Urinary Tract Infection (UTI): Chanzo, Dalili na Kinga/Tiba yake

Sina access na jukwaa la JF Doctor lakini kwakuwa ni jukwaa la hoja mchanganyiko naomba wenye utaalam na uzoefu watatue na watuelimishe katika hili.
Ugonjwa wa UTI hupunguza kweli nguvu za kiume?
 
Natumaini Dr Riwa atakusaidia tafadhali mPM.

Sina access na jukwaa la JF Doctor lakini kwakuwa ni jukwaa la hoja mchanganyiko naomba wenye utaalam na uzoefu watatue na watuelimishe katika hili.
Ugonjwa wa UTI hupunguza kweli nguvu za kiume?
 
Wana JF naombeni msaada juu ya hili.

Mke wangu anasumbuliwa na kuumwa tumbo na mgongo mara kwa mara.

Mara ya kwanza tulienda hospitali wakasema ana U.T.I, akapewa dawa baada ya kumaliza ile dose alikaa kama miezi miwili bila hayo matatizo then akaanza tena kulalamika.

Tukaenda hospital nyingine akapewa dawa na kushauriwa aache kutumia vidonge vya uzazi wa mpango(akasitisha matumizi yake), tangu mwezi 9, mwaka jana mpaka juzi 14/01/2012 ameanza tena kulalamika tumbo na mgongo.

Kabla na nikiwa nafikiria nini cha kufanya naombeni mawazo yenu kwa uzoefu, ufahamu na ushauri wa kitaalamu juu ya hili.
 
Hutapata ushauri mzuri humu zaidi ya kwenda tena kwa Dr. amchukue vipimo na kuona nini hasa tatizo. Pole sana mkuu,endelea kumpenda na kumjali mkeo namna hiyo.
 
nendeni tena kwa daktari tena NAWE UPIME,U.T.I inaambukizana kupitia huko chini.pia haiponi kirahisi.na wewe usipoangalia utakuwa huwezi ku do.yaani uta do mara moja hadi kesho.pima mkojo
 
Wanajf naombeni msaada juu ya hili. Mke wangu anasumbuliwa na kuumwa tumbo na mgongo mara kwa mara. Mara ya kwanza tulienda hospitali wakasema ana U.T.I,akapewa dawa baada ya kumaliza ile dose alikaa kama miezi miwili bila hayo matatizo then akaanza tena kulalamika. Tukaenda hospital nyingine akapewa dawa na kushauriwa aache kutumia vidonge vya uzazi wa mpango(akasitisha matumizi yake),tangu mwezi 9, mwaka jana mpaka juzi 14/01/2012 ameanza tena kulalamika tumbo na mgongo. Kabla na nikiwa nafikiria nini cha kufanya naombeni mawazo yenu kwa uzoefu, ufahamu na ushauri wa kitaalamu juu ya hili.

Pooole bwn kaka. Ucjali yana mwisho hayo. Cna utaalamu wowote ila langu ni hili nenda kwa Dr. tena kwa vipimo zaidi. Usichelewe maradhi yakaongezeka. Tafadhali fanya fasta. Mungu wetu yu nawe.
 
Halafu mnaweza kujaribu kipimo cha culture,inawezekana hiyo uti haikupona kabisa,ila nendeni kwa dactari wa wanawake anaweza kuwa na msaada zaidi.
 
Jamani huu ugonjwa wa UTI unasababishwa na nini kwa mwanaume?
Dalili zake ni zipi?
Je, kama mwanaume anaumwa UTI akifanya mapenzi na mke wake atamwambukiza?
Tiba ya U. T. I
 
U.T.I ni ugonjwa unaoathiri mfumo wa mkojo wa binadamu{urinary system}ugonjwa huu unasababishwa mara nyingi na aina moja ya bacteria anayeitwa ESCHELICHIA COLI,ugonjwa huu unaweza ukawapata wanawake na wanaume .Kutokana na swali lako ugonjwa wa U.T.I kwa mwanaume unasababishwa na njia nyingi kama vile ushoga[homosexual},kunywa maji yasiyo salama,kushea nguo za ndani{chupi},kushea choo kichafu na watu mbalimbali,kuanika nguo za ndani nje .n.k.

Na dalili za huu ugonjwa ni homa kali[fever},kukojoa mkojo mzito na wenye harufu kali[clouds urine},pia unaweza ukapata maumivu chini ya kitovu[abdominal pain} na maumivu wakati wa kukojoa.Ila si lazima ukiumwa huu ugonjwa uwe na dalili zote hizi nilizozitaja unaweza ukapata dalili mojawapo kati ya hizi.

Mwanaume anayeumwa U.T.I akifanya mapenzi na mwanamke anaweza akamwambukiza au kutomwambukiza inategemea na jinsi walivyofanya hayo mapenzi.matibabu ya U.T.I ni unapewa antibiotics kama vile ceftriaxone,rimfapicin gentamycin n.k.
 
Young_Master,
Hapo kwenye bluu, panaenda kinyume na shule yangu ya Microbiology. Unaweza ukanifafanulia? inawezekana shule yangu ipo outdated....
 
U.T.I Ni ugonjwa unaoathiri sehemu ya kibofu cha mkojo( bladder infection) na figo ugonjwa unaoitwa pyelonephritis. Pyelonephritis mara nyingi wengi wetu hapa tz inawapata sana inasababishwa na gram negative bacteria kama E.coli . Dalili ni homa, maumivu, kutapika na kusika baridi (chill) tiba, kambla ya dawa cha muhimu kuhakisha mgonjwa anakunywa maji ya kutosha kama 2litre na juice ya kutosha.

DAWA ADULT Amoxycillin 500mg kila baada ya masaa 8 kwa siku 7-10 , co-trimoxazole 960 mg kila baada ya masaa 12 kwa siku 7-10, Trimethoprim 300mg moja kila siku kwa siku 7-10, potassium citrate 1-2g unayoweka kwenye maji mara tatu kwa siku, kama hali ya mgonjwa ni hatari mpe ampicillin (iv) 500mg kila baada ya masaa 6 ndani ya siku 5 hadi 10 ukiunganisha na Gentamicin (Iv) 4mg kwa masaa 24 kwa siku 5 hadi 10 . NAFIKIRI MKUU UMENIPATA
 
Young_Master,
Hapo kwenye bluu, panaenda kinyume na shule yangu ya Microbiology. Unaweza ukanifafanulia? inawezekana shule yangu ipo outdated....

Mkuu nashukuru kuliona Hilo na mie nimepata utata nikadhani my old school microbiology..... Hapo hapana!
 
ila mara nyingi hutokana na vyoo na nguo zenye unyevu kwa nijuaavyo na ukishirikiana na mwenzako kwa asilimia90 unamuambukiza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom