Urithi wetu kugeuka kuwa umaskini wetu

Gwallo

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
3,200
3,761
Katika moja ya makosa makubwa yaliyofanywa na serikali inayoongozwa na ccm ni pamoja na kuuza nchi yetu kwa matapeli wanotumia kivuli kiitwacho ‘WAWEKEZAJI’ nitazungumzia maeneo mawili muhimu tu ya mengi yaliyopewa kwa wawekezaji.

1. Loliondo- Eneo hili amepewa mwekezaji mwarabu ambaye anaendesha shughuli za uwindaji. Lolindo ni eneo linalopakana na Serengeti National park kwa upande wa kaskazini mashariki (maarufu kwa jina la Lobo area). Wanyama wetu wanawindwa hata kama hawajaingia katika kitalu cha uwindaji.

Eneo hili lijulikanayo kwa jina la LOBO lilikuwa na Pride wengi sana ya Simba miaka ya 1960-1995, leo hii unaweza kwenda lobo usiweze kumwona simba, simba amekuwa ni mnyama adimu kumwona. Mahali walikopelekwa hawa Simba wetu Serikali yetu inajua na mwarabu pia anajua.

2. Grumeti Game reserve:- Ukitaka chozi likutoke na ujue nini maana ya uwekezaji haramu tembelea eneo hili. Katika eneo la Serengeti wanyama wana tabia ya kuhamahama(Migration). Sasa Grumeti Game reserve area iko Kaskazini magharibi mwa Serengeti National park na iko within the Migration route, sasa cha ajabu mwekezaji huyu amechimba mabwawa ya maji ambayo wanyama hawa wakifika katika maeneo hayo wanakaa muda mrefu bila kuendelea na safari yao.Hurusiwi kabisa kuingia katika eneo hili na mwekezaji amewaajiri Ma-guides kutoka South Africa. Kama mnakumbuka kamati ya BUNGE iliyokuwa ina ongozwa na Cheyo iliwahi kuzuiliwa kuingia VIP Camp ya huyo mwekezaji.

ANGALIZO kwa Watz. Taifa letu linaisha, urithi wetu umekuwa ndiyo umaskini wetu na wachache kufaidika, tutaendelea hivi mpaka lini????????? Je ni hatua zipi zichukuliwe????? Mwaka jana mwezi June serikali yetu bila ilileta Bungeni mswada wa kuruhusu uchimbaji wa madini Serengeti ndipo nilipoona Dr.Mwakyembe aliposema kujadili jambo hili ni uwendawazimu. Kwa taarifa yako huyu mwekezaji wa VIP CAMP ndiyo aliyekuwa anaipeleka serikali mbio mbio akitaka aanze kuwekeza huko kwenye madini yaliyoko Serengeti.

Tuulizane maswali ya msingi kuwa tutawaambia nini kizazi kijacho??????


Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom