Urais CHADEMA moto 2015: Dk Slaa, Mbowe, Zitto hapatoshi

CCM AMBAYO KWA VYOVYOTE LAZIMA ISHINDE UCHAGUZI UJAO HATA IKIWAHI NDANI YA KATIBA MPYA:

Maneno niliyoyapigia mstali yanaonyesha kuwa unaipenda siasa ila haujakomaa ktk siasa za ushindani. Hapana sababu ya kupendekeza mgombea wa urais 2015 eti kwa ajiri ya kutoa ushindani tu bila lengo wa kuingia Ikilu. Na kama lengo ni ushindani tu bila nia ya dhati ya kuikomboa nchi toka mkoloni mweusi CCM basi hatuna sababu ya CHADEMA kuingia kwenye uchaguzi wa 2015. Tusipende kukatishana tamaa kwa vita iliyopo mbele yetu, kwani tulio wengi ni matumaini yetu kuwa 2015 Tanganyika itakombolewa rasmi na kurudisha matumaini yaliyopotea baada ya kifo cha baba wa Taifa ( Nyerere). Ushindi ni lazima ndio moto wa wafuasi wa ukombozi wa nchi hii. Matumaini na mawazo ya watanzania ni kwamba 2015 tuwachague wahuni wengine maana waliko sasa basi kwa usanii wao. KUGOMBEA UONGOZI NI LAZIMA IWEPO NIA YA DHATI YA KUONGOZA WATU NA WALA ISIWE KUSINDIKIZO TU.
 
Sidhani kama Chadema wana hilo,hiyo ni style ya CCM kufikiria madaraka kila baada ya uchaguzi. 2010 mnakumbuka ilivyokuwa mbinde kumshawishi Slaa asimame kugombea
 
Hii habari imekaa kama ya kuuzia gazeti, sikutegemea kama Mwananchi lingeripoti habari kama hii

Kwanza, muda bado na sidhani kama ndani ya CHADEMA kuna mwelekeo wa kimagamba

Wwaliotajwa mmoja kashawahi kugombea na mwaka jana akampa nafasi mwenzake, hata kama anapenda kugombea tena nafasi itapatikana bila zengwe, kupigana vikumbo ni habari ya udaku udaku na kimagamba magamba.

Zitto Kabwe alishasema hatagombea, na hata kama ikitokea akabadili msimamo na akawa na sifa binafsi na za kikatiba kugombea hahitaji kupigana vikumbo maana uwezo wake unajulikana.

Dr Slaa aligombea mwaka jana, uwezo wake unajulikana kwa watanzania, kama akiamua kutogombea tena ndani ya CHADEMA kuna hazina kubwa ya viongozi ukiachana na hao waliotajwa, swala la kupigana vikumbo halipo
Mkuu usitake kutuaminisha kwamba CDM inaongozwa na malaika kwa hiyo ikifika siku ya kumpata mgombea urais basi itapatikana tu! Kwa kuwa CDM haina mgombea urais aliyepitishwa kwa hiyo kila mtu ana nafasi ya kuomba ridhaa ya wana CDM wakati ukifika.

Lakini pamoja na hayo ni kwamba ubinadamu wa kawaida unasema kwamba ili uweze kufanikiwa katika jambo lako unatakiwa ujiandae na mpango mkakati ambao huwa si chini miaka 3!
 
Kwani mnamtaka Slaa tu ndio awe mgombea pekee wa urais Chadema?
 
Wana JF,

Itakuwa vizuri zaidi tukajikita katika kujadili mchakato wa katiba.Tujadili maudhui ya katiba mpya ili tupate katiba bora kabisa ili tufike kwenye demokrasia ya kweli na tujenge Tanzania tuitakayo miaka 50 ijayo kuanzia sasa

Kwa wanachadema,tujadili namna bora ya kutunga sera mbadala na tufikirie zaidi kujiimarisha kama timu ili ifikapo 2015 tuingie kwenye uchaguzi mkuu tukiwa hatuna mgogoro wala makundi.Tukiimarishe chama chetu,tunayo fursa ya kuendelea kusaidiana na viongozi wetu wa ngazi zote na tuweke miundombinu itakayotupatia viongozi bora watakaotupeleka 2015.Wakati wenzetu wanagawanyika basi tutumie fursa hii kujiimarisha ila kwa tahadhari ya hali ya juu ili tusije tukaingia kwenye mtego wa kutegemea udhaifu wao tu

Tuweke mikakati mizito,tuzibe mianya yote na udhaifu uliokuwepo uchaguzi uliopita.Tunayo dhamira moja,naamini chama chetu kitatoa mgombea bora 2015 bado.Kitu cha msingi tuepuke ubinafsi tualenge kwenye maslahi mapana ya chama na taifa letu kwa ujumla.Uchaguzi wowote au uteuzi ndani ya chama chetu ni lazima tuuweke kwenye mizani ya 2015,ni uchaguzi wa Transitional team.

Ni wakati muafaka kwa wanachama na viongozi kupima aina ya kauli tunazotoa vinywani mwetu,sio muda wa kutoa reckless statements.Tuwekeze na tuimarishe kitengo chetu cha research.Ni muda wa uwajibikaji zaidi na kila mmoja awe evaluated kupitia results zinazoonekana

Kuna mgombea/wagombea wa chama tawala wanajitahidi kujitenga na udhaifu wa serikali iliyopo ili kujenga aura ya messiah ajaye.Watanzania tusidanganyike.Wanajitahidi kujifanya wanaguswa na matatizo ya vijana ili kuteka kundi la vijana ambao ndio mtaji mkubwa wa vyama na wagombea urais 2015.Tuitumie taasisi ya BAVICHA katika hili na kitengo cha research.Tusiingie kwenye mtego wa majungu kama wenzetu.Pia katibu mkuu na secretariat wanajituma tuwaongezee nguvu

Tujipange kikamilifu kwani uchaguzi ujao utakuwa mgumu sana,naamini CHADEMA itaweka historia.Tupanue mtandao,tuimarishe safu ya uongozi na kuhakikisha umoja na mshikamano ndani ya chama,tufanye tafiti za kutosha tuandae ilani ambayo itakuwa the best na itakayo sustain transition kwa kuzingatia waathirika wakubwa na walengwa ambao ni kundi kubwa la vijana katika aspect zote
 
Siku hizi maoni ya watu yanafanywa heading kwenye magazeti. Au ndiyo mbinu za kuifanya CDM nayo ionekane ina migogoro kama CUF, NCCR mageuzi na CCM? Uzushi, hakuna mbio za urais CDM muda huu. Utaratibu wa kumpata mgombea ndani ya CDM upo wazi kabisa wala hatuna shaka na hilo. Magezeti yaache kuchochea vitu ambavyo havina msingi.
 
Sio jambo baya kutamani urais;nina uhakika CHADEMA watakuwa makini kuchagua mgombea wao,ingawa haihitaji unabii kuona kama slaa ATAOMBA;HAKUNA MWENYE UBAVU WA KUMSHINDA KWA SASA!
 
Hakuna kitu kama hicho ndani ya Chadema kwa wakati huu, CCM wameanza kujihisi aibu baada ya kubainika ni wao tu wenye tamaa ya mzee fisi sasa wanahangaika kuwaambukiza wengine.
 
Hakuna kitu kama hicho ndani ya Chadema kwa wakati huu, CCM wameanza kujihisi aibu baada ya kubainika ni wao tu wenye tamaa ya mzee fisi sasa wanahangaika kuwaambukiza wengine.

Wanataka tutoke nje ya ajenda za kitaifa.Kuna thread nyingine kule inaendelea
 
Siku hizi maoni ya watu yanafanywa heading kwenye magazeti. Au ndiyo mbinu za kuifanya CDM nayo ionekane ina migogoro kama CUF, NCCR mageuzi na CCM? Uzushi, hakuna mbio za urais CDM muda huu. Utaratibu wa kumpata mgombea ndani ya CDM upo wazi kabisa wala hatuna shaka na hilo. Magezeti yaache kuchochea vitu ambavyo havina msingi.

Tena ndani ya Chadema kamati kuu ndiyo inaomba watu kugombea.Tena wanabembelezwa
 
hamna hata mwenye sifa hapo. kuwa wabunge tu wameshindwa kuzuia nepotism, sasa wakiwa rais itakuwaje? think, tundu lissu=christina lissu, wilbroad peter slaa=rose kamili, zitto=some body, mbowe ndo usiseme.
Hakuna hata mmoja mwenye sifa hapo. nyerere amekaa 25years ikulu bila nepotism.

Itifaki yako hiyo imetokea tu coensidency na sivyo kama unavyotaka kutuaminisha hapa jf. Ukiangalia kwenye chati ya viongozi wa cdm ukimotoa Zitto hakuna mwingine aliyejijengea jina kutoka upande wetu sisi akina ...., na Zitto mwenyewe ndiyo huyo yuko very royal kwa JK zaidi ya kwa Dr. S. Tatizo letu sisi ...., huwa tunakuwa kigeugeu mfano mzuri Z mwenyewe. Mpaka sasa hivi hajulikana anawajibika kwa chama kipi hasa.
 
Kwani mnamtaka Slaa tu ndio awe mgombea pekee wa urais Chadema?

Ritz,

Suala la mgombea Urais ndani ya chadema linajulikana kwamba linategemea mchakato wa kidemokrasia na muafaka ndani ya chama chetu. Siyo kama ilivyo kwa CCM ambako hadi wanajimu walitumika kumtishia yeyote ambaye angetaka kupambana na JK. Pia usisahau maneno ya katibu mkuu Yusuf Makamba kwamba alikuwa tayari kufungwa kwa ajili ya JK, yaani demokrasia huko ni mwiko.

Leo hii mgombea urais wa chadema mwaka 2010 Dr. Wilbroad slaa anaonekana mwenye appeal kwa watanzania kuliko Jk na ni tumaini kubwa kwa watanzania.Pia usisahau kwamba Chadema kimejipanga kuwa na hazina kubwa ya viongozi wa baadae.

Dr. Slaa is proof that more can be achieved with his moderate and pragmatic style in Tanzania than with the uncompromisingly hardline stance of much celebrated chaps in CCM. You then , as a focused opposition politician, need a hands-on approach, between election periods, to gain support, visibility and acceptance .

I am just not comfortable with folks thinking they have a divine right to be supported to win when, between elections, those folks do not behave like oppositions who want to win . Anyone who seriously wants to defeat the CCM crew should start their effort now (but without jeopardise harmony and peaceful co-existence within the party) or save us the finger pointing in 4 years time.

I personally believe it is not difficult to defeat the CCM if the opposition has the energy, enthusiasm and ideas to stay the course instead of going to sleep for 4 years and hoping to win magically during election when issues such as the mental divisions of Tanzanians still play a huge part in how people vote

Instead our Politicians in opposition remain indolent before election time yet they want to defeat the Chama Cha Mapinduzi with 3 months of election campaign alone.

NB:
Halafu ukishauri chama chako(just in case you are a CCM Cadre) kirudi kwenye mstari kabla ya 2014 kwani hukumu yenu itakuwa kubwa, utakuwa ni uchaguzi utakao-evaluate falsafa ya maisha bora kwa kila mtanzania kama chama na pia uchaguzi utakaopima confidence ya wananchi kwa mgombea atakayejiita bora lakini ndani ya chama kibovu kisicho na rekodi ya kuwatendea mema watanzania dhidi ya ilani bora na mgombea bora wa chadema
 
Hivi kuna mzungu yeyote atakayethubutu kumnunulia suti Dr Slaa ili apate kibali cha kuendeleza biashara zake hapa? Je, Mbowe ana mshipa wa kukataa kununuliwa suti?

Ushauri wangu, Mbowe aachane kabisa na ndoto za urais kwa sasa, ajielekeze kwenye kuimarisha chama.
Una wazimu wewe aliyekwambia Mbowe ananunulika nia nani? Angekuwa hivyo CHADEMA ingeshauzwa long time, fanya research na kwa taarifa yako "no Mbowe no more chadema" Chama kinaendeshwa na Mbowe wengine woooote wanafuata ideas za Mbowe.

Amekua mbunifu wa mambo mbalimbali ndani ya chama. Uliza uambiwe sio unaropoka tu hapa jamvini
 
Ni vyema kujadili sasa ili waoplan kugombea wajue ni kiongozi wa namna gani tunayemuhitaji. Inawezekana wengine wakajiengua wenyewe tu kukosa sifa tunazozitaka na hivyo kuepusha migogoro inayoweza kuja kujitokeza huko mbele ya safari.

Watanzania ikiwa ni mwaka mmoja tu umepita tangu tutoke kufanya uchaguzi mkuu, na sasa mnatuaminisha tuanze kuwa busy na kujadili tena kiongozi ajae kwa mwaka 2015.
Hii inaonyesha ni jinsi gani hatuna mambo ya msingi ya kufanya au kujadili kama kipindi chote ni kuongelea na kufikiria nani na nani awe kiongozi wetu.?

Muda mbona upo tena wa kutosha kuanzia kwenye vyama vya kisiasa mpaka kwenye tume ya uchaguzi, kipindi kingine kinachobaki ni kwa ajili ya kufanya shughuli za kimaendeleo kwa ajili ya nchi yetu.
 
Una wazimu wewe aliyekwambia Mbowe ananunulika nia nani?????? Angekua hivyo CHADEMA ingeshauzwa long time, fanya research na kwa taarifa yako "no mbowe no more chadema" Chama kinaendeshwa na Mbowe wengine woooote wanafuata ideas za mbowe. Amekua mbunifu wa mambo mbalimbali ndani ya chama. Uliza uambiwe sio unaropoka tu hapa jamvini
 
hamna hata mwenye sifa hapo. kuwa wabunge tu wameshindwa kuzuia nepotism, sasa wakiwa rais itakuwaje? think, tundu lissu=christina lissu, wilbroad peter slaa=rose kamili, zitto=some body, mbowe ndo usiseme.
Hakuna hata mmoja mwenye sifa hapo. nyerere amekaa 25years ikulu bila nepotism.

Kama msanii anaendelea kupeta bila wasiwasi ina ashiria nini, nchi hii inaweza ikatawaliwa hata na kaburi na watu wasifanye lolote! Tatizo tumekosa "UWEZO", NIA ya kumng'oa madarakani tunayo, SABABU za kumtimua tunazo lakini UWEZO ndo hatuna! Tutaendelea kupiga kelele zisizokuwa na maana mpaka muhura utakwisha na ataweka mtu wake anayempenda na hatutafanya kitu!

Kusema fulani hawezi siyo kweli, nchi hii inatawalika kirahisi mno kiasi kwamba hata mkimbizi anaweza kuja kututawala na tusifanye kitu.
 
Back
Top Bottom