Urais 2015 tusimlaumu Zitto: Nani anaujua Msimamo wa Dr. Slaa?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,442
113,452
Wanabodi,

Mara baada ya mazishi ya Mhe. Regia, (RIP), on route back to Dar, nilibahatika kukutana mahali na Katibu Mkuu wa Chadema, Dr. Wibroad Slaa akiwa na wife wake, Fina, tuliendesha maongezi mafupi informally na sio mazungumzo rasmi na miongoni mwa maswali niyomuuliza, ni hili la iwapo atagombea tena nafasi ya urais kwa tiketi ya Chadema katika uchaguzi wa 2015!.

Nayakumbuka vizuri sana majibu ya Dr. Slaa kuhusu swali hilo!. Kwa vile yalikuwa ni maongezi tuu na sio mazungumzo rasmi, sisi waandishi wa habari, ukizungumza na mtu yoyote katika maongezi ya kawaida, huruhusiwi kuripoti mlichoongea, unless kama ulimjulisha utakwenda kuandika, hivyo kuna uwezekano Dr.Slaa alizungumza
"off the record", sio busara kuyaleta mazungumzo ya "off the record" kwenye public na kuyaweka "on the record" bila "idhini" ya msemaji.

Kwa vile msimamo wa "Dr. Slaa kuhusu kugombea urais 2015, mimi naujua!, nawashauri, wale wote wanaomlaumu au kumshutumu Zitto, kwa kuonyesha nia ya kuwania urais wa 2015 kwa tiketi ya Chadema, kwa kujenga mazingira "impliedly" not "expressly"!, wasimlaumu bali wamsupport!.

Hivi kuna ubaya gani, kuonyesha nia ya kuwania the highest office?. Wote wanaoutaka urais, huitwa "presidential hopeful", hivi kuna ubaya wowote to aim high?!.

My Take.
Kwa vile mchakato wa kuwania urais wa 2015 bado haujaanza rasmi kwa vyama vyote, lakini tunashuhudia "presidential hopefuls" wa vyama mbalimbali wakijenga mazingira na mitandao ya uungwaji mkono kupitia mikakati mbalimbali, nawaombeni wapenda demokrasia ya kweli, tuwe open minded kuhusu watu hawa, tusianze kuwanyooshea vidole vya kuwashutumu na kuwakatisha tamaa, bali tunapaswa kuwaunga mkono kwa nguvu zote ili at the end of the day, tumpate mgombea bora kabisa miongoni mwao ambaye atapeperusha bendera ya upinzani na kuwaletea ushindi.

Mfano hakuna ubishi kuhusu uwezo wa Zitto katika masuala ya organization na mass mobilization!, hakuna ubishi kuhusu nguvu ya Zitto katika ushawishi na kujenga hoja zenye mashiko na kusimamia utekelezaji. Kama ni kweli Zitto ni "presidential hopeful" ndani ya Chadema na sasa anajenga mtandao wa kuandaa mazingira hayo, this is very healthy kwa Chadema, kwa sababu by the time muda wa mchakato rasmi unawadia, Chadema iwe na a pool of able people ya kuwa wagombea wake wenye sifa za urais, ikawachuja na kumpata the best na ikampitisha, akitokea kuwa ni Dr. Slaa, then fine, wagombea wengine wote wanavunja kambi zao na ku rally behind Dr. Slaa kupeperusha bendera ya upinzani, hii ndio utakuwa an added advantage kwa ushindi wa kishindo wa Chadema, na Zitto ndio atafaa zaidi kwa post ya Waziri Mkuu, kama alivyofanya Obama na Hillary Clinton!.

Kufuatia mimi kuufahamu msimamo wa Dr. Slaa, lets support Zitto or anybody else!,

Mhe. Zitto, just follow your dreams, "Sky is the limit!".

I wish Zitto all the best!.

Wasalaam.

Pasco. (wa jf).

NB. Pasco wa jf, sio mwanachama, mshabiki au mkereketwa wa Chadema, ni mwanacha wa chama cha siasa bali pia ni muumini wa demokrasia ya kweli.

Update 1.

Kufuatia hoja nyingi ambazo zimeibuliwa na uzi huu, sitaweza kuzijibu zote, bali nazijibu kiujumla jumla humu

Wakuu kwanza lazima nikiri wazi kuwa baadhi ya wapenzi wa Chadema mliojibu uzi huu ni miongoni mwa hazina kubwa sana ndani ya Chadema kutokana na genuinity na objectivity ya majibu yenu makini kwenye hoja hii.

Niliwahi kusema humui kuwa
CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga! - JamiiForums
nilishambuliwa sana. Wapenzi wa Chadema hawakusoma hoja zangu wakaishia kumjadili mtoa hoja!.

Kuna siku nilisema humu jinsi ccm imechokwa mpaka basi!, nikimaanisha there is an opportunity to be seized!.

Siku nyingine niliwaambia chadema, 2015 Ikulu njia nyeupe ila mjipange!, ni wachache waliojibu kwa makini!.

Hiyo siku nilipokaa na Dr. Slaa, nilimweleza reservations zangu kuhusu sio tuu mgombea urais wa Chadema, bali nilieleza kuhusu udhaifu mkubwa wa Chadema katika kuwapata viongozi wake na wagombea wake wa nafasi mbalimbali za uongozi wa ndani ya chama, na nje ya chama, kama serikali za mtaa, ubunge na udiwani.

Nilimshauri Dr, Chadema ianze kuwa na succession plan ya kuwatayarisha viongozi wake from the grass roots levels, kwenye kila posti kuanzia nafasi za uongozi ndani ya chama, hadi nafasi za kugombea serikali za mitaa, udiwani, ubunge hadi urais, badala ya kuwategemea wanaotemwa CCM na kuwadaka tuu. Yes japo wanaotemwa tayari ni mtaji, lakini lazima Chadema kiwe na timu yake, ili kufika mahali hao wanaotemwa CCM kupimwa streghts zao kwa kulinganisha na waliopo, kama aliyepo ni stronger kuliko aliyetemwa, huyo anayetemwa CCM, hapati nafasi kuwa mgombea wa Chadema.

Na ili kujenga Chadema imara, Chadema pia lazima kiwe na internal mechanism yake ya kutafuta wanachama wapya waaminifu na kufanya internal vetting kwa viongozi wake, vinginevyo inaweza kujikuta ina kundi kubwa la viongozi, kumbe wengi ni mamluki tuu na mapandikizi ya waliotemwa CCM na kuhama kwa hasira za ketemwa tuu CCM, lakini mapenzi yao yako bado yako CCM, hivyo wanakuja Chadema ili kupata tuu fursa za kugombea, na wakikosa, mtawashuhudia wengi wakirejea CCM!.

Pia ili kupata a dedicated team ya viongozi imara, Chadema ianzishe mfumo scouting from grass roots levels na kuanzisha succession plan, kuwatayarisha viongozi wake wa kesho by headhunting recruitment of committed leaders, iwafanyie grooming, iwapike, waive, ndipo ije iwape uongozi, mfano sasa hapo ilipo, tayari Freeman Mbowe ameisha overstay as Chairman, Chadema ianze maandalizi ya kutafuta atajayerithi mikoba ya Mbowe kwa kuwapika viongozi wake kwa nafasi ya uenyekiti hadi waive kwa kumuandaa nani atapokea Mbowe uenyekiti, ili kujenga succession plan bila makundi ili kujenga sustainability ya chama chochote sustainable kina succession plan.

Kwenye Chadema haijajipanga niliwaambia kuwa kuna baadhi ya maeneo, watu wameichoka CCM mpaka basi kiasi kwamba hata kama Chadema ingesimamisha jiwe, hilo jiwe lingepita!. Hii inamaanisha kama Chadema ingesimamisha wagombea kila jimbo, saa hizi mngekuwa na wabunge wengi zaidi ya hawa waliopo!.

Miongoni mwa ushauri wangu kwa Dr. Slaa, Chadema isishobokee wagombea maarufu wala kusubiria makapi ya CCM!, good leaders are made and not born!. Nikashauri, Chadema ifanye incouragement kwa wanachama wake wenye uwezo na nia mbalimbali za kugombea, wajitanabaishe tangu sasa ili wapimwe, wawe groomed kuja kugombea mara wakati utakapo wadia na sio kusubiria kipenga cha NEC kipulizwe, by the time kipenga kinapulizwa, the time left will be too little too late!.

Nikatolea mfano wa jimbo la Kinondoni, linashikiliwa na CCM miaka nenda, miaka rudi. Mgombea wa CCM tayari anajulikana, weaknesess zake zinajulikana, kama mimi ni mwana Chadema na nina nia ya kugombea Kinondoni come 2015, nitasema sasa na wote wenye nia wajitangaze sasa ili miongoni mwetu, sote tujue nani ni best kutuletea ushindi, ndipo tumgroom tayari kwa kuiteka Kinondoni na sio kusubiri hadi 2015 na kusubiri CCM itamsimamisha nani!.

Mfano kwa Mwaka 2015, Jimbo Ubungo, kwa vile jimbo limeshikwa na upinzani, CCM huenda itampeleka mtu very strong ili kulikomboa, Jimbo la Kawe, CCM itamrudisha Kippi, na majimbo yote yanayoshikiliwa na wapinzani, CCM itapeleka watu makini, au wenye fedha na very strong, ili kuyagomboa, hivyo kama mimi ni mwana Chadema, najijua uwezo wangu kuiletea Chadema ushindi kwa jimbo fulani ni mkubwa kuliko mbunge aliyepo, mfano jimbo la Kawe ni mkubwa kuliko uwezo wa Halima Mdee kulitetea jimbo la Kawe, nitaonyesha nia sasa kwa kujenga mtandao wa mazingira ya ushindi. Muda kuchukua fomu ukifika, mimi nitachukua fomu kwa jimbo la Kawe, na Halima Mdee nae atachukua fomu, Ben Saanane nae atajaza na Mzee Mwanakijiji pia atajaza, Chadema kitatupima wote, ni nani mwenye uwezo zaidi na chances kubwa za ushindi, kinampitisha kupeperusha bendera ya Chadema, kama sio Halima, then Halima Mdee anakuwa ndio mhamasishaji mkuu wa mgombea mpya wa Chadema Kawe. Baada ya kumuengua Charles Mwera Tarime, niliwaambia makosa yenu na jimbo mlilitoa sadaka bure kabisa kwa kukosa busara!.

Kwa sisi wapenzi wa demokrasia ya kweli ambao japo tuna vyama vyetu, tunaamini hakuna mwana Chadema yoyote, mwenye hakimiliki ya kuhodhi nafasi yoyote ya uongozi kuanzia chini hadi uenyekiti. Nafasi zote za uongozi ndani ya chama na nje ya chama, ni haki ya kila mwanachama mwenye sifa, vigezo na uwezo!. Kama Zitto anazo sifa, vigezo na uwezo, kwanini azuiliwe asigombee?!.

Kwenye ule uzi wangu wa Chadema Hamjajipanga, niliwaambia Chadema kinakabiliwa na tuhuma za "udini" na "Ukaskazini", japo tuhuma hizi sio za kweli, likini zipo na sio za kupuuzwa!. Nikawashauri ili Chadema kiaminiwe na Watanzania wote, wa dini zote na maeneo yote, lazima hilo koti lenye harufu ya udini na ukaskazini, livuliwe!. Nikawashauri Zitto ni mtaji mkubwa sana kwenye kwenye kuondoa dhana hizo potofu, utumieni vizuri mtaji mlio nao kujiongezea mavuno!.

Japo haikuandikwa popote, wagombea wa urais kwa CCM, wanapokezana, Muislamu na Mkristo!. Alianza Nyerere, Mkristo, akaja Mwinyi, Muislamu, akafuatia Ben Mkapa Mkristo, sasa ni JK, Muislamu, anayefuatia is more likely, Mkiristo tena ni Mkatoliki (msiniulize why). Prof. Lipumba, aligombea kama boya tuu ili kuhakikisha kura za Waislamu wasioipenda CCM, zisiende Chadema!. Kama 2015 CCM itamsimamisha mgombea Mkristo na Chadema ikamsimamisha Zitto ambaye ni Muislamu, Prof. Lipumba, hatathubuti kutia pua, maana yake boya halitaweza kufanya chochote!. Chadema itajivunia kura zote za ukanda wa Pwani zilizokwenda CUF!. Chadema itavuna kura za Waislamu wote wenye msimamo mkali walioko CCM, Chadema itavuna kura zote za Watanzania walioichoka CCM, Kundi kubwa la vijana, waliokata tamaa na kuamua kutopiga kura kwa sababu ya watu wale wale, chama kile kile na mambo yale yale, wakimuona Zitto kijana mwenzao anapeperusha bendera ya Chadema kuelekea magogoni, kwanza watajitokeza kwa wingi kujiandikisha na siku ya kupiga kura watajitokeza kwa wingi kupiga kura na watapiga Chadema kura nyingi kiasi kwamba hata CCM waibe vipi, bado hazitaibika, hivyo CCM kuanguka chali, sio tuu kwa kifo cha mende, bali itaangukia pua!. Hivi hizi opportunities zote za Zitto kuwa mgombea urais wa Chadema nyie wenzangu hamzioni?!.

Kwa vile nilishasema toka juzi, jana, leo na kesho nitasema tena, na tena, mimi Pasco wa jf, nina chama na sio Chadema na kiukweli, CCM ndicho chama tawala kilichoko madarakani, namfagilia sana EL kama atakuwa ndie mgombea wa CCM, na nikasema kama afya yake ni mgogoro kuhimili pilika pilika za uchaguzi wa 2015, then the second best candidate kwa CCM awe ni John Pombe Magufuli!, sio nawafangilie ili washinde, bali CCM iwasimamishe wagombea wa aina hii ili muwatumie kama pace makers wenu, ili Chadema mteue wagombea makini wa kuwaletea ushindi na sio kuendelea kuteua wasindikizaji tuu wa mgombea wa CCM !.

Mwenye masikio na asikie!.

Pasco.
12:24 am
 
huu ndio upuuzi tusioutaka humu ndan...wewe peke yako ndio unajua ukweli juu ya dr slaa na hutaki kuusema hapa na wakati huo huo unasema kwa kuwa unaujua ukweli wa dr slaa juu ya hatima ya urais basi tumsapot zitto bila kutwambia hicho unachokijua juu ya dr slaa!!!!......sasa kwa nini umeleta uzi huu hapa? unataka kutuaminisha nini?.....halafu usinikumbush kabisa siku ya mazishi ya regia mtema maana uliharibu kaburi lake kwa kupanda juu eti ukitafuta kupiga picha kama dr slaa atashikana na mkono na kikwete wakati wa kusalmiana.....

wewe ulishasema kuwa uko kwenye Eliairline na juzi hapa membe aliosema ana maadui 11 na watahamia kenya 2016 kama ataoteshwa na wewe ulionekana kumuunga mkono kama ataoteshwa...sasa unakuja na matango pori tena juu ya zitto......huyu zitto tunamdai video aliyosema ataweka humu tangu jana..sasa na wewe usitichanganyie habari sisi...wewe na ramadhani semtawa mko kundi moja!!!
 
CDM haina mambo ya mitandao.Hayo ya mitandao yapo CCM.By the way wewe msimamo wako unajulikana kwamba unamuunga mkono Edward Lowassa kwa hiyo unataka mitandao CDM ili isambaratishe chama mtu wako Lowassa apenye kirahisi.Umechemsha.
 
Zitto kutaka kugombea Uraisi sio tatizo wala sio kosa.. Dr. Slaa kwa maono yangu naona it is better hata yupo kimya on the matter sababu cha ajabu mengi ambayo yanazungumziwa kuhusu Uraisi in relation na Zitto (whether ni kweli ama ni uongo); kimsingi yalitakiwa yajadiliwe ndani ya CDM.

Hili silent tiff lilitakiwa liwe resolved kwa njia za kujenga - In the sense ingekuwa ndani ya CDM wao wangeyajadili then mmoja wao ambae ni muwakilishi aje awakilishe msimamo wao juu ya habari za Zitto na Uraisi in relation na akina Nassari, Mdee et al.

Kosa ambalo kwa wengine linaweza lisiwe apparent ni kitendo cha Zitto kutowa tamko ambalo linakuwa kama linawakandamiza wanachama wenzie... Kwa mtu mwenye akili ni lazima ujiulize huyu mtu ana nia gani? Unakuwa na mashaka kuwa yawezekana zile rumors juu yake za kuvuruga chama ni kweli? Haeleweki kabisa niya hasa na madhumuni yake.

Kwa muktadha huo hata wana CCM ambao wanajua FIKA kuwa CCM ipo ulikingoni mwa maisha yake watataka Zitto ndio asimame kama raisi kuiwakilisha CDM...
 
Wanabodi,

Kwa vile msimamo wa "Dr. Slaa kuhusu kugombea urais 2015, mimi naujua!, nawashauri, wale wote wanaumlaumu au kumshutumu Zitto, kuonyesha nia ya kuwania urais wa 2015 kwa tiketi ya Chadema, kwa kujenga mazingira "impliedly" not "expressly"!, wasimlaumu bali wamsupport!.


Kufuatia mimi kuufahamu msimamo wa Dr. Slaa, lets support Zitto or anybody else!,

I wish Zitto all the best!.

Wasalaam.

Pasco. (wa jf).

Damn!! Who da hell are you???
 
Ooh boy!! mbona umezunguka sana kusema hicho.


Mzee salaam.......wala usipate taabu.....

Composition is an art of which if supported with knowledge and courage then the result will obvious be the expected impact delivered from the content......and if one is not lucky enough to have all these qualities and yet s/he believes to be famous and strong then behind the very brain the thinking is that the later will replace the former pre-requisite.......

Oooh poor believer.....!!!!!!!

Si wote maarufu ni weledi kama wao wanavyopenda kueleweka
 
sasa kama unakiri mchakato bado, ya nini mtu kuanza kujijengea awareness kwa watu wakati utaratibu wa CDM kupata mgombea unafahamika? Zitto, kama ipo, ipo tu lakini mnayofanya sasa ni kama yale ya MAGAMBA na akina SHIBUDA. just keep silent and wait for the procedure.!
 
Pasco wa jf, sio mwanachama, mshabiki au mkereketwa wa chama chochoite cha siasa, bali ni muumini wa demokrasia ya kweli. Haaaaa wapi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
ni kweli kabisa,sio kosa mtu kutaka kuwa kiongozi wa nchi hii.lakini pia naona kama mh. zitto anapaswa akae chini atulie and ajifanyie tathimini mwentewe.binafsi zito ni mwakilishi mzuri wa wananchi andamekuwa akifanya vizuri kazi zake.chaajabu,ni njinsi jammii anayoiongoza ilivyokuwa na mtazamo hasi(-) kwake.mie namshauri zitto atulie maana jinsi siku zinavyoendelea,amekuwa akihusishwa na tuhuma kibao ambazo sio nzuri,ajiulize ni wapi anakosea maana asipotulia magamba watamtumia and mwisho wa kuwa tegemeo kwa wananchi utafika.zitto skando zimekuwa nyingi sana bana,utadhani msanii kumbe kiongozi na mwakilishi wa wananchi.
zito wa zamani anapotea anaelekea kuwa zito mambo leo.tafadhali mh.turejeshee yule zito mwenye uchungu na nchi hii anayefanya kazi yenye maslahi kwa wote.hivyo vya urais mie sitaki kuviongelea maana maamuzi yapo kwa wanachama wenzio.
 
Tunasubili video aliyotuahidi. Na kwanini aanze kujenga uadui na wenzake kina Mdee na Nasari kama kweli nia yao yote ni moja ya kukijenga chama.
 
[h=2]Urais 2015 tusimlaumu Zitto; Nani anaujua Msimamo wa Dr. Slaa?[/h]
Kwani kuna kuna uhusiano gani kati ya ugombeaji wa Slaa na wa Zitto au mwanachama mwingine? Kwamba kuna watu wanataka Slaa kwanza akatae ndio wengine waruhusiwe? Kwani CHADEMA wanapeana nafasi, au ni mchakato wa mchujo? Naona hapo umeandika kama Ponda wa sensa!
 
Back
Top Bottom