Uropokaji wa Makamba utaisha lini?

Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
59,189
79,420
Kumfananisha Marehemu na dhahabu iliyopandwa? Sipati maana? navyojua mimi dhahabu hununuliwa, hutumika kwa urembo baada ya kuchimbwa kufinyangwafinyangwa kutengenezwa katika maumbo anayopenda muhusika, thamani yake hushuka na kupanda! sasa kama Dr Gama alikuwa dhahabu ni kumshushia heshima ina maana CCM ilimfinyangafinyanga ikamtumia ilivyotaka baada ya kumchimba na huyu bwana akaongezea wali-mpanda walivyotaka! Kha! Binafsi nathani alikuwa mtu safi na mchapa kazi! Hivi huyu Makamba ana wasaidizi? Huwa anaandika speeches au huwa ana-flow tu? Maana tunajionea mengi kila siku na yanakuja mengineyo! Fikra zake zimejaa fweza fweza tu zaidi ya utu!

20th December 09
JK kuhudhuria mazishi ya Gama

Gideon Mwakanosya

Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwasili mjini hapa leo mchana kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), marehemu Dk. Lawrence Gama.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dk. Christine Ishengoma, alisema jana kuwa Rais Kikwete anatarajiwa kuwasili leo saa 6:00 mchana ambapo ataelekea katika kijiji cha Amani Makolo atakakozikwa marehemu Gama.
Hata hivyo, jana mamia ya wananchi walijitokeza kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Gama mara baada ya mwili wake kuwasili mjini hapa. Mwili wa Gama ulipelekwa katika makumbusho ya mashujaa wa vita vya Majimaji na kuagwa kwa heshima zote za kimila.
Baadaye mwili huo ulipelekwa katika uwanja wa Majimaji ambapo viongozi mbalimbali wa chama na Serikali waliweza kutoa heshima zao.
Akizungumzia utendaji wa Dk. Gama, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba alisema marehemu alikuwa dhahabu iliyopandwa katika maeneo mbalimbali Tanzania na kwamba mchango wake hautasahaulika.
Mwili wa marehemu Gama ulisindikizwa na Makamba ambaye aliongozana na Naibu Waziri wa Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Emanuel Nchimbi.
Marehemu Gama anatarajiwa kuzikwa leo mchana.

NIPASHE JUMAPILI
http://www.ippmedia.com/frontend/functions/print_article.php?l=11479
 
Kumfananisha Marehemu na dhahabu iliyopandwa? Sipati maana? navyojua mimi dhahabu hununuliwa, hutumika kwa urembo, thamani yake hushuka na kupanda! sasa kama Dr Gama alikuwa dhahabu ni kumshushia heshima! Binafsi nathani alikuwa mtu safi na mchapa kazi! Hivi huyu Makamba ana wasaidizi? Huwa anaandika speeches au huwa ana-flow tu? Maana tunajionea mengi kila siku na yanakuja mengineyo!

20th December 09
JK kuhudhuria mazishi ya Gama

Gideon Mwakanosya

Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwasili mjini hapa leo mchana kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), marehemu Dk. Lawrence Gama.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dk. Christine Ishengoma, alisema jana kuwa Rais Kikwete anatarajiwa kuwasili leo saa 6:00 mchana ambapo ataelekea katika kijiji cha Amani Makolo atakakozikwa marehemu Gama.
Hata hivyo, jana mamia ya wananchi walijitokeza kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Gama mara baada ya mwili wake kuwasili mjini hapa. Mwili wa Gama ulipelekwa katika makumbusho ya mashujaa wa vita vya Majimaji na kuagwa kwa heshima zote za kimila.
Baadaye mwili huo ulipelekwa katika uwanja wa Majimaji ambapo viongozi mbalimbali wa chama na Serikali waliweza kutoa heshima zao.
Akizungumzia utendaji wa Dk. Gama, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba alisema marehemu alikuwa dhahabu iliyopandwa katika maeneo mbalimbali Tanzania na kwamba mchango wake hautasahaulika.
Mwili wa marehemu Gama ulisindikizwa na Makamba ambaye aliongozana na Naibu Waziri wa Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Emanuel Nchimbi.
Marehemu Gama anatarajiwa kuzikwa leo mchana.

NIPASHE JUMAPILI
http://www.ippmedia.com/frontend/functions/print_article.php?l=11479

- Tanzania bwana, huu unafiki wa siasa utaisha lini? I mean yaani mwili ulisindikizwa na Makamba akishirikiana na Nchimbi? Incredible!

Respect.

FMEs!
 
Ni kutokujua thamani ya utu wa mtu, kwani kwa hakika huwezi kumlinganisha mtu na kitu chochote. Utu wa mwanadamu uko juu ya thamani ya dhahabu, almasi na chochote kile mtu uwezacho kufikiria. Kumbe mheshimiwa yule alikosea kumlinganisha marehemu na dhahabu. Ni ajabu sana sijui alikuwa anawaza nini!
 
Sijawahi kuona thamani ya mtu inafananishwa na kitu hata kama ni cha thamani namna gani. Im sorry... but inategemeana ni nani ameongea... angeongea Kikwete wote tungeduwaa, lakini kama ni Makamba tushamzoea....
 
kuna watu na viatu, kwa hio kila mtu na tafsiri yake....binafsi sioni ubaya mzee Makamba alivyosema.Naona hapa hamumtendei haki mzee Makamba kwani nyie hio ni tafsiri yenu...sometimes jamani lazima tuwe fair sio kila kitu kucriticise just because kimesemwa na mwana CCM....
 
- Tanzania bwana, huu unafiki wa siasa utaisha lini? I mean yaani mwili ulisindikizwa na Makamba akishirikiana na Nchimbi? Incredible!

Respect.

FMEs!
Wakati u hai hai ni ngumu hata kukujulia hali.Ukifa bwana watu walewale waliokuwa wanakusulubu ndo wanakuwa karibu na jeneza lako wakiimba sifa zote kubwa humu duniani.Unafiki siasa za Tanzania sijui nani aliziasisi. Ni azimio la arusha tu limeweza kufa lakini sio unafiki ndani ya siasa
 
uropokaji ni staili yake ya maisha/kuzeeka.

ALIVYO NDIVYO ALIVYO!REST IN PEACE MZEE MAKAMBA
 
Back
Top Bottom