Urembo: Jinsi ya kuzuia na kuondoa wrinkles

queenkami

JF-Expert Member
Feb 8, 2010
1,599
1,025
Hello ladies,so leo nimeona niwape tips jinsi ya kufanyakuwa na ngozi nzuri inayovutia.Najua wengi wetu labda tunajua ninachotaka kukisema ila pia si ajabu kuwa kuna ambao bado hawajui hivyo wanaweza kuwa wamenufaika na hii topic.Nitaanza mara moja ili nisiwachoshe kwa maneno mengi.

MAHITAJI
Yai,asali,sukari laini ya unga,limao,manjano,nyanya iliyoiva vizuri lakini ngumu,bakuli mbili,liwa,sabuni,taulo laini na safi na moisturizer.

JINSI YA KUFANYA
Safisha vizuri uso kisha kausha kwa taulo,usiache maji yakaukie yenyewe usoni,sio vizuri.Chukua nyanya uliyoisafisha vizuri kisha ikate katikati kisha inyunyuzie sukari,halafu sugua nayo usoni taratibu sana bila kujichubua ,sugua kama unachora maduara kuanzia kidevuni kwenda kwenye paji la uso,usianzie juu kwenda chini siku zote anzia chini kwenda juu.Kitendo hiki /exfoliation husaidia kuondoa ngozi zilizokufa,kufungua vitobo katika ngozi,hivyo ngozi kupumua vizuri maana ngozi isipoingiza hewa mtu anaweza kupata chunusi.Ukishafanya hivyo kwa kama dk 2 then acha ibakie hivi hivi usoni then;

Chukua yai lipasue katikati ukihakikisha kuwa kiini hakivurugiki,kishatenganisha ute mweupe kwenye bakuli lake na kiini kwenye bakuli lake,Kisha chukua bakuli lenye kiini weka manjano,asali,matone ya limao na liwa kisha koroga upate mchanganyiko unaoona utanata usoni bila kuchuruzika.Kila kitu pima kulingana na jinsi wewe unavyoona itatosha kukupatia mchanganyiko usio mwingi wala kidogo sana na wala usio mgumu wala mwembamba sana.Then;

Safisha uso kuondoa zile nyanya na sukari,jikaushe then jipake huu mchanganyiko ukae nao kwa dk 10-15 au zaidi kama muda unaruhusu.

Baada ya hapo,safisha vizuri uso wako huku ukisugua sugua kama kuna ngozi zilizokufa zilizobakia zitoke zote kisha jikaushe halafu;

Chukua lile bakuli lenye ute mweupe wa yai,(hakikisha kiini hakijaingia humu hata kidogo),chukua uma kisha pigapiga huo ute hadi uwe kama povu halafu jipake usoni kwa wingi mara moja kisha toka nje upigwe na upepo ambao utasaidia kukausha kwa haraka huo ute.Kadiri ute utakavyokua ukikauka usoni mwako utaona kuwa ngozi ya uso wako inajivuta na kuwa tight.Kaa na huu ute kwa dk 10-15 kama unaweza kukaa nao zaidi ni vizuri.Hii inasaidia kukaza misuli ya uso hivyo kuzuia wrinkles au kama zipo inasaidia kuziondoa maana wrinkles huja pindi misuli ya uso inapokua imelegea.

Baada yah apo safisha uso paka moisturizer/lotion yako.

Ukifanyahivi kila wiki mara moja baada ya mwezi utaona jinsi ngozi yako inavyobadilika,ila hata siku ya kwanza utaona ngozi yako haiko kama ilivyokua kabla ya kufanyahivi.

NOTE:Vipo vitu vingi sana vya asili vinavyotumika na sio mbaya kuongeza vitu vingine kama kitunguu saumu,matango,wengine maziwa,unga wa dengu na vingine vingi ila kuna watu wanachanganya pia na mafuta ya mawese,kabla ya kuchanganya mawese kwenye mchanganyiko wako ni lazima uwe na uhakika wa asili mia moja kuwa ngozi yako haitareact vibaya baada ya kujipaka haya mafuta.Kuna ngozi hazitaki mafuta,hivyo mtu unaweza kujipaka mawese ukashangaa umepata chunusi za kufa mtu.

Okay,hope kuna aliyefaidika.
 
hahahaha! Mkorogo ni noma queen. Huu mchanganyiko wako nimeshausoma muda tena nimeusave kabisa. Lol

wee Husninyo acha kujishaua hapa baada ya mm kuweka jinsi mkorogo ulivyokukubali LOL au sio wewe uliyekusema bora desh desh(sipendi kuitaja jina nitaipromote) wiki moja matokeo tu,sasa unoma wake ni nini tena.
Kumbe mchanganyiko wangu uliosoma lakini kunipa moyo kuwa umenufaika nao ili siku nyingine nikiwa na kitu kizuri ni-share tena na nyie ukaona no way bora nisifie mkorogo LOL (hope unaelewa kuwa natania tu mpenzi wangu)
 
Last edited by a moderator:
Urembo ndo kila kitu haswa kwa sisi wanawake so Asili zaidi na unakuwa mrembo zaidi.

umeonaee Okya vitu vya asili ni vizuri sana,na mtu akiwa na ngozi nzuri inayotunzwa awe mweupe au mweusi ataonekana mrembo tu.Sema wengine wanadhani kuwa mweupe ndo kuwa mzuri wakati unakuta mtu ni mweupe ndio lakina ngozi ngavuu plus mabaka baka kama kenge na masugu sasa hapa utakuaje mrembo.!
 
Last edited by a moderator:
Asante queen, nitajaribu this weekend.

Jaribu dora utajionea mwenyewe jinsi itakavyokua,inalipa halafu ni cheao plus mim naona mfano kwenda salon kufanyiwa scrub na facial treatment hata uwezekano wa kuambukizwa magonjwa upo na salon siku zote wanatumia products za viwandani,hapo uombee wasitumie ambazo zimesha expire.
 
Last edited by a moderator:
Jaribu dora utajionea mwenyewe jinsi itakavyokua,inalipa halafu ni cheao plus mim naona mfano kwenda salon kufanyiwa scrub na facial treatment hata uwezekano wa kuambukizwa magonjwa upo na salon siku zote wanatumia products za viwandani,hapo uombee wasitumie ambazo zimesha expire.

Ni kweli nilishafanya facial salon nikatoka vipele vingi usoni. I hope itanisaidia kuondoa mikunjo (laugh lines/wrinkles) iloanza kujitokeza usoni mwangu. Will give u feedback!.
 
Ni kweli nilishafanya facial salon nikatoka vipele vingi usoni. I hope itanisaidia kuondoa mikunjo (laugh lines/wrinkles) iloanza kujitokeza usoni mwangu. Will give u feedback!.

itakusadia sana tu,kuhusu hapo pekundu,jaribu uwe unakaa na ule ute mweupe kwa muda mrefu zaidi kila upatapo muda,nitafurahi kupata feedback yako.
 
Yes, kama unataka urembo basi vitu vya hasili ukitumia unakuwa mrembo like me na wengine wengi huna haja ya kutumia mahela kwa kununua mavipodozi ya gharama alafu baadae hukiishiwa ngozi inaharibika na kuwa namabaka mabaka. Acheni jamanii Asili inatosha kukufanya mrembo zaidi .
 
Back
Top Bottom