu usioelewa kwamba hata hii mipaka ya nchi ni superficial tu na kadiri biashara inavyozidi kupanda mipaka hii ya kihistoria itafutika.
comoro.....Hebu nipe mfano wa nchi iliyojengwa namna hii hapa duniani? Huo mfano wa CEO wa benki ni unique na sidhani kama ni realistic. Wengi hawaleti faida hiyo unayoongelea.
Ulishwahi kunyimwa visa ya kuingia Tanzania?kutokea nchi gani mkuu?kama una gamba tayari visa za bongo unaweza chukulia airport bongo ukishafika,kwenda ubalozi si lazima sana,unless wawe wamebadili utaraibu ama depending na hapo ulipo.
Kuna kajinga kamoja huwa kanasumbua sana hapa ninapoishi na kinachofanyika inabidi mtu upate visa toka huko kwa fax..
Hebu nipe mfano wa nchi iliyojengwa namna hii hapa duniani? Huo mfano wa CEO wa benki ni unique na sidhani kama ni realistic. Wengi hawaleti faida hiyo unayoongelea.
tehe teh teh ingekuwa enzi za julius tungemwuita msaliti uyu awa ndo sasa wankomaa na agenda za uraia wa nchi mbili
Green Card ni kupewa US permanent resident,siyo urahia,unakuwa mkazi na unapewa haki ya kufanya kazi na kupata social security number,ambayop itakuwezesha kufanya kazi bila kujificha,
Unaweza kuomba uraia baada ya kuwa na hiyo Green card kwa miaka mitano!.Green Card ni kupewa US permanent resident,siyo urahia,unakuwa mkazi na unapewa haki ya kufanya kazi na kupata social security number,ambayop itakuwezesha kufanya kazi bila kujificha,