Urais wa ZZK 2015 Kupitia Chadema: Kwa nini Wanatetemeka!, Kuweweseka! na Kutishika?!.

Status
Not open for further replies.
Pasco,

..matatizo ya Zitto na mashabiki/wanachama wa CDM yalianza baada ya kuteuliwa kwenye tume ya Jaji Bomani.

..kuna ambao walitaka Zitto akatae uteuzi huo kwa imani kwamba tume hiyo ingekuwa sawa na tume nyingine za serikali, ambazo zimekutumika kuhalalisha uzembe wa serikali.

..wengi waliamini kwamba Zitto atatumika kuhalalisha uzembe wa serikali ktk utiaji saini mikataba mibovu ktk sekta za madini na nishati.

..mashaka hayo yalitiwa nguvu zaidi baada ya Zitto kuonekana "kulainika" kimsimamo baada ya kutumikia kama mjumbe wa tume ya Jaji Bomani. nakumbuka baada ya hapo ndipo Zitto akajitokeza waziwazi akijenga hoja kwamba serikali inunue mitambo ya dowans.

..suala lingine ambalo liliamsha mori wa mashabiki wa CDM ni pale Zitto aliposhindwa kutokea bungeni kuungana na wenzake kutoka nje wakati JK anahutubia. kitendo cha Zitto kilikiumiza chama ambapo mbele ya jamii CDM walionekana kukosa ile nidhamu ya uwajibikaji wa pamoja.

..wanachama na mashabiki wengi wa CDM wanapenda viongozi wao wawe na msimamo mkali dhidi ya CCM na serikali yake. mwanzoni Zitto alikuwa kipenzi na tegemeo la kundi hilo, lakini hapa katikati amewa-disappoint manazi wa CMD kutokana misimamo yake laini-laini, pamoja na siasa zake za mlengo wa kati.

NB:

..binafsi I crossed Zitto off my list kutokana na msimamo wake kuhusu ushiriki wa Tanzania ktk jumuiya ya Afrika Mashariki.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Pasco Mayalla

Pole sana nilikuwa sijakujibu muda mrefu maana naona kila siku anaangaika kwa ajili ya Zitto
Mimi ni CCM damu lakini nakuhakikishia kuwa Zitto anatumika wewe subiri true colour will show.......
Kama ilivyokuwa kwako baada ya kugundulika kuwa wewe ni mwanaCCM mwenzetu ukawa unasema
wewe ni independent advicer mara Political Analysist lakini yote kwa yote hakuna chochote na wewe your
true colour show at the end

Last:.................... Pasco Njaa Mbaya tujenge taifa letu tuache siasa za majungu................

Nilikuwa napitia hiyo mada ya Pasco, ukisoma kwa makini ni kama mtu aliyetumwa na ZZK kuandika hayo, au ni ZZK mwenyewe ameandika, angalia sana anavyojaribu kubold UDINI, UKABILA, UKANDA, nadhani there is no way unaweza kumpatia mtu asiyekuwa na sifa kujaribu post kubwa kwa kuhofia na kutanguliza eti UDINI, UKABILA, UKANDA, nadhani kuna poll iliwekwa humu JF, ili watu bila kujali dini, kabila, kanda, wapige kura wajiridhishe waone kati ya watu wawili tu nani anaweza kupeperusha bendera ya CDM mwaka 2015, mpaka leo ZZK ana kama 15% tu na Yule mzee anayetukanwa sana na CCM ana kama 85% Nadhani asilimia hizi hazina reflection kwenye dini, Kabila, wala kanda ! Dini gani ina watu wanaofika 85% ? kabila gani lina watu wanaofika 85% Kanda gani in watu wanaofikia 85%. Unless mniambie kuwa humu JF wamezidi watu wa dini fulani au kabila fulani, au kanda fulani, WHICH IS QUITE WRONG. Nadhani imefika wakati tujenge hoja, tujadili, tuchambue, tuone ukweli uko wapi ! NAPITA TU !
 
Kuhusu wagombea hawa wawili ni muhimu pia utazame michango ya wanabodi wengi sana hawampendi Zitto na sababu zake zimeelezwa. Pamoja na hayo hatuwezi kudai hakuna Udini, Ukabila wala Ukanda ikiwa sisi wenyewe tunashindwa kuonyesha takwimu ama utafiti wetu wenyewe ktk matokeo kama haya. Na tunashindwa pia kuziba midomo yetu kuonyesha Udini, Ukanda na hata Ukabila..

Siku zote mimi nasisitiza sana kupokea na kuyasikia malalamiko ya WATU wengine, halafu tunajiuliza kwa nini watu wanafikiria hivyo, Je kuna dalili zozote zinazoashiria Udini Ukabila na Ukanda? Tunafanya utafiti wetu na kurudi na majibu na sii tunavyofiiria toka kichwani. Hakika hapa JF tu Upo Udini, Ukabila na Ukanda japokuwa wanaoandika humu sio viongozi wa Chadema lakini chama hakijengwi na viongozi bali wanachama. Ukizungumzia mikoa ya kusini na pwani utawasikia wana Chamdema wakitukana matusi ya nguoni, Ukizungumzia Uislaam utayasikia matusi, Tukizungumzia makabila ya watu wa Pwani utawasikia watu wakisema vibaya kuhusu kabila la rais. Ni tabia mbovu sana ya wana Chadema ku generalise hili lipo na wala tusilipinge maana hata mimi hunikwaza sana naposoma hoja za baadhi ya wana Chadema.
 
Pasco,

..matatizo ya Zitto na mashabiki/wanachama wa CDM yalianza baada ya kuteuliwa kwenye tume ya Jaji Bomani.

..kuna ambao walitaka Zitto akatae uteuzi huo kwa imani kwamba tume hiyo ingekuwa sawa na tume nyingine za serikali, ambazo zimekutumika kuhalalisha uzembe wa serikali.

..wengi waliamini kwamba Zitto atatumika kuhalalisha uzembe wa serikali ktk utiaji saini mikataba mibovu ktk sekta za madini na nishati.

..mashaka hayo yalitiwa nguvu zaidi baada ya Zitto kuonekana "kulainika" kimsimamo baada ya kutumikia kama mjumbe wa tume ya Jaji Bomani. nakumbuka baada ya hapo ndipo Zitto akajitokeza waziwazi akijenga hoja kwamba serikali inunue mitambo ya dowans.

..suala lingine ambalo liliamsha mori wa mashabiki wa CDM ni pale Zitto aliposhindwa kutokea bungeni kuungana na wenzake kutoka nje wakati JK anahutubia. kitendo cha Zitto kilikiumiza chama ambapo mbele ya jamii CDM walionekana kukosa ile nidhamu ya uwajibikaji wa pamoja.

..wanachama na mashabiki wengi wa CDM wanapenda viongozi wao wawe na msimamo mkali dhidi ya CCM na serikali yake. mwanzoni Zitto alikuwa kipenzi na tegemeo la kundi hilo, lakini hapa katikati amewa-disappoint manazi wa CMD kutokana misimamo yake laini-laini, pamoja na siasa zake za mlengo wa kati.

NB:

..binafsi I crossed Zitto off my list kutokana na msimamo wake kuhusu ushiriki wa Tanzania ktk jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkuu Joka Kuu, kwanza nakushukuru kwa objectivity yako na frankness kumhusu ZZK. Kwa vile nafahamiana na ZZK, naanza kuchelea kujibu baadhi ya post humu nikaonekana nimetumwa na ZZK hivyo mimi ni mouthpeace yake!.

Katika hayo uliyoyasema, kosa la ZZK ni lile lile kuwa mkweli tuu much hivyo kujikuta anashindwa kufanya baadhi ya mambo ambayo Chadema kama chama wanayafanya ila kwake ni kinyume cha dhamira yake. Imetokea tuu mimi kujikuta nina side na ZZK kila anapo tofautiana na Chadema. Kwenye kutoka nje, he did what was best kutokuja kabisa!, angekuwa ni msaliti kama ange turn up na asitoke nje!.

Hili la Chadema, kujifanya kutomtambua rais, nililisema sana hapa Chadema Yakubali Yaishe! Yamtambua Rais kimya kimya!, Yampongeza!. baadae Marehemu Regia akanitaka niombe radhi hapa,Pasco Tuombe radhi CHADEMA-Umemwelewa Vibaya Hon Mbowe na mimi kibinaadamu niliomba radhi hapa,Nawaomba radhi wana CHADEMA, nilimwelewa vibaya Mhe. Mbowe ila ukweli unabaki unasimama kuwa Chadema ilijifanya haimtambui rais kwa kauli "expresilly" na mpaka leo haikuwahi kuifuta kauli ile, huku imanafanya matendo "impliedily" yanayothibitisha kumtambua rais!. Hili la kumsusia JK, Dr. Aliendelea nalo, hata JK alipojitoa kuja msiba wa Regia pale Tabata, Dr akawa hapatikaniki, JK akatia timu mpaka Kilombero hapa lazima wangekuta, mpaka masizishi yalikwisha bila kusalimiana!, Kwa nini Dr. Slaa Amenuniana na JK?! - Chadema wakakaribishwa "chai" Ikulu, Dr. akagoma, hatimaye mbio za sakafuni zilimalizikia ukiongoni, jamaa walikutana, wakashikana mikono waka hug hostilities zikamalizika, Chadema sasa inashirikiana vizuri na serikali katika baadhi ya mambo, lakini kauli ya "hatumtambui rais" bado imesimama!. Kwa vile ukweli daima husimama, na kwenye siasa, The end justifies the means, pamoja na yote Chadema iliyoyafanya kwenye kususa, at the end of the day, all was wrong, and ZZK ndio yuko right!.

Hata ule msimamo wa ZZK kuhusu ununuzi wa mitambo ya Dowans au kuitaifisha, he was 100% right!. Stta, Mwakyembe and their team are dam wrong!, and belive me, tozo ya ICC lazima tutailipa!, at the end of the day, ni sisi Watanzania, mimi na wewe ndio tutailipa the last price and feel the pinch!.

Hata hivyo pamoja na kumsupport ZZK, lazima pia nikiri, ZZK ni binadamu tuu kama wengine hivyo na yeye anayo madhaifu yake, mfano uongozi ni team work, na ZZK is not a good team player ndio maana haonekani kwenye hadhara za M4C na huu ni udhaifu wa ZZK na nimeishamwambia hapa Urais wa ZZK 2015: Ngoma Ikivuma Sana...!.

All and all, pamoja na yote haya, wanaChadema, haswa manazi wa Chadema, lazima wa change their atitutes towards some issues nazo nimezizungumza hapa Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!
P.
 
....uh! kamanda..naechelea kwamba kwa ukweli uliousema (mi naukubali wote, pamoja na kuwa mchungu ka shubiri)...subir uone maneno mbofu mbofu yatakayoelekezwa kwako...kwa kosa gani? kuuchambua ukweli kama ulivyo...salute kamanda!!!!
 
Thanks Mkuu COMRADE CHRIS HANI, ukikubali kuwa mkweli, lazima uwe tayari kukubali matokeo including to pay the price!. Miongoni mwa gharama ni kuchukiwa "an anemy of the people"!. Humu jf nimeisha zoea kubezwa, kutukanwa, kudhihakiwa but at the end of the day, kweli itasimama!.
 
Kama ilovyo TBC yako kumbe akili zako nazo ndivyo zilivyo ? Najua wewe ni mtumwa huko ila sikutegemea mawazo duni kama Duni wa KAFU kama haya
 
Mkuu Pasco

Last:.................... Pasco Njaa Mbaya tujenge taifa letu tuache siasa za majungu................
Kiukweli kilichonisukuma kuandika haya ni njaa tuu!. Nimeyaandika hayo ili nivute kitu kidogo kutoka kwa ZZK ili angalau mkono uende kinywani, tumbo lijae, siku ipite!, kesho nitafuta issue nyingine ya kuvutia fungu!, and that is how I survive!.
P.
 
mkuu unahangaika sana na issue ya zito,mbona ulishasema wewe sio chadema sasa kelele nyingi za nini,
Kwa hiyo wenye right ya kuzungumza mambo ya Chadema, ni Chadema wenyewe?, hivyo huo uongozi wanaotafuta ni kuwatawala wanachama wao tuu?, mimi kama Mtanzania, nina haki ya kutoa maoni yoyote kuhusu chama chochote au mtu yoyote anaetafuta public office ili tusije ingizwa chaka!.
P.
 
Pasco,
Kwa hiyo wewe mathalan una binti ana miaka 15 halafu mtu akakwambia kuwa akifikisha miaka 18 atakuja kumposa utajisikiaje? Kwa nini asisubiri mtoto afikishe hiyo miaka 18(umri wa mtu mzima) ndio aje kuposa?
Mkuu Safari ni Safari, as a mater of fact, I'm a father of six!, 3 boys na 3 girls, 4 of them ni teens!. Kama mzazi nazungumza pont blank na watoto wangu kuhusu choice za marafiki zao!, ninawaeleza mabinti zangu all about men kwa dose ndogo ndogo according to their age!. Tena nimewaruhusu wawalete rafiki zao nyumbani ili kama mzazi uonde kinds of associations na kuwapa muongozo ili kesho na keshokutwa waweze ku manage healthy friendships ikiwa ni pamoja na kuwatoa out from time to time na sio kusubiri vijana ndio wate kunitolea hao mabinti na kuwapeleka vichochoroni!.

Tuna miaka 3 tuu kabla ya uchaguzi, we need ample time kuwapima hawa wanaotaka uongozi wa taifa letu!. JK ndio huyu ametuingiza chaka, unazubiri mpaka 2015 surprises names ziibuke tuingizwe chaka tena?. What is wrong kuonyesha nia mapema ili watu wakupime according to vigezo?!.
 
EL na ZZK wako kambi moja.
Kama unadhania, kitendo changu cha kumpigia debe EL ndio niko kwenye kambi yake!, you are wrong!, so do kambi ya ZZK kama ipo!. Mimi huwa na express my opinion freely, sina chama, sina kambi, sina upande zaidi ya kuweka mbele maslahi ya taifa!.
 
Zito ataanzisha chama chake hawezi kwenda ccm this soon, (ego yake haimruhusu). atapewa zawadi ya uwaziri mwandimizi au hata PM pindi EL akishinda kama zawadi kwa ZZK kusplit kura za upinzani. Hii itakua serikali ya umoja na EL atajidai kukuza demokrasia nchini na kuapa kua kiongozi wa kila mtu ikiwemo na wale wengi waliopiga kura za siyo. Ukichukulia kua CCM ina hatari ya kumeguka kutokana na kupitishwa mgombea EL, zzk anaonekana kama ni mtu muhimu kwenye kufanikisha urais wa EL kwa kuwanyima kura nyingi CDM pamoja na wale waasi toka CCM hapo 2015..

hii political chess game kuelekea 2015 ni complicated na kutakua na twist and turn kibao, ilawale waliojipanga tokea 95' wana nafasi zaidi.
 
Tuna miaka 3 tuu kabla ya uchaguzi, we need ample time kuwapima hawa wanaotaka uongozi wa taifa letu!. JK ndio huyu ametuingiza chaka, unazubiri mpaka 2015 surprises names ziibuke tuingizwe chaka tena?. What is wrong kuonyesha nia mapema ili watu wakupime according to vigezo?!.

Pasco,
Katika mazingira ya siasa miaka mitatu ni mingi sana. Imagine splits zinazoweza kujitokeza ndani ya chama ikiwa kila mtu anaamka na kusema anataka kugombea. Ni kujenga makundi amabayo kuja kuyavunja ni kazi kubwa baadae.
 
Kwa mara ya kwanza heading ya Thread ya Pasco tu imenifanya nisione umuhimu wa kusoma habari yenyewe kwasababu zifuatazo;

1) Heading tayari imeshatoa picha halisi ya mtizamo wake hivyo naamini maandiko mengine yamejaa utetezi wa anachokiamini ambacho kupitia heading tumeshafahamu ni nini!!

2) Mtizamo wake kupitia hiyo heading(naamini hata contents ni chai hizo hizo tu) ni potofu kwasababu sioni kiongozi ninayehisi anaweza kugombea urais kupitia CDM nje ya Zitto (wale most probable) anayeweza kutishwa na Zitto tena ukichukulia mtizamo wa wananchi na wanachadema kuhusu Zitto (hata kura humu JF zinajionyesha si za kupuuza).

3) Wako wachambuzi wa mambo ya siasa huru pamoja na itikadi zao hapa JF(mfano Mchambuzi) lakini wanaheshimu maslahi ya taifa na wanatoa hoja zanye lengo za kujenga lakini sio Pasco (mara nyingi ni mpotoshaji) na lazima umsome ukiwa na chujio asikujaze mambo yenye hila za kinafiki hasa kama hujui kinachoendelea.

Hitimisho, sasa tumechoka upotoshaji wa makusudi wa nini sisi wapenda mabadiliko(mfano mimi si mwanachama wa Chadema) tunalalamika juu Zitto.mnaongea ukabila,udini kwakujifanya mnaelimisha kumbe ndio mnazidi kupigilia misumari ya ukabila na udini.

Hakuna kiongozi wa CDM aliyelalamika rasmi au hata kusikika pembeni (kama kuna aliyesikia atuambie humu) kuhusu Zitto na Urais ukitoa muasisi wa CDM ambaye nae ni mtoa maoni kama akina siye.

Narudia tena acheni kupotosha malalamiko yetu kama wapenda mabadiliko hasa upotoshaji kama huu wa eti kutetemeka,kuweweseka na kutishika maana kuna thread nyingi humu tumeandika malalamiko hayo mpaka sasa inaboa kurudia!!! Hayo ni maneno ya kinafiki kutoka kwa mnafiki na ipo siku maandiko yenu haya haya yatawavua nguo.

Hatutaki tena mjadala wa Zitto labda pawepo na tukio la msingi,otherwise mnatuhujumu tusijadili mambo ya msingi yaliyojaa mbele yetu.
 
Mpango huu ni miongoni mwa njama zinazoandaliwa kwa ajili ya Chama Tawala kuangamiza upinzani wa kisiasa nchini.

Mgombea binafsi wa kiti cha urais ama ubunge atakuwepo kwa mujibu wa Katiba Mpya ijayo. Zitto utashawishiwa kugombea nafasi mojawapo kati ya hizo mbili nje na Chama ulichopo sasa. Kisha utaahidiwa uwaziri wa fedha ama madini. Utategwa ujichagulie kati ya nafasi hizo. Lengo litakuwa ni kuhakikisha unajiengua CHADEMA ili kusababisha mgawanyiko katika idadi ya wapiga kura waliowaumini wa vyama vya upinzani, CHADEMA ikilengwa.

Nawe Zitto utashawishika kwenda huko, utagombea urais, utashindwa lkn utakuwa umefanikiwa kuleta mgawanyiko ktk suala zima la wapiga kura. Ila hutaachwa hivi hivi, utapewa ubunge wa kuteuliwa kama ilivyo kwa Mtu Makini Joseph Mbatia, kisha utaingizwa Serikalini kuchukua mojawapo ya hizo nafasi nilizokutajia hapo juu.

Sasa hilo litakuwa ndiyo ANGUKO lako la jumla katika siasa za Tanzania, nawe utafuata nyayo za Waridi Amani Kaborou.

Yawezekana hulijui hilo lkn laandaliwa na laja kwa ajili yako. Tafakari wewe ni kijana mwenye uwezo mkubwa wa kufikiti. FIKIRIA

Mimi tu kukuletea habari.

We kichwa sana,unabusara na uwezo mkubwa sana,maneno ulioyaongea mazito,mimi ni shabiki wa Zitto lkn nimelegea,Zitto umakini unatakiwa ktk kuzichanga karata zako.
 
Kama unadhania, kitendo changu cha kumpigia debe EL ndio niko kwenye kambi yake!, you are wrong!, so do kambi ya ZZK kama ipo!. Mimi huwa na express my opinion freely, sina chama, sina kambi, sina upande zaidi ya kuweka mbele maslahi ya taifa!.

Mkuu Pasco hujanisoma, sijasema unamtumika yeyote hapo, nilimjibu Tiqo aliyekutuhumu kuwatumikia mabwana wawili.
 
Pasco unapoteza nguvu nyingi hivyo kwa ajili ya kujadili urais wa zzk kweli,
hivi kwa kuwaza tu ni mtanzania yupi atakayempigia kura huyu dogo ili aweze kuwa rais.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom