Urais Wa Tanzania NOOOMA!!!!!

NGUVUMOJA

JF-Expert Member
Jul 1, 2011
1,347
325
Ni ukweli usiopingika kwamba Tz ina magonjwa mengi mno. Karibu kila nyanja inaumwa, tena kibaya zaidi nyanja zingine zimegubikwa na magonjwa sugu!!!!
Tunaambiwa na 'Great Thinkers' kuwa kila Mtu anastahili apate mahitaji yake muhimu ya kibinadamu ili maisha yake hapa duniani yawe muruwaaa.
1. Ale chakula kizuri chenye virutubisho
2. Alale kwenye nyumba nzuri (ikiwezekana iwe na umeme na Maji ya uhakika sio mgao)
3. Akiugua apate matibabu ya uhakika (Madaktari na Madawa yawepo)
4. Watoto wasome kwenye Shule za uhakika (Walimu na vifaa vya shule viwepo)
5. Na mengineyo ya muhimu
Sasa unapokuwa Rais wa Tz. wakati unahangaika kuweka sawa timu yako ya Mawaziri na Serikali kwa ujumla ili uyafanyie kazi kikamilifu masuala hayo muhimu, baadhi ya watendaji wake wanakuhujumu. Kibaya zaidi ni kuwa mengi ya magonjwa umeyarithi toka kwa 'Wastaafu'.
Pia baadhi ya wananchi wanakuvua nguo kwa matusi na kejeli nyingi kamasio kurushiwa vinyesi. Kila unavyowafanyia mema wananchi ndio matusi zaidi badala ya shukrani.
Watanzania kweli wanakatisha tamaa. Wana hamu ya Rais Dikteta ama vipi?????
Urais wa Tanzania noooooooma kweli hata sina hamu nao.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom