Urais, Halima, Nassari na Kigoma

Status
Not open for further replies.
Hivi kwani kuna ubaya gani Nasari na Halima wakitamani ZITTO awe rais? how is it different from those who wish Membe au Lowasa kuwa rais?

Nadhani ushauri wangu kwa ZITTO ni kuwa makini na hili la urais, historia inaonyesha wote wanaaoutaka saaaana hawaupati.
 
Twende taratibu Zitto:
1. Je kuna uhusiano wowote wa Moja kwa moja kati ya Mwasiti Almasi na kamanda Halima Mdee, Joshua Nassari, na
hao waheshimiwa wa magambaEsther Bulaya, Deo Filikunjombe bila CONNECTION yako?
2. Je ni kwanini unadhan kamanda Mdee na Nassari wamekana kilichoandikwa na Mwananch?
3. je ni kwanini hiyo Story itoke kwenye gazeti la mwananchi pee yake na siyo mengine?

ni hayo kwanza ikija video nitaendelea isipokuwa imechakachuliwa

Hili nalo neno! kama ipo insubiri nini kuwekwa? Au mpaka ipitie kwanza maabara? Kwa jinsi huyu Zitto alivyo na tamaa ya haya madaraka ya juu anaweza kufanya lolote huyu- nasikitika huyu bwana amegeuka liability ndani ya CDM kama yule mwingine aliyetangaza nia kwenye mkutano wa CCM!
 
Zitto wewe n mnafki namba moja katika siasa za Tanzania undumilakuwili wako ipo siku watanzania watakuhukumu kwa matendo yako tatanishi ndani ya chama chako huaminiki hata ndan ya jamii ya watanzania kwa sababu zifuatazo
1.Huna uzalendo bali una umimi 2.Ndan ya chama chako umekua tofauti na wenzako katika maamuz ambayo ni halali kiitifaki 3.Mahusiano yako na baadh ya viongoz wa usalama wa taifa ambao nh wahusika wa matukio tata katika kuzuia jamii kudai haki zao za msingi 4.Mahusiano yako na ROSTAM AZIZ .Zitto umechafuka unahtaj kujisafisha ili kurudisha imani yako kwa watanzania jibu Mh. ZITTO
 
........ukitumia kiasi kidogo cha ubongo kufikiri/kutafakari nyuzi hii, utagundua inaelekea hawa wabunge (Mdee na wenzake) walisema hayo maneno, anyway tusubiri hiyo video isije ikawa ni tamnthilia ingine hii.
 
Zitto naye kaleta mipasho tupu humu, Nassari kakana, Halima Mdee naye kakana, wewe unakili baada ya Mdee na Nassari kukana iyo taharifa ndio imeleta mjadala ktk jamii, kwa maana iyo kwa nini hii thread yak ukuiambatanisha na iyo video hili huo mjadala umalizike badala ya kuongezeka.

Alafu kwa nini kila siku ni wewe Zitto unaleta kauli tata? Mbona Dr.Slaa na Kamanda Mbowe, Mnyika hawapo hivi? unafikili Uraisi hawautaki? au hawana ushawishi ktk jamii?
Kabla ya kufika 2015 inabidi tufanya kazi kubwa sana kukijenga chama mpaka ngazi ya chini, viongozi wote wa chadema chungeni kauli zenu popote mnapopata nafasi ya kuzungumza.

Mimi ni kiongozi wa kata chadema, kata yangu tunakabiliwa na ukosefu mkubwa sana wa bendera, makao makuu hakuna bendera za chama, wananchi wanataka kufungua majiwe ya msingi ya chadema ila bendera hakuna, sasa wananchi wanapowasikia viongozi wao wanaongelea URAISI 2015, unafikiri watawaelewaje?

Tujenge chama kwanza, tuachane na kauli tata. ccm imeshakufa imebaki kuzikwa tu 2015.
 
Last edited by a moderator:
Hivi kwani kuna ubaya gani Nasari na Halima wakitamani ZITTO awe rais? how is it different from those who wish Membe au Lowasa kuwa rais?

Nadhani ushauri wangu kwa ZITTO ni kuwa makini na hili la urais, historia inaonyesha wote wanaaoutaka saaaana hawaupati.
Siyo kweli....JK aliutaka saaaaaana na akaupata. Leo Lowassa na Zitto wanautaka saaaaaana na wataupata. Kumbuka
kuwa Tanzania na wananchi wake ni shamba la bibi....sijui tumelogwa!
 
Miezi ya nyuma nilileta hii mada hapa jukwaani lakini kwa bahati mbaya MODs waliinyofoa dakika 20 baada ya kuiweka. Sina budi kurudisha hii mada baada ya sakata la Zitto Kabwe, Nassari, Alima Mdee pamoja na gazeti la Mwananchi. Kwa muda wa miaka kadhaa sasa, nimekuwa katika tasnia ya habari na lazima nikiri kwamba mengine yanayofanyika katika hii tasnia ni ya kukatiza moyo hasa kazi za wanahabari zinapoingiliwa na wanasiasa. Kwetu sisi wanawake inakuwa ni vigumu sana kukataa kutii haya maagizo ambayo mengine unaona kabisa ni za vitisho

Zitto Kabwe, January Makamba, Bernard Membe na hata Ngeleja kwa siku za nyuma alishiriki sana katika kuingilia kazi za waandishi. Kinara wao akiwa Zitto January na Membe. Hawa viongozi hasa Zitto wamezoea sana kujiandikia makala na hata habari kisha kumlazimisha mwandishi kuzichapisha ukurasa wa mbele kwa gharama yoyote ile. Wanatoa hela nyingi sana kwa waandishi na wahariri. Mbaya zaidi ni kwamba hawa viongozi wanajitengenezea kashfa au kutoka ndani ya vyama vyao.

Matokeo yake kesho wanaitisha waandishi tena kukanusha (kashfa) zao za kujipikia wakati ni wao ndio chanzo cha hizo habari. Lengo lao kubwa ni kutafuta huruma kutoka kwa umma wa kitanzania kwa vitu ambavyo havipo.
Kinachonishangaza ni kwa nini mtu ajichafue kwa kujitengenezea kashfa maadui feki ndani ya chama chake heti ndio wanaomchafua kumbe ni yeye mwenyewe alafu kesho yake akane hizo taarifa? Nadhani tunaelekea kubaya hawa watu wakiendelea nah ii tabia. Moja ya habari hizi ni zile zinazomlaumu Mbowe kam mtazikumbuka..

nawakilisha
Katika utawala na siasa za nchi, kila mwanasiasa anatakiwa kuwa na ushirikiano mzuri sana na waandishi wa habari. Na maadam nchji yetu ni ya mkono uendao kinywani nawapongeza sana Zitto, Makamba, Na Membe kwa kuelea kwamba mwanasiasa unatakiwa ku control media. Mtachukia na kuwasema kwa mabaya lakini ndivyo Rostam alivyoweza kutukamata.. Huwezi kutumia UTU na Uzalendo wakati wote hata kama unashambuliwa na huna pa kushtaki..

Labda tatizo ya swala hili zima ni kama Makamba, Zitto na Membe wanaifanya kazi hii wao wenyewe bila kutumia mtandao lakini kisiasa hakuna uharamu kabisa unless kwa kutumia media unajaribu kuzuia habari za makosa ya ubadhilifu iwe ufisadi, wizi, na kadhalika. Siasa ni mchezo mchafu sana na ukiingia ni sawa na kuingia nyumba ya anasa - Casino. Kipimo cha uzalendo ni wewe mwandishi if you can be bought..Na ikijulikana mhariri au mwandishi unaweza kununuliwa basi unatakiwa kufukuzwa kazi wewe sio swala wala makosa ya mwanasiasa kujipamba gazetini..

Mwisho, binafsi yangu nilidhani kweli Zitto amepania kugombea mwaka 2015, maana kutangaza nia ya kugombea sidhani kama ni makosa isipokuwa makosa ni kufanya kampeni na maandalizi kabla ya wakati wake (binafsi yangu hili nalo sii kosa)... Nina hakika kabisa mtu yeyote anayetaka kugombea urais mwaka 2015 by now na kisha weka nia yake. Kama kweli hakuna mtu aloweka dhamira na nia kugombea mwaka 2015 basi hizi ndizo sababu hatupati viongozi bora maana watu wanakurupushwa tu na kupewa usukani.

Vyama havina maandalizi yoyote kama rais ila wana maandalizi ya kugombea urais kazi ya miezi mitatu inakuwa muhimu zaidi ya kazi ya miaka mitano. For that, Katiba lazima ibadilishwe ili tuwaandae marais wetu kwa miaka na watuonyeshe uwezo wao ktk mamlaka walokabidhiwa kabla ya kugombea..

Hivyo maadam Zitto naye anakanusha yaliyoandikwa ktk gazeti la mwananchi, basi sioni sababu hata ya kuweka hizo video..Habari hii ni ya Uongo nani anapenda kuuujua Uongo? Kama ingelikuwa kweli na Zitto kweli amepania kugombea urais hapo mjadala ungependeza zaidi na hizo video zingeleta starehe. Maadam ndivyo sivyo, am not interested tuwaachie wenyewe watu wa GP.
 
Sipendi kuwa mnafiki kwenye hili, na nimependa mheshimiwa Zitto kaja mwenyewe! Kwa miaka kama minne iliyopita Zitto umekuwa busy sana kutengeneza PR yako, both internally and world wide! Najua unajitengenezea mazingira ya urais!!

Najua unajua kuwa hili suala litakiua chama chako, na nina uhakika u kazini, kutimiza malengo ya upande wa pili. Wakati wa kampeni 2010 nilifuatilia sana nyendo zako and for sure, you had a mission accomplish!!! Naamini chama chenu kita utaratibu wa kuzima wazandiki kama wewe, naomba watumia instruments mlizonazo kuzima hili jaribia lako! Katika maeleza yako kuna maswali mengi zaidi ya majibu, na hili linanipa mashaka sana juu ya uadilifu wako mbele ya chama.

Nasema acha undumilakuwili, tutaanza kuamini jinsi mnavyotutumia wananchi kwa kisingizio cha changes!! Kama kweli mna dhamiri nzuri kwa mtanzania, kwa nini mnakimbilia IKULU? All of you guys, naona mnapigana vikumbo tu..... haya twasubiri tuone mkuu...

Nawasilisha.
 
Ninachokiona hapa Zitto anawajibia Mwananchi.Ukisoma taarifa yote ya Nassari na Mdee hakuna mahali popote wanamtaja Zitto bali wanakanusha habari ya gazeti kuwalisha maneno.Sasa ningemshauri Zitto awaachie Mwananchi wathibitishe au wakanushe madhali kasema hakualika waandishi.Hiki anachokifanya Zitto nadhani ni kuanzisha vita isiyo na maana yoyote kati yake na wabunge hao wa chama chake.Huo ni ushauri wangu kwake.
Hii inathibisha kauli za watu huku kuwa Zitto huwa anaandika habari na kuzipeleka magazetini wachapishe! Huyu bwana ni wa hovyo tu.
 
Ninachokiona hapa Zitto anawajibia Mwananchi.Ukisoma taarifa yote ya Nassari na Mdee hakuna mahali popote wanamtaja Zitto bali wanakanusha habari ya gazeti kuwalisha maneno.Sasa ningemshauri Zitto awaachie Mwananchi wathibitishe au wakanushe madhali kasema hakualika waandishi.Hiki anachokifanya Zitto nadhani ni kuanzisha vita isiyo na maana yoyote kati yake na wabunge hao wa chama chake.Huo ni ushauri wangu kwake.

Kweli mkuu kamanda Zitto asiwasemee gazeti la mwananchi, kwakuwa hata habari ya ramadhani semtawa kuonekana kutumiwa nae kutengeneza habari za uchonganishi dhidi ya chadema hajataka kuisemea. Ingawa pia amefanya jambo jema kujitokeza hadharani kuelezea kile anachokifahamu juu ya habari hii iliyotaka kuzua kizaa zaa.

Mimi bado nasubiri hiyo video anayosema ipo na ataitundika kwenye blogu yake. Nadhani baada ya hapo tutaweza kuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuujua ukweli na kuuchambua uongo.
 
Last edited by a moderator:
Malumbano haya ni mabaya sana...

Lakini once again my young Zitto try to be yourself acha kuwa na haraka be sober watu wanataka kukutumia kama daraja kuficha maovu yao baada ya kuona una ambition ya kuwa kiongozi....

Please and please hala hala mti na macho. From the inner most of my heart take this advice from me hata kama wana nguvu vipi hawatakuwezesha kufikia malengo yako na kinyume watakuharibia. You stand a big chance if you are to be sober na kuamini kuwa wakati ukuta...

Kama unajali dhamira yako na uko radhi kuukubali ukweli pamoja na kuwa sometimes ni mchungu lakini kama zilivyo dawa ziponyazo zikiwa na the same kind of attributes basi kaa chini sikiliza tena mwangwi huu unaousikia once usomapo maneno haya that... be yourself na kwa wakati ufaao utafikia malengo yako kwa furaha na amani...Ukiona vipi potezea tu!
 
kwanza amemanza kwa kujitoa kwamba hakuandaa tamasha na wala hakualika waandishi wa habari...melezo yake humu yanaoonyesha mwendelelezo wa uchonganishi kati yake na wabunge wenzie...
 
Zitto ndugu yangu wewe ni mnafiki. Hii tabia umekuwa ukiifanya kwa muda mrefu. Unaleta habari tatanishi tena muda mwingine unajijengea kashfa feki alafu kesho yake unarudi kuikana. Mwenendo wa leo ni hule hule. Nina uhakika 100% kwamba kuna mkono wako mwananchi. Na wewe pia hilo unalifahamu kaka yangu. hii tabia ni mbaya hachana nayo. madaraka tunapewa na wananchi usiyalazimishe. niliwahi kukuambia hii miaka miwili nyuma tulipoonea kule dodoma

mwendo ni hule hule muke ya muzungu. Hachana na Zitto kabisa.
 
Mkandara tatizo langu ni mikanganyiko katika statement ya Zitto!! Haileti maana, mi naona anjichanganya tu.

Mimi naamini Zitto kaanza siku nyingi tu kujitengenezea uzoefu...!! Siasa za bongo zime-copy na kupesti muundombinu wa CCM, hawana jipya tofauti linahusisha ukweli na uwazi juu ya nia za watu kugombea urais!!! Akianza now chama kitasambaratika ndo maana nakanusha awe safe! Anasubiri muda ufike wanyukane vizuri!!
 
Last edited by a moderator:
Kwa kuwa tumejuzwa kuwa tutaujua ukweli punde, kwa sasa ,itoshe tu kutamka kuwa hii mitafaruku inayojitokeza inakera sana.
Tofauti kabisa na UDP, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kama taasisi inayojiandaa kukamata dola inatakiwa iwe makini na ichunge namna inavyoenenda.

Aidha kila mwanachama anawajibika na anategemewa ashiriki kujenga taswira chanya ya chama kuelekea 2015.

Pamoja na mambo mengine, CCM , kama chama kinachojiandaa kuachia dola, ilipoteza umoja ,amani ,utulivu na utengamano kwa matamko na matendo ya hovyo na sasa inalipa gharama.
 
Hivyo maadam Zitto naye anakanusha yaliyoandikwa ktk gazeti la mwananchi, basi sioni sababu hata ya kuweka hizo video..Habari hii ni ya Uongo nani anapenda kuuujua Uongo? Kama ingelikuwa kweli na Zitto kweli amepania kugombea urais hapo mjadala ungependeza zaidi na hizo video zingeleta starehe. Maadam ndivyo sivyo, am not interested tuwaachie wenyewe watu wa GP.

Mkuu Mkandara ni muhimu sana hiyo video ije hapa ili kila mmoja apate nafasi ya kuujua ukweli. Pamoja na kwamba zitto amejaribu kuandika hiki alichokiandika hapa ambacho unasema amekanusha lakini ni ukweli kwamba hajakanusha maneno yanayodaiwa kusemwa na josh nasasary na halima mdee bali amesema hata yeye alisikia kile kilichoandikwa na gazeti la mwananchi.

Na utaona alivyolisifia sana gazeti la mwananchi, sasa hapo lazima ujiulize swali la nyongeza ni kwanini analisifia sana mwananchi wakati ndilo linalotuhumiwa na wadau kwamba analitumia kutengeneza habari za chokochoko ndani ya chadema? na hapa tumegundua kwamba kuna wanasiasa ambao kwa macho ya nje tunawaona ni tumaini la watanzania kumbe ndani ya mioyo yao wana agenda zao za ubinafsi.

Hata kama kutumia media ni jambo jema lakini kwa mwanachama mwenzetu kutumia media kuleta mifarakano ndani ya Chadema si jambo la kuungwa mkono katu. Mambo ya membe na january makamba hayo yabaki huko huko ccm walikozoea kutumia media kumalizana, kama baba yao jk alivyozitumia kuwamaliza washindani wake, kwetu Chadema tunasema hapana, siasa hizo za kumalizana hatuzitaki.
 
kwanza amemanza kwa kujitoa kwamba hakuandaa tamasha na wala hakualika waandishi wa habari...melezo yake humu yanaoonyesha mwendelelezo wa uchonganishi kati yake na wabunge wenzie...


mwasiti anayemtaja kuandaa tamasha na kuwaalika waheshimiwa naye hakuhusika kuwaalika hao wabunge, sasa sijui ni nani aliwaalika!!??
 
WADAU NAOMBA NIWE NABII WA KISIASA.

ZOTTO amekuja hapa kiutata kama ilivyo kawaida yake,hakuna kijana aliyekuwa katika mawazo yangu kwa siasa za tanzania kama Zitto, huyu bwana ana kampeni chafu ndani na nje ya chama muda mrefu sana nitatoa mifano.

huyu jamaa yupo kinyume na mipango ya chama iwe mizuri au mibaya.
huyu bwana ana marafiki ambao ni adui kisiasa na chama chake.
huyu bwana hajawahi kukanusha au kukubali madongo ya kikanda na kidini yanayoelekezwa kwa chama chake.
huyu bwana ndiye aliyewaunganisha wasanii kutoka kigoma kwa hiyo chochote kitakachofanyika kitakacholihusisha kundi hilo lazima kina mkono wake.

Wabunge walioalikwa kigoma ilikuwa ni mkakati maalum wengine wakijulishwa na wengine wakifuata mkumbo bila kujijua. angalia koment zake kuhusu hili suala hapo juu, anataka kutuaminisha kuwa kama Mdee na Nassari wametamka hayo maneno basi watakuwa wamewasemea watanzania na hapo itakuwa halali kwake kuendelea kukiyumbisha chama chake.

Jamani kuna chama kimoja kimeanzishwa kwa hela chafu na mpango mchafu wa kusambaratisha upinzani wa ccm wanahusika na mpango huo na kuna mawaziri waandamizi walishaahidi kuwa baada ya muda mfupi chama kikuu cha upinzani kitasambaratika kama nccr mageuzi na kama hicho chama viongozi wake hawatakuwa makini na viashiria vya chokochoko wa baadhi ya marafiki wa maadui wao kisiasa ni lazima watakamatwa na mtego huo ulioandaliwa, kigezo kikuu cha kukisambaratisha hicho chama ni udini na ukanda kwa mbali.

Haya matishio bado yangali mabichi kama watajidanganya kuwa wananchi wa tanzania ni waelewa kiasi hicho naomba niwe wa kwanza kutabiri kifo na msambaratiko wa kutisha kwa hicho chama.

MTANIAMBIA.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom