Elections 2010 URGENT: Mawakala wa Uchaguzi

Bado Niponipo

JF-Expert Member
Aug 15, 2008
680
168
Zikiwa zimebakia siku sita kabla ya Watanzania kwenda kupiga kura za kuchagua Madiwani, Wabunge na Rais kwa 2010 -2015. VITUO vya kupigia kura ni 51,800 nchi nzima, hii inamaanisha kila chama kinatakiwa kiwe na mawakala 51,800 nchi nzima, gharama ya posho kwa kila wakala si chini ya sh. 10,000, na mwaka huu gharama ya posho kwa mawakala haitalipwa na Tume ya Uchaguzi, italipwa na vyama husika.

Kwa hesabu za haraka haraka mawakala 51,800 kila mmoja akilipwa sh. 10,000

51,800 X 10,000 = 518,000,000
(hii ni kwa wakala mmoja mmoja kama wakiwa wawili 1,032,000,000, bilioni moja)

Je vyama vya upinzani vimejipanga vipi Juu ya hili.

Bado
 
mkuu kwenye ccm primaries mawakala walilipwa 20,000... kama unataka wakala wako asikuangushe mpe 50-100K, la sivyo atanunuliwa
 
Mkuu, nataka kutoa msaada basi usisite kama Mzee Sabodo alivyodhihirisha.. ila unasahau kuwa mwaka huu zaidi ya mawakala wa chama, tupo sisi mawakala wa kujitolea tutakaokuwa makini kulinda kura... hii isikuumize kichwa...
 
mkuu kwenye ccm primaries mawakala walilipwa 20,000... kama unataka wakala wako asikuangushe mpe 50-100K, la sivyo atanunuliwa

Mkuu hii sasa itakuwa hatari sana. Vituo viko 51,800 kwa gharama ya 50,000 kwa wakala:-

51,800 X 50,000 = 2,590,000,000 bilion mbili na nusu, na wakiwa mawakala wawili kila kituo ni 5 bilion.

Hizi gharama vyama vya upinzani wanazo?.
 
Mkuu, nataka kutoa msaada basi usisite kama Mzee Sabodo alivyodhihirisha.. ila unasahau kuwa mwaka huu zaidi ya mawakala wa chama, tupo sisi mawakala wa kujitolea tutakaokuwa makini kulinda kura... hii isikuumize kichwa...

Mtakuwa ndani au mita 200 mkuu?.
 
Makubaliano kati ya NEC na vyama vya siasa yalikuwa NEC itawalipa lakini leo NEC imeruka jukumu hilo chini ya makubaliano hayo.......Inashangaza NEC inawalipa wasimamizi na makarani wa muda iliyowaajiri lakini haipo tayari kuwalipa mawakala kama siyo njama za CCM mimi sijui hili linatoka wapi......
 
Sasa vyama vya upinzani vimejipanga vipi juu ya hili, hapa tukumbuke siyo wagombea urais tuu hata wabunge na madiwani.
 
Am ready kuwa wakala wa CHADEMA Iringa Mjini, sitaki hiyo 10,000. Inasikitisha sana,am 100% Chadema wataangushwa na mawakala. Take it JF members,we are gone
 
Mtakuwa ndani au mita 200 mkuu?.
Tutakuwepo kote wala usiwe na wasiwasi ndnai na nje, wengine ni wasimamizi wa kura, wengine ni askai polisi, wengine ni wapiga kura ambao watabaki mita 100 kutoka kituo na tutakizingira kwa pande zote. Ondoa hofu kwani mwaka huu mabadiliko si jukumu la Chadema tu bali ni ya watanzania wote!
Kila mtu acheze nafasi yake... ikibidi mchangie wakala wa kituo chako iwe ndo mchango wako kwa mabadiliko wa kweli.
Sijui umenielewa mkuu? HIi ndo maana ya people's power!
 
Hapo kwenye DEEP GREEN, NEC wamepiga marufuku hii kitu, unapiga kura na baada ya hapo uaondoka kituoni kabisa.
 
Hapo kwenye DEEP GREEN, NEC wamepiga marufuku hii kitu, unapiga kura na baada ya hapo uaondoka kituoni kabisa.

Hapana, mkuu unapotosha umma. Tamko imetoka NEC - ruksa kusimama ndani ya mita 100 ya kituo. Wanaotaka kuleta longolongo ni wasimamizi wa uchaguzi katika wilaya lakini NEC imetoa ruksa.
 
Hapana, mkuu unapotosha umma. Tamko imetoka NEC - ruksa kusimama ndani ya mita 100 ya kituo. Wanaotaka kuleta longolongo ni wasimamizi wa uchaguzi katika wilaya lakini NEC imetoa ruksa.

Mkuu hii DEEP GREEN kama ikiwa kweli basi safi sana lakini, lakini Zanzibar wametangaziwa kuwa baada ya kupiga kura watu waongoke, hakuna mita 100 wala mita 200.
 
Hii ndiyo maana tunatakiwa kutambua na kuchukua picha halisi ya aina gani ya TUME YA UCHAGUZI tuliyo nayo Tanzania. Hawa ni waharibifu tu wa demokrasia kwa masilahi ya walio madarakani. Njama ni nyingi toka CCM na tume yake. Toka awali hawakuarifu umma na vyama kuhusu gharama za kujilipia mawakala wao! JE, Jumuiya ya ulaya na wafadhili walitoa fedha za uchaguzi, hela hii ipo wapi? Wanaujua ufidhuli huu unaofanywa na Tume inayoelekezwa na CCM kwa vile wao wanachangiwa na mafisadi? Haya ni makusudi na hila wakijua vyama havitakuwa na fedha kulinda kura na hivyo CCM waibe wawezavyo au wawahonge wawakala kirahisi. Hi ni dhambi kubwa na mwenyekiti na mkurugenzi wa tume wanafaa kushtakiwa mahakamani na kwa wafadhili pia ili wajue yote haya.
Hawa ndio maadui wa uhai na ustawi wa taifa na demokrasia.
Vyote hivi vya kuilinda CCM na pia huu uozo wa TUME hii umewadia.MUNGU anasimama na watanzania. Wote tuungane, KURA NYINGI YA NDIYO KWA DR SLAA ndio pigo sahihi. TUME Watakimbiana Slaa ataposhinda kwa nguvu kubwa.
 
mkuu hii sasa itakuwa hatari sana. Vituo viko 51,800 kwa gharama ya 50,000 kwa wakala:-

51,800 x 50,000 = 2,590,000,000 bilion mbili na nusu, na wakiwa mawakala wawili kila kituo ni 5 bilion.

Hizi gharama vyama vya upinzani wanazo?.
kila mtu anajua kwamba lazma uzalendo uzidi kipato kuwa fair
 
Tutakuwepo kote wala usiwe na wasiwasi ndnai na nje, wengine ni wasimamizi wa kura, wengine ni askai polisi, wengine ni wapiga kura ambao watabaki mita 100 kutoka kituo na tutakizingira kwa pande zote. Ondoa hofu kwani mwaka huu mabadiliko si jukumu la Chadema tu bali ni ya watanzania wote!
Kila mtu acheze nafasi yake... ikibidi mchangie wakala wa kituo chako iwe ndo mchango wako kwa mabadiliko wa kweli.
Sijui umenielewa mkuu? HIi ndo maana ya people's power!

Mkuu umeongea jambo muhimu sana, kama kweli NEC imesema hivi, CHADEMA watangaze tu kuwa wanaomba wapenzi wao wachangie hela ya kulipa wasimamizi.... naamini kabisa kwa mia , mia tano , alfu moja na kuendelea hii itakuwa sio tatizo.
unapiga kura na unachangia ulinzi wa kura... hakishindikani kitu ni organization tu inatakiwa.....
 
Acheni ujinga majimbo mengi watu wako tayri kufanya kazi bila kulipwa TZS 10,000 nini nini bwana!
 
Upinzani wa kweli unahitaji sana kujitoa. Vyama pinzani hususani CHADEMA wanahitaji kushirikiana na wanachama wa kweli ktk kufanikisha zoezi la uangalizi wa kura. ALL THE BEST:thumb:
 
Back
Top Bottom