Urais 2015, Rushwa vyaitesa CHADEMA

Nalitazama jambo hili kwa jicho kali lenye utafakari wa kutosha, yawezekana kabisa uwepo wa kundi hilo linalompinga zitto ni ishara ya ukomavu katika siasa za kidemokrasia, lakini nachelea kusema kuwa njia zinazotumika zaweza kuwa ni za kimafia na zisizo za kidemokrasia kabisa.

kuna umafia zaidi ya kupeleka watu mabwepande?
 
hakusema atagombea mwaka 2015, anautaka urais, na anajua hana sifa na ndio maana anaomba kupewa
 
hakuna chama duniani ambacho hakina makundi duniani. hata nchi za magharibi kunakuaga na makundi. nakumbuka 2008 obama na mama clinton walikua na makundi yao. lakini tofauti ya sisi na wao ni
wao wanauchaguzi wa haki na usawa. huku ccm watatumia fedha chafu. chadema watahakikisha lazima mtu wa kaskazini ashinde.kwa ujumla nchi zetu zina udini naukabila,
 
..........................................
Lakini wanaompinga wakidai amechafuka kwa tuhuma za ufisadi na hivyo hawezi tena kuwa mgombea sahihi wa kiti hicho wanatoka zaidi katika mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Mara ambayo ipo kaskazini mwa Tanzania.

..........

Haha....Bado hujaweka Nyanda za Juu kusini(Msigwa na Sugu), Kati ukanda wa Singida(Lissu), kwani hao ni vinara wa Kanda zao na nchi nzima.

Unajua hofu mara nyingine zintokana na kutojua..ndio maana wazee wetu walikuwa wakitambika wakati radi zikipiga, wenzetu walikuwa wakifanya earthing.Sishangai ukipokea kirahisi habri za kuchekesha kuhusu CDM.Mbona kwa CCM sasa hivi familia imeamua na kutangaza wazi hakuna wa Kaskazini kushika nchi?Hujaweza ona hilo?
 
TandaleOne mawazo yako na mwigulu ni sawa kabisa au ndio wewe mchemba mwenyewe ,endelea kuficha id yako
 
Hivi kwa enzi hizi unafikiri kwa mawazo ya kizee kama haya utaisambaratisha CDM! Kajipange upya na mbinimpya zaidi!
 
Unaonekana kama si mzee basi unamawazo ya kizee, na mbinu za kizamani, huwezi kushawishi! In short you are myopic!
 
TandaleOneTandaleOne Hii tittle ya Dissertation yako mpelee Nape aipitie kabla hujaileta kwa External halafuu hii Tittle Magamba wengi wameshaitumia sana Sugua kichwa uje na Nyingine kama
1: Lema anashirikiana na Mashoga japo hii imeshatumiwa na Ritz
2: Chadema ni Wezi wa Mali za Umma
3: Dr Slaa ameoa
4: Mtoto wa Mbowe Anasoma shule za kisasa badala ya shule za kata
5: Chadema wachochea Vita Malawi
6: Chadema inasambaza Ebola

This is rubbish kama huna cha kusema afadhali ukalale
 
bado naamini kabisa kambi ya upinzani.inakazi kubwa sana kujipanga ili kutoa mgombea wa 2015, so far nikionacho humu ni matusi na kejeli kwa kila atakae jaribu kugusa suala hili hasa upande wa CMD, tumieni hoja na vielelezo kufikisha points zenu na sio kejeli na matusi.
 
TUNTEMEKE
anajua yote ya wizi wa dr.slaa na mbowe Jana kaweka uzi hapa wa kufichua namna dr slaa alivyo vunja katiba akamchambua vizuri sana.Mods wakaiondoa haraka sana waliogopa umma utajua namna dr.slaa alivyokosa sifa za uanachama
 
kwa chama makini,huu ni wakati muafaka wa kuanza kuandaa mgombea wa urais

kiongozi haandaliwi,ndo yaleyale ya dr slaa kusema kwamba hakutaka kugombea ila aliombwa,sasa kuna maan gani kuwa na kiongoz asie na uthubutu?uongozi ni uthubutu,uwezo na mvuto wa kisiasa kwa jamii.zitto ameonyesha uthubutu ,uwezo na ana mvuto kwa makundi yote ya jamii.kiongoz ni yule anaejitathimini na kujiandaa kuingia ulingoni
 
SAFARI ya CHADEMA kuelekea 2015 na ndoto za kuingia ikulu zinazidi kupaa kwa Chama hiki kikuu cha Upinzani Bungeni.

HATUA ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, Zitto Zuberi Kabwe ya kutangaza nia yake ya kutaka kugombea urais mwaka 2015 na sakata la tuhuma za rushwa bungeni, vimekifanya chama hicho kigawanyike makundi makubwa matatu yanayovutana.ambapo kila kundi lina msimamo wake, hali iliyosababisha kuzuka kwa mvutano wenye mkanganyiko mkubwa na kuibua sintofahamu miongoni mwa viongozi waandamizi wa chama chake.


Miongoni mwa waandamizi ,Watatu waliojitokeza waziwazi kumkemea huku kwa visingizio tofauti wakiwemo mwasisi wa chama hicho, Mzee Edwin Mtei; Mwenyekiti wa Taifa wa sasa, Freeman Aikaeli Mbowe na Katibu Mkuu, Dk. Wilbroad Peter Slaa.

Hata hivyo ZITTO alipuuza makemeo hayo na alichukua hatua ya mbele zaidi kwa kusisitiza kauli yake hiyo katika Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, kwa kusema kuwa anaitaka nafasi hiyo na anaimudu, na pia ana uwezo mkubwa wa kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama huku akitamba kwamba ni MWADILIFU na MZALENDO.

Ikiwa kashi kashi hiyo inaendelea kwenye Chama, Karibuni ZITTO ametajwa kuhusika katika sakata la RUSHWA katika TANESCO, ambapo kashfa ya tuhuma hizo za rushwa ziliibuka baada kauli yake ya kuwatetea maofisa waandamizi wanne wa Shirika la Umeme.

Kuhusika kwa Zitto kumeibua mtafaruku ndani ya Chadema. Viongozi, wanachama na wafuasi wa chama hicho wenye msimamo mkali wa ukabila na ukanda wanapinga kwa kelele nyingi uwezekano wowote wa mbunge huyo kugombea urais wakitoa sababu tofauti (ambazo kabla ya hili la rushwa, sababu nyingi hazikuwa za msingi).

Jumatano iliyopita, Zitto aliwashutumu baadhi ya wabunge kutoka nje na ndani ya Chadema akidai wanatumika kumpakazia tuhuma za rushwa kutokana na sababu za kisiasa. Alisema wengine hususan wapinzani wenzake wanaitaka nafasi ya Uenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC). Pili, alisema wapo wanaofanya hivyo wakilenga kumchafua hasa baada ya kutangaza kutaka kugombea urais mwaka 2015.

Kuibuka kwa makundi hayo kumeelezwa na vyanzo hivyo vya habari kuwa kumegawanyika kimikoa. Wengi wanaomuunga mkono wanatoka mikoa ya Kigoma, Geita, Kagera, Tabora, Rukwa na Katavi na baadhi ya mikoa iliyopo kusini.

Lakini wanaompinga wakidai amechafuka kwa tuhuma za ufisadi na hivyo hawezi tena kuwa mgombea sahihi wa kiti hicho wanatoka zaidi katika mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Mara ambayo ipo kaskazini mwa Tanzania.

Hata hivyo, sehemu kubwa ya mikoa iliyobaki haijaingia katika mvutano huo wa kisiasa, lakini imeelezwa kwamba baadhi ya wabunge wa Chadema nao wanampiga vita kwa siri na vya wazi, lakini wapo baadhi ambao wapo upande wake na wanamuunga mkono katika harakati zake hizo kuelekea urais.

Miongoni mwa wabunge wanaotiliwa wasiwasi kuwa inawezekana ni mmoja kati ya wale waliogusiwa na Zitto lakini bila ya kutajwa majina yao kwamba wanainyemelea nafasi ya Uenyekiti wa POAC ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu

Hali ya vita ya Urais ni JINAMIZI zito ambalo linaelekea kuimaliza CHADEMA moja kwa moja, kwani wapo baadhi ya viongozi ambao wanaamini katika wao tu na si mwingine na ambao wamejitengenezea wigo na ngome imara ya kujilinda ili kuhakikisha nafasi hiyo inabki kwao na kutumia mbinu mbalimbali hasa kwa kuwachafua wenzao ili wao wabaki pekee katika kinyang'anyiro hicho. Shibuda alijaribu japo kwa UTANI tu na alijadiliwa zaidi ya mara 5 katika vikao vya maadili kwa kitendo chake hicho cha kusema anataka urais akiwa chama hiko.

Zitto ndo anauweza uraisi,, achaneni na hao wegne,,,
 
Mimi nilijua tu huyu babu anaoa lazima akifilisi chama na ndo dalili za michango kila Kukicha
 
safari ya chadema kuelekea 2015 na ndoto za kuingia ikulu zinazidi kupaa kwa chama hiki kikuu cha upinzani bungeni.

Hatua ya mbunge wa kigoma kaskazini ambaye pia ni naibu katibu mkuu wa chama hicho, zitto zuberi kabwe ya kutangaza nia yake ya kutaka kugombea urais mwaka 2015 na sakata la tuhuma za rushwa bungeni, vimekifanya chama hicho kigawanyike makundi makubwa matatu yanayovutana.ambapo kila kundi lina msimamo wake, hali iliyosababisha kuzuka kwa mvutano wenye mkanganyiko mkubwa na kuibua sintofahamu miongoni mwa viongozi waandamizi wa chama chake.


Miongoni mwa waandamizi ,watatu waliojitokeza waziwazi kumkemea huku kwa visingizio tofauti wakiwemo mwasisi wa chama hicho, mzee edwin mtei; mwenyekiti wa taifa wa sasa, freeman aikaeli mbowe na katibu mkuu, dk. Wilbroad peter slaa.

Hata hivyo zitto alipuuza makemeo hayo na alichukua hatua ya mbele zaidi kwa kusisitiza kauli yake hiyo katika bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania, kwa kusema kuwa anaitaka nafasi hiyo na anaimudu, na pia ana uwezo mkubwa wa kuwa amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama huku akitamba kwamba ni mwadilifu na mzalendo.

Ikiwa kashi kashi hiyo inaendelea kwenye chama, karibuni zitto ametajwa kuhusika katika sakata la rushwa katika tanesco, ambapo kashfa ya tuhuma hizo za rushwa ziliibuka baada kauli yake ya kuwatetea maofisa waandamizi wanne wa shirika la umeme.

Kuhusika kwa zitto kumeibua mtafaruku ndani ya chadema. Viongozi, wanachama na wafuasi wa chama hicho wenye msimamo mkali wa ukabila na ukanda wanapinga kwa kelele nyingi uwezekano wowote wa mbunge huyo kugombea urais wakitoa sababu tofauti (ambazo kabla ya hili la rushwa, sababu nyingi hazikuwa za msingi).

Jumatano iliyopita, zitto aliwashutumu baadhi ya wabunge kutoka nje na ndani ya chadema akidai wanatumika kumpakazia tuhuma za rushwa kutokana na sababu za kisiasa. Alisema wengine hususan wapinzani wenzake wanaitaka nafasi ya uenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma (poac). Pili, alisema wapo wanaofanya hivyo wakilenga kumchafua hasa baada ya kutangaza kutaka kugombea urais mwaka 2015.

Kuibuka kwa makundi hayo kumeelezwa na vyanzo hivyo vya habari kuwa kumegawanyika kimikoa. Wengi wanaomuunga mkono wanatoka mikoa ya kigoma, geita, kagera, tabora, rukwa na katavi na baadhi ya mikoa iliyopo kusini.

Lakini wanaompinga wakidai amechafuka kwa tuhuma za ufisadi na hivyo hawezi tena kuwa mgombea sahihi wa kiti hicho wanatoka zaidi katika mikoa ya arusha, manyara, kilimanjaro na mara ambayo ipo kaskazini mwa tanzania.

Hata hivyo, sehemu kubwa ya mikoa iliyobaki haijaingia katika mvutano huo wa kisiasa, lakini imeelezwa kwamba baadhi ya wabunge wa chadema nao wanampiga vita kwa siri na vya wazi, lakini wapo baadhi ambao wapo upande wake na wanamuunga mkono katika harakati zake hizo kuelekea urais.

Miongoni mwa wabunge wanaotiliwa wasiwasi kuwa inawezekana ni mmoja kati ya wale waliogusiwa na zitto lakini bila ya kutajwa majina yao kwamba wanainyemelea nafasi ya uenyekiti wa poac ni mbunge wa singida mashariki (chadema), tundu lissu

hali ya vita ya urais ni jinamizi zito ambalo linaelekea kuimaliza chadema moja kwa moja, kwani wapo baadhi ya viongozi ambao wanaamini katika wao tu na si mwingine na ambao wamejitengenezea wigo na ngome imara ya kujilinda ili kuhakikisha nafasi hiyo inabki kwao na kutumia mbinu mbalimbali hasa kwa kuwachafua wenzao ili wao wabaki pekee katika kinyang'anyiro hicho. Shibuda alijaribu japo kwa utani tu na alijadiliwa zaidi ya mara 5 katika vikao vya maadili kwa kitendo chake hicho cha kusema anataka urais akiwa chama hiko.

wewe ikome kagera, wanakagera siyo wajinga kiasi cha kumsupport mzandiki na mnafiki kama zzk tuna heshima zetu na usithubutu tena kutudharirisha. Hebu mwone!
 
wewe ikome kagera, wanakagera siyo wajinga kiasi cha kumsupport mzandiki na mnafiki kama zzk tuna heshima zetu na usithubutu tena kutudharirisha. Hebu mwone!

shemeji lazima umsupport slaa kwa sababu nyumba za mzee zote kaweka jina la dada yenu.katelelo noma mzee hapindui wala hachomoi.nasikia alikuja huko kagera vp mlimpa senene!bigup sana mshumbusi indelea kumlea babu!
 
Back
Top Bottom