Urais 2015: Mtei amshukia Zitto

Zitto ndoto zako ni sahihi lakini gari unayosafiria ndio mbovu,haikukubali
 
zzk ataharibu chama ameanza kuleta mipasuko ndan ya chama nawashaur kamati husika ndan ya cdm ishughulikie hil
 
Political adolescence inatesa sana.

Mama Asha Rose Migiro jiandae kwa KURA yangu 2015.
 
Aaah mkuu are you afraid that I `m gonna expose your dirty game? Do I need a reward for expressing my view? Hell no! what I do is engaging in political correction; by the way I did ask some question in my previous post I am still waiting for the answers; I will up for next hours waiting for explainations why Zitto is feared by Chadema top brass .

Chama
Gongo la mboto DSM

Chama kama mnadhani Zitto anafaa kuwa rais wa TZ kwa nini msimuite aje CCM asimame kugombea kwa tiketi ya CCM, kwa nini iwe CDM?
 
Zitto nakushauri utulie, nia yako imeshajulikana tuachie watanzania tuendelee kulitafakari.
 
Sitashangaa iwapo Zitto atafuata nyayo za Lulu kwenda mahakamani kutaka umri wake utambuliwe kivingine (japo watatofautiana malengo Ukubwa/Utoto) endapo kigezo cha umri kitambana kugombea hapo 2015
 
Hivi nyinyi wapenzi wa Chadema, bado hamjajua ZZK ndio mtaji wenu pekee wa ushindi 2015?(Sababu ni muislamu au?). Jee mnajua CCM itamsimamisha Membe?(Waislamu hawatampigia kura Membe sababu ni mkristo), sasa kwa vile huyo mgombea kipenzi wetu na Membe hawana tofauti katiuka zile kampeni za "kivile",(wote wakristo (Membe na Slaa) na hamjajua kwa mujibu wa katiba mpya, ili chama kishinde urais wa JMT, lazima kipate angalau theluthi moja ya kura za Visiwani!(99% Waislamu), hivi huyo mgombea wenu kipenzi (Dk Slaa-Mkristo), kwa siasa zetu "zile", hizo theluthi ya kura kutoka visiwani zinatokea wapi?!.

ZZK anakubalika sana kutokana na kuendesha "strategic politics" kwa urafiki wake na January Makamba(Muislamu), atazivuna kura zote za vijana wa CCM!, kwa urafiki wake na Jussa(Muislamu), atazivuna kura zote za CUF (Wanachama wake karibia woote waislamu) kule visiwani. Kwa usomi wake, atazivuna kura zote za vijana/wasomi na wataka badiliko ya kweli with clear goals na right strategies!.Nafikiri mtakuwa mmemuelewa kwanini anataka ZITO awe Rais,Viongozi wa CHADEMA haya ndio baadhi ya mawazo ya wanachama wenu kaeni chini muyapatie ufumbuzi!VIVA CDM!

Nani alikuambia January Makamba ni Muislam?
 
Mwanzoni nilidhani chadema itatuongoza na kutupeleka nchi ya ahadi ifikapo 2015 lakini kwa jinsi mambo yanavyoendelea ndani ya chama safari baaaaado sana na km hamtashtuka na kujipanga vzr CCM itatawala milele na mtabaki kulalamika wakati tatizo liko kwenu wenyewe. Why is it tht everyone is against zitto, whts the secret behind? So mmeshindwa km chama kukaa ndani ya vikao na kuwekana sawa mpaka mmehamia kwenye vyombo vya habari,,,zitto zitto zitto me nshawachoka, jipangeni


Unajua sababu ya lowasa kusema akifikia daraja atavuka? Membe nikioteshwa ntagombea urais, sitta ni mapema mno, January makamba sina mpango wa kugombea urais zitto Mimi ndio chaguo la Wana CDM, ndio Rais 2015 Hata bro JK ananikubali hajui Kama katba itabadilika na kumruhusu? Hajui nec ya CDM Kama itampitisha? Hashirikiani na wenzake kujenga chama JIULIZE ki umri, kielimu nk nani angetakiwa kukimbia kimbia Kati ya slaa na zito? Zito anaonekana sababu ya CDM nani kwenye mitandao sio kwa mwananchi wa chini...democrasia bila sheria na busara ni fujo zzk sio chochote ndani ya CDM
 
Hivi uenyekiti wa CDM Zitto alipotangaza nia akabaniwa kigezo kilikuwa umri? Wazee wa CDM hawana tofauti na wachawi..
Na Nyerere aliposema JK bado tatizo lilikuwa ni nini?
Pamoja na democrasia lakini pia kuheshimiana kama wanafamilia ni njia nzuri ya kutufanya wanachama tuzidi kuwa na imani na chama, sio dhambi wala uhaini kutangaza kugombea urais lakini kama una hekima utajiuliza mbona wewe tu kila mara, wenzako wako kwenye mapambano, wanalima jua lao, mvua yao, virungu na mabomu ya machozi wapigwea wao wewe kila siku kiguu na njia mara uholanzi mara ujerumani halafu ghafla ooh mimi nitagombea urais, kwa mavuno yepi? waliyolima wenzako?.......Zitto tunakupenda, tunakuheshimu umekuwa mwanga mzuri kwa vijana tangu ulipoingia bungeni lakini kwa makusudi unaipa hekima kisogo......utalaumiwa sana kama utakuwa kikwazo cha mabadiliko Nchini......Tafakari.
 
Kwa nafasi na heshima yake ndani ya CHADEMA kauli ya Mtei ni nzito na inapaswa kuchukiliwa kama kauli ya chama.Yaweza kuchukukliwa kama kauili yaa chama tukiamini haata Nyeree aliendelea kuwa na saui na kauli hata baada ya kung'atuka katika chama na serikalini.Aliendelea kuaminiwa kwa kuwa wananchi waliamini matamko na maonyo yake yalikuwa yakisukumwa na 'nia njema' huku akitishwa na udhaifu wa upinzani kwa wakati huo.Hakika,nasi, sasa tunapaswa kuogopeshwa na udhaifu wa CCM.
Mwenye busara na hekima ataelewa na atabadilika.
Nina hakika kauli ya Mwasisi wa chama inawakilisha msimamo wa Katibu Dkt Slaa..Na ninaamini vile vile, kuwa huo ni msimamo pia wa Mwenyekiti Mbowe.Katika uzinduzi wa M4C Dar Es Salaam ,Mbowe alitamka ''siongozi chama cha wasaka urais... sasa tunajenga chama" .
Tunapoona wakuu wengine wa Chama wapo kimya, tuyakosea sana tukifikiri wanaunga harakati za ''watangaza nia'' mapema.La hasha.
Mhusika ,sasa,anapaswa aheshimu kauli ya Mzee Mtei .Asipotendea kazi ushauri wake nia hofu hakuna mwingine atakayesikilizwa na huyu ndugu yetu presidential aspirarant.Vinginevyo tunahitaji kauli ya Kamati Kuu.
Kuna mwanajamvi anadai eti Barack Obama alitangaza nia tangu mwaka 2004!
Jibu langu kwake ni kuwa ,ndani ya Tzanzania,tunajenga chama katika mazingira na nyakati tofauti kabisa na zile za Marekani .Mwaka 2004 tayari chama cha Democrats kilikuwa kimewahi kushinda urais na kuongoza nchi mara nyingi kabisa na kabla ya 2004 nchi ya Marakani ilikuwa tayari na kiwango cha juu cha demokrsia kutokana na kuwa wananchi wengi wenye kiwango cha juu cha uelewa wa masuala ya uraia(strong civic competence).Kwetu hapa ,baadhi ya variables hizo bado zipo katika hatua zake za awali na zingine hazijawahi kabisa hata kutokea.Tunaijenga CHADEMA katika mazingira ya Tanzania huku tukiendelea kuamini katika dhana ya demokrasia.
Kwa sasa tunapaswa kuwaonyesha wapiga kura watarajiwa wa mwaka 2015 kuwa CHADEMA ni chama makini.
Mambo ya urais kwa sasa ni upungufu ama ukosefu wa hekima na busara.
Mwenye masiko na asikie.

A valuable Post! I will not add anything here.
 
Mkuu chama,
Makundi kutoka Kaskazini kamwe hawawezi kuacha kupambana na Zitto, wakikaa kimya ni sawa kumuachia Nguruwe akuchomee mishikaki.

Zitto Kabwe, ana nguvu kubwa kutoka kwenye makundi ya vijana pamoja na wazee, sehemu kubwa ya Tanzania mikoa kama Dar es Saalam, Pwani, Kigoma, Mwanza, Shinyanga, Mwanza, Morogoro, Tanga, Bukoba, Mtwara, Lindi, Singida, Tabora, hawa wajumbe wote wa Chadema wapo upande wa Zitto Kabwe.

Sehemu za Kaskazini ni kweli Zitto hana nguvu zozote za kisiasa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom