US Sec of State, Hillary Clinton in major African trip.

Hizo Visa za Marekani na China, zote ni kutuingiza mkenge tu, tena bora Marekani walivyotunyima. Kwa sababu sisi hatufanyi biashara na Wamarekani wala Wachina, China wameturuhusu tuingine China kiholela holela kwa sababu tunaenda kuokota bidhaa-takataka kuja kuzi dampu Afrika. Afrika ni dampo la bidhaa mbovu, Kiingereza wanaita "dumping ground." hata wewe ungeanzisha biashara ya kuuza takataka zinazotupwa Tabata dampo halafu ukawapata wateja wanakuomba wazifuate wenyewe, ungekataa? Ndo maana China haimnyimi mtu visa!

Unataka Visa ya Marekani na China ya kwenda kufanya nao biashara, wewe Mmakonde wa Ntwala unapeleka nini Marekani, vinyago?
Sorry, this is a stupid contribution, accepting your own weakness as a staying fact.
Ho low!
 
Hivi ni kipi ambacho US hawajakifanya ambacho china inakifanya kiasi kwamba tuwakatae?Kwa upande wangu naona bora hata china ingawa wote ni wanyonyaji lakini china hawana mpango wa kutuchonganisha tupigane kama wanavyotufanyia US,France na UK.
 
In Africa, Clinton takes subtle swipe at China


"I will be talking about what that means, about a model of sustainable partnership that adds value
rather than extracts it," Clinton told a university audience in this West African capital. "That's America's commitment to Africa."

China surpassed the United States as Africa's largest trading partner in 2009
, with the energy sector leading the change. Africa accounts for an estimated one-third of Chinese oil imports, behind only the Middle East.

Clinton acknowledged that the United States and other Western nations, with centuries of exploitative trade and business enterprises in Africa, are hardly blameless.
"The days of having outsiders come and extract the wealth of Africa for themselves, leaving nothing or very little behind, should be over in the 21st century," she said....

The fear of extremism and terrorism undergirds Clinton's choice to visit Uganda, which is led by one of Africa's long-surviving strongmen but is also a key U.S. partner in counterterrorism and other security goals.

Clinton will also visit the new nation of South Sudan - where the Obama administration is worried about a war with Sudan or a prolonged economic decline - along with Kenya, ... and Malawi.

Hapo buluu, ndio amesema nini?

Vyandarua na vita dhidi ya ugaidi ndio added value?

Clinton atatembelea Malawi na Malawi wanatafuta mafuta katika Lake Nyasa na kuijibu ufedhuli Tanzania... Added value hio! Vita inakuja.

Sasa wacha niwachekeshe kidogo. Siku ambayo Twin towers ziliripuliwa ni siku hiyo hiyo ndio yalifanyika mazoezi ya matayarisho ya terror attack katika minara hiyo. Lakini hakukuwa na jet za kijeshi zilizoweza ku-intercept ndege zilizotekwa. Na zaidi siku hiyo Mdogo wa Bush ndio alikuwa anamaliza mkataba wa kutoa security service/ ulinzi katika majengo hayo.

Pili, siku balozi za US zilipopigwa mabomu Dar na Nairobi zilipigwa kwa wakati mmoja/ (saa) na ni balozi za US tu!

Hapa ndio kichekesho chenyewe, Hawa US wana CIA, State dept na Homeland security dept ambazo kila wakati hutoa vitisho(tahadhari) alert kuwa kutatokea ugaidi lakini katika matokeo hayo mawili wanasema hawakuwa na fununu/ habari.

Cheka halafu changanya na zako. Tembelea hapa addedvalue
 
Americans should wake up and realise that they are no longer a super rich nation... China is and they will soon take over the world
 
IDHAA YA KISWAHILI / Matukio ya Kisiasa
[h=4]Matukio ya Kisiasa[/h][h=2]
ALeqM5i4da2Dtulqo9GVtGsFS1AzGJRbZQ

[/h]

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani Hillary Clinton amewahimiza viongozi wa kiafrika kuimarisha uhusiano na nchi zinazojali misingi ya demokrasia , na kuzipa kisogo zile zinazoweka mbele tu maslahi ya kibiashara.
Ushauri huo wa Bi Clinton kwa viongozi wa Kiafrika, ulitafsiriwa kuilenga China bila kuitaja kwa jina, ambayo imekuwa ikikosolewa na nchi za Magharibi kuweka mbele maslahi yake ya kibiashara barani Afrika, huku ikipuuza masuala mengine muhimu kama vile haki za binadamu na utunzaji wa mazingira.
Aliitoa kauli hiyo mbele ya hadhara ya wanasheria na wanadiplomasia katika mji mkuu wa Senegal, Dakar, ambako alianzia ziara yake barani Afrika. Bi Clinton alisema kuna maeneo mengi barani Afrika ambako demokrasia inakabiliwa na kitisho, na ambako haki za binadamu hukanyagwa.
''Waafrika wengi bado wanaishi chini ya utawala wa madikteta ambao kwao suala lenye kipaumbele ni kung'ang'ania madarakani kuliko kuinua kiwango cha maisha ya watu wao''. Alisema Hillary Clinton.
Mwisho wa siku za unyonyaji
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton akikutana na kundi la wanawake Senegal

Waziri huyo wa mambo ya nchi za nje wa Marekani alisema nchi yake inataka uhusiano na Afrika ambao unazinufaisha pande mbili, na si ule wenye nia ya kuchukua raslimali za bara hilo.
''Siku za wageni kuja barani Afrika na kuchukua utajiri wa bara hilo, bila kuacha chochote nyuma, zimekwisha'' Aliongeza.
Bi Clinton alisema Marekani itazingatia utawala wa sheria na demokrasia, kinyume na nchi nyingine ambazo zinayafumbia macho masuala hayo katika kulinda maslahi yake.
Ushindani wa biashara
Mchambuzi Jackie Cilliers kutoka Taasisi ya Utafiti juu ya Masuala ya Amani iliyopo nchini Afrika Kusini, anasema mtazamo huu mpya wa Marekani kuhusu bara la Afrika, una malengo ya ushindani wa kibiashara.
''Hakuna shaka kwamba ushindani kati ya Marekani na China unaweka ushawishi katika siasa za nje za Marekani. Na ushindani wa kibiashara kati ya China na Marekani barani Afrika unashika kasi. Alipokuwa ziarani nchini Tanzania, Hillary Clinton alisema Afrika inakabiliwa na aina mpya ya ukoloni, ambao unalenga kunyonya raslimali za bara hilo. Alisema Cilliers na kuongeza kwamba hiyo haina tofauti na yale yaliyoyafanywa nchi za magharibi barani Afrika siku za nyuma.'
Nchi za magharibi huishutumu China kupuuza haki za binadamu barani Afrika

Kauli ya waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani inakuja baada ya rais wa China Hu Jintao kutangaza mkopo wa dola bilioni 20 kwa nchi za Afrika, na kusema kuwa China ni rafiki wa Afrika ambaye anajali uhuru wa nchi za bara hilo kujichagulia njia ya kufuata katika mchakato wa kujiendeleza.
Katika ziara hii ya siku 11, Hillary Clinton atazitembelea pia Sudan Kusini, Uganda, Kenya na Malawi. Nchi nyingine atakazozizuru ni Afrika Kusini, na Ghana.
Mwandishi: Daniel Gakuba/APE
Mhariri: Mohammed Khelef
 
kuna viongozi wa serikali mbalimbali za africa ambao wamepigwa ban kwenda uk or america kwa sababu ya kukandamiza wananchi wao. JK na wenzake wanaikandamiza sekta ya habari hapa nchini kwamba vyombo vya habari haviko huru kuandika wanachotaka. Wafanya kazi wao kunyanyaswa kwa kushindwa kupewa haki yao ya msingi kama kuandamana au kuongezewa posho..alafu akienda america anaenda kupokelewa kwa moyo wote...Viongozi wa nchi hii wapigwe ban kwenda ulaya mpaka hapo watakapo sort out hii nchi
 
Waandishi wa habari wa tanzania ndiyo chanzo cha shida zote hizi, vyombo vya habari vinanunulika sana tena kwa bei ya kutupwa leo mwandishi anakubali kupewa ukuu wa wilaya na kukubali kuweka kalamu chini, ni aibu, leo mnaitwa na rais badala ya kuuliza maswali muhimu yanayoisumbua jamii bila ufumbuzi kama;

  • ukandamiza wa demokrasia kupitia jeshi la polisi kwa kuzuia mikutano ya kisiasa eti intelijensia
  • kupigwa kwa ulimboka na serikali
  • Migomo isiyoisha
  • rushwa ktk bunge
  • kuingiliwa kwa uhuru wa mahakama
Halafu leo media mnataka kuwa mhimili wa nne wa dola hii ni ajabu na kweli, alivyorusha tundu lissu kombola la uteuzi wa majaji wasiojua kimombo, na nyie wandishi ni bora mkubali mmeshindwa kazi.Chombo cha habari huru ni Kubenea and co. Kama ilivyokuwa enzi ya gazeti la MOTOMOTO.Tanzania atatokea Kenny Salawiwo wa bongo kweli??????
 
Hizo Visa za Marekani na China, zote ni kutuingiza mkenge tu, tena bora Marekani walivyotunyima. Kwa sababu sisi hatufanyi biashara na Wamarekani wala Wachina, China wameturuhusu tuingine China kiholela holela kwa sababu tunaenda kuokota bidhaa-takataka kuja kuzi dampu Afrika. Afrika ni dampo la bidhaa mbovu, Kiingereza wanaita "dumping ground." hata wewe ungeanzisha biashara ya kuuza takataka zinazotupwa Tabata dampo halafu ukawapata wateja wanakuomba wazifuate wenyewe, ungekataa? Ndo maana China haimnyimi mtu visa!

Unataka Visa ya Marekani na China ya kwenda kufanya nao biashara, wewe Mmakonde wa Ntwala unapeleka nini Marekani, vinyago?

Mkuu umesikia wapi nguo za mtumba au viatu zinatoka china? Wazungu ndio wanaona zinatufaa sisi, Jameni wanatuletea hata chupi na soksi za mtumba. Dharau hiyo. Marekani na europa pia wamejazana vitu vya mchina kwao. Ila mchina anapeleka vitu vya quality kwao kwa sababu ndio wanamtolea order na masharti, Pembeni wanatengeneza vitu vile vile lakini vya bei ya chini (quality nayo inapungua) kwa sababu ya soko la Afrika, sisi inabidi tununue kwa kuwa tumefulia zaidi. Ukiona kitu hakifai usikinunue, mwenye kuleta akipata hasara trip nyingine hataleta.
 
wHAT AN INSOLENCE! Why should she teach the Africans? I bet she still thinks we are just niggers. If the Chinese are bad we will discover that ourselves, we do not need a ***** to come and tell us.
I want to see America go down in my lifetime because of their crimes, endless wars and arrogance. Since the 60's the whole continent has been allied to US, UK and Germany. What did we get? Even clothes, people now wear good clothes and have shoes because of China. During the European hegemonies they were not thinking of a poor man. They were producing goods only for a certain class. I lived in times when you go to rural Tanzania you will be lucky to see a person wearing shoes!

Mkuu,

I have no further comment, get 5/5.
 
Mh yote mliyosema sawa mie nikifikiria anakwenda malawi jamani usa na malawi toka lini....na ukinikumbusha habari za meli za iran na malawi kudai mipaka ziwani basi moyooo unanienda mbiiioooooooo
 
Mh yote mliyosema sawa mie nikifikiria anakwenda malawi jamani usa na malawi toka lini....na ukinikumbusha habari za meli za iran na malawi kudai mipaka ziwani basi moyooo unanienda mbiiioooooooo

Vita inanukia.
Link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...awi-ni-hatari-kwa-tanzania-2.html#post4007564

Link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...te-journal-article-published-in-1973-a-3.html

link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-malawi-kutangaza-vita-na-tz-leo-au-laa.html
 
In Africa, Clinton takes subtle swipe at China

Clinton acknowledged that the United States and other Western nations, with centuries of exploitative trade and business enterprises in Africa, are hardly blameless.

“The days of having outsiders come and extract the wealth of Africa for themselves, leaving nothing or very little behind, should be over in the 21st century,” she said....

Clinton will also visit ....Malawi.

Link DVD Watch: Apocalypse*Africa « one white guy
 
Americans should wake up and realise that they are no longer a super rich nation... China is and they will soon take over the world

Well said Mkuu. President Kabila once said ''Kila mtu anakuja hapa anachimba Almasi, dhahabu na kila kitu then anaondoka. Toka enzi za wabeleji,sasa Kuna ubaya gani leo hawa Wachina wakitujengea mabarabara,mashule,mavyuo,badala ya kulipa faranga tukalipa madini ambayo huko nyuma wabeleji na wengine walibeba tu Bila kuacha faranga au chochote?''. According to me he has a point here.
 
Back
Top Bottom