Urais Zanzibar: Je, ni Lini zamu ya watanganyika kutwaa urais?

Kivp mkuu? Unaweza kutoa mifano michache ili kuweka uzito kwenye hoja yako? Natumai hii habari hapa itawafikia wakuu wa nchi ili nao watafakari. Kwa hivyo ukitoa mchango tafadhali hakikisha kuna evidence.
kwenye muungano, wazanzibari wanatunyonya tu, na ni wakoloni wetu
 
Bila kuiondoa madarakani CCM hili suala la Munngano litaendelea kutusumbua hadi Yesu atakaporudi Duniani!
 
Seif kanena sawa kutokana na loopholes zilizopo kwenye muundo wa muungano wa sasa! Viongozi wetu na wao wameridhika kuona identity yao inamwezwa na hili neno la Mtanzania. Huku wazanzibar wakiendelea kujipambanua kwamba wao si watanzania bali ni wazanzibar!

Najiuliza sijui vitambulisho vya Taifa vitaandikwaje kwenye Nationality, Mtanzania pekee, mzanzibar pekee au wote tutachukuliwa ni watanzania?
Payuka umeleta mada muafaka na wakati muafaka. Ni juzi tu maalim seif ametamka kuwa safari hii ni zamu ya mzanzibar kuwa rais wa muungano pamoja kwamba utaratibu huo haujaandikwa popote.hjlo halijaandikwa popote. Hivi sasa seif yuko mwanza anarandaranda na vingora barabarani.
 
Nimesikia mara nyingi kauli hii "kuna mambo yasiyo ya Muungano na yaliyo ya Muungano",. Kwa uelewa wangu Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tz wanashughulikia yale mambo ya Muungano, wakati ambao Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inashughulikia mambo ya yasiyo ya Muungano kwa upande wao. SWALI: Mambo yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanganyika chombo gani kinayashughulikia? Kumbuka si sahihi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tz kushughulikia mambo yasiyo ya muungano ya upande mmoja tu.
 
Angalau akina JK waone kwamba Wadanganyika wameanza kutambua kwamba wanatawaliwa na wazanzibar. Leo hii tuna mifano ya wabunge wazanzibar waliopita kupitia majimbo ya bara, mfano Kinondoni. Lakini haiwezekani kutokana na siasa za zanzibar mtu wa bara akapiga hata hiyo kura tu bila mizengwe. Rais akitoka Zanzibar atashughulikia mambo yote ya muungano na yasiyo ya muungano (ya Tanganyika), lakini akitoka Tanganyika, yale ya zanzibar hayamhusu. Kwa mfumo huu wa muungano raia wa upande mmoja wa muungano anakuwa na haki zaidi kuliko raia wa upande mwingine wa muungano. Wanzanzibar wanajiona wana haki na utaifa zaidi kuliko watanganyika. Na kama watanganyika tutaendelea kulala na kuwasikiliza CCM na uroho wao wa kutawala, tumekwisha. Wake up all and fight for our mother land.
 
Kivp mkuu? Unaweza kutoa mifano michache ili kuweka uzito kwenye hoja yako? Natumai hii habari hapa itawafikia wakuu wa nchi ili nao watafakari. Kwa hivyo ukitoa mchango tafadhali hakikisha kuna evidence.
Namsaidia mpendwa kujibu hili, unyonyaji unajitanabaisha kwa jinsi nyingi. Mnapokuwa ni raia wa nchi moja wenye fursa tofauti ni unyonyaji, mfano haki ya kupata elimu (Mtanzania wa Zanzibar ana haki ya kupata elimu Tanzania, Mtanzania wa Tanganyika ana haki y akupata elimu Tanzania bara), ajira (Mzanzibar ana haki ya kuajiriwa Tanzania, Mtanganyika ana haki ya kuajiriwa Tanzania bara), Uwekezaji (Mzanzibar ana haki ya kuwekeza katika chochote popote Tanzania, Mtanganyika ana haki ya kuwekeza chochote popot Tanzania bara), haki ya kuishi (Mzanzibar ana haki ya kuweka makazi yake na kutambuliwa kuwa ni mkazi popote na wakati wowote katika Tanzania, Mtanganyika atabaki huru Tanganyika na kama atataka ukazi zanzibar shurti aishi huko bila kutoka kwa miaka isiyopungua mitano ndipo apewe kitambulisho cha ukaazi). Kutokana na tofauti hizo ni rahisi sana kuwakuta wapemba wanamiliki mashamba makubwa huko Simanjiro na aghalabu sana kumkuta mtanganyika akimiliki hata kipande cha ekari tano huko pemba. Huu haufanani na unyonyaji kama ule wa waingereza wa zama zile?
 
kama wewe ni mwanamme kamuulize baba yako lini itakuwa zamu yako kulala kitanda kimoja na mama yako.Kama wewe ni mwanamke kamuulize mama yako line itakuwa zamu yako kulala kitanda kimoja ya baba yako

You deserved to be greater thinker..!!
 
Nimesikia mara nyingi kauli hii "kuna mambo yasiyo ya Muungano na yaliyo ya Muungano",. Kwa uelewa wangu Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tz wanashughulikia yale mambo ya Muungano, wakati ambao Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inashughulikia mambo ya yasiyo ya Muungano kwa upande wao. SWALI: Mambo yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanganyika chombo gani kinayashughulikia? Kumbuka si sahihi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tz kushughulikia mambo yasiyo ya muungano ya upande mmoja tu.

Hii ni point kubwa, Pindi mzanzibari atakapokuwa raisi wa JMT, maana yake ni kwamba kwa yale mambo yasiyo ya muungano mzanzibari huyu atakuwa bado ana final say wakati yeye si mtanganyika.

Kama Mtanganyika hawezi kuenjoy benefits wanazozienjoy wazanzibar huko Zanzibar, wakati huo huo Wazanzibar wanaweza kuenjoy Benefits zote wanazozienjoy Watanganyika kule bara, then huu Muungano una faida gani kwa Watanganyika?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom