Uraia wa Sioi utata mtupu,CCM kutangaza mgombea mpya ARUMERU leo!!

Feedback, japo sina chama na Chadema naikubali sana tuu, ila kwenye uchaguzi wa Arumeru, nasimama na Sioi na machalii wote wa AR wako nyuma yake!. Asipopitishwa na CC leo, ile kambi yote ya Sioi, watashiriki kampeni za CCM, ila kura Chadema!. Kiuhakika bila Sioi, CCM itaangukia pua!.Igunga RA ni muoga kama kunguru siku za mwisho alijitokeza kuokoa jahazi, Sioi asipopitishwa Mmeru No. 1 hatatia mguu Arumeru!, CCM ni kifo cha mende straight away!.

Sijui ni lini umefika Arusha Pasco, ila kwa taarifa yako tu hiyo analysis uliyotoa sio sahihi. Huyu mtoto wabgemwacha aomboleze msiba wa baba yake. He is very young, 2015, sio mbali.
 
This is nonsense, hata kama watu wanamchukia mtu lakini huu ni ujinga wa hali ya juu. Sioi ni Mtanzania , period. Huu ujinga wa kutetea ****** kwa sababu tuu mtu wanayemattack ni mkwe wake Lowassa ni ujinga uliopitiliza. Leo wamemwita Sioi sio raia tunakaa kimya, kesho watakuita wewe sio raia na kutakuwa hakuna wa kukutetea. CCM ni chama chenye ubaguzi wa hali ya juu! Tuliona walivyomwita Salum mwarabu kipindi cha kampeni, yule jamaa wa Tabora walisema ni msomali, sasa Sioi ambaye baba yake ni mtanzania na mama yake pia wanamwita sio mtanzania. The guy is holding a Tanzanian passport and they are saying is not a citizen, this is pathetic.

Kama ni raia mbona kukanusha rahisi tu, aonyeshe ushahidi mambo yaishe.

Birth certificate, declarations nyingine zinazohusika etc.
 
Ninavyoelewa mie, ukizaliwa nje ya Tanzania kwa wazazi wa Kitanzania, unatakiwa ku-declare uraia wako by age 18. Kama hujadai haki ya uraia kwa minajili ya wazazi wako, unakosa haki ya uraia wa Tanzania.

Kama huyu Sioi alizaliwa Kenya, alifanya declaration ya kuuchukua uraia wake wa Tanzania? Kama haja declare si Mtanzania, ni Mkenya.

You are damn right. Section 6 of the Tanzania Citizenship Act 1995 provides that every person born outside the United Republic on or after Union Day shall, with effect from the date of his birth, be deemed to have become and to have continued to be, and with affect from the commencement of this Act shall become and continue to be, a citizen of the United Republic if at the date of his birth his father or mother is or was a citizen Republic on or after Union of the United Republic otherwise than by descent, subject to the provisions of section 30.

Then, section 7 (1) states that any person who, upon the attainment of the age of eighteen years, is a citizen of the United Republic or was a citizen of the former Republic of Tanganyika or of the former People's Republic of Zanzibar and also is or was a citizen of some country other than the United Republic or either the former Republic of Tanganyika or the former People's Republic of Zanzibar shall, subject to the provisions of subsection (8), be deemed to have ceased to be a citizen of the United Republic upon the specified date unless he previously renounced his citizenship of that other country, taken tile oath of allegiance and, in the case of a citizen by descent, made and registered the declaration prescribed by Parliament regarding his intention as to residence.

Sasa kama kweli huyu jamaa alizaliwa Kenya kwa wazazi wa Kitanzania, ilitakiwa akishafikisha umri wa miaka 18, a-rennouce uraia wake ya Kenya wa kuzaliwa, ale kiapo or make declaration kuwa ana intention ya kuwa raia wa Tanzania. Ukiangalia kwa undani wa kulaumiwa wala sio huyo jamaa. It is those who made the law. I can tell very few people know about this law. Kuna watu wengi tuu wamezaliwa nje ya nchi na hawana habari kuwa wakifikisha miaka 18 wanapoteza uraia wao unless they renounced citizenship of other country, taken oath of allegiance or registered a declaration. Ni mpaka pale unapotaka kuingia kwenye siasa ndio unakuja kujua haya mambo.
 
Ninavyoelewa mie, ukizaliwa nje ya Tanzania kwa wazazi wa Kitanzania, unatakiwa ku-declare uraia wako by age 18. Kama hujadai haki ya uraia kwa minajili ya wazazi wako, unakosa haki ya uraia wa Tanzania.

Kama huyu Sioi alizaliwa Kenya, alifanya declaration ya kuuchukua uraia wake wa Tanzania? Kama haja declare si Mtanzania, ni Mkenya.

Watu washaweka vifungu vya sheria, hoja zijengwe kwenye vifungu hivyo sasa na siyo kile unachoelewa. Una uhakika gani na usahihi wa kile unachokielewa? Leta vifungu.
 
Kuna rafiki yangu mmoja alizaliwa Canada wakati wazazi wake wakiwa Chuo Kikuu. Wazazi wakamaliza Chuo, wakarudi Tanzania mshkaji akiwa mdogo sana. Kasoma shule ya msingi mpaka Form six bongo.

Baada ya kumaliza form six, akaanza mipango ya kutafuta vyuo Marekani ili aende kusoma chuo kikuu. Akaenda uhamiaji kuchukua passport, wakamuomba cheti cha kuzaliwa. Akatoa cha Canada. Wakamwambia ulivyofikisha miaka 18 ulikataa uraia wako wa Canada? Jamaa akashangaa, uraia wangu gani wa Canada? Mie baba na mama yangu Watanzania. Akaambiwa wewe raia wa Canada kwa hiyo kaombe passport ubalozi wa Canada. Jamaa kaenda ubalozi wa Canada, kawapa birth cerificate, wakaihakiki, wakampa passport ya Canada.

Pia pale pale wakamwambia ana nafasi kubwa ya kulipiwa chuo na serikali ya Canada kama akienda chuo kikuu cha Canada.

Watu wengi hawajui hili na huja kushtuka baadaye sana. Wanafikiri Watanzania muda wote lakini si Watanzania.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Watu washaweka vifungu vya sheria, hoja zijengwe kwenye vifungu hivyo sasa na siyo kile unachoelewa. Una uhakika gani na usahihi wa kile unachokielewa? Leta vifungu.

Kama ninachoelewa hakijakosana na kifungu cha sheria, na mie nilichokiweka ni kifungu kile kile cha sheria, kwa maneno yangu.

Msome EMT kaweka kile kile nilichokisema kwa kutumia vifungu vya sheria.

Kama una kifungu kingine kinachopingana na hiki cha kusema mtu aliyezaliwa nje kwa wazazi wa Kitanzania inabidi a declare kutaka uraia wa Tanzania kiweke hapa.

Watu wameweka kifungu cha sheria na kukiblast vile vile. the law is an ass if you ask me so do not even come here and try to act like sheria ni lazima u quote verbatim, kwa sababu hata wanasheria wanaweza kuijadili sheria katika contexts za "spirit of the law" na "letter of the law".
 
Watanzania wanga wana vyeti vya kuzaliwa.....?

Ukikosa cheti cha kuzaliwa ni kosa la nani? Umepanda basi, hata kama umelipa nauli, huna tiketi, utatuonyeshaje kwamba umelipa tiketi? Kondakta akija kukudai nauli utamuonyeshaje kwamba umelipa? Akikudai ulipe nauli mara ya pili kosa ni la nani?

Usitake kuhalalisha mediocrity kwa kutoa mfano wa mediocres.

Watanzania wengi kukosa vyeti vya kuzaliwa hakuhalalishi Mtanzania yeyote kukosa cheti cha kuzaliwa.
 
Kuna rafiki yangu mmoja alizaliwa Canada wakati wazazi wake wakiwa Chuo Kikuu. Wazazi wakamaliza Chuo, wakarudi Tanzania mshkaji akiwa mdogo sana. Kasoma shule ya msingi mpaka Form six bongo.

Baada ya kumaliza form six, akaanza mipango ya kutafuta vyuo Marekani ili aende kusoma chuo kikuu. Akaenda uhamiaji kuchukua passport, wakamuomba cheti cha kuzaliwa. Akatoa cha Canada. Wakamwambia ulivyofikisha miaka 18 ulikataa uraia wako wa Canada? Jamaa akashangaa, uraia wangu gani wa Canada? Mie baba na mama yangu Watanzania. Akaambiwa wewe raia wa Canada kwa hiyo kaombe passport ubalozi wa Canada. Jamaa kaenda ubalozi wa Canada, kawapa birth cerificate, wakaihakiki, wakampa passport ya Canada.

Pia pale pale wakamwambia ana nafasi kubwa ya kulipiwa chuo na serikali ya Canada kama akienda chuo kikuu cha Canada.

Watu wengi hawajui hili na huja kushtuka baadaye sana. Wanafikiri Watanzania muda wote lakini si Watanzania.

Kiranga,
Mfano wako ni tofauti na hii case ya Sioi.

Ili iwe hivyo, nchi uliyozaliwa lazima iwe na uraia wa kuzaliwa. Yaani mtoto yeyote aliyezaliwa ndani ya mipaka ya nchi hiyo anakuwa raia. Hii ni kama ilivyo Canada na USA ingawaje sina uhakika kama hiyo sheria inaendelea. Kwa UK ilikuwa mpaka 1983. Baada ya hapo ilifutwa.

Tanzania kama ilivyo Kenya hatuna uraia wa namna hiyo kutokea Uhuru. Uraia wa Tanzania na Kenya pia ulikuwa unategemea wazazi. Sijui katiba hii mpya ya kenya kama wamebadili lakini huko nyuma sheria yao ilikuwa inafanana tu na Tanzania.

Hivyo japo Sioi alizaliwa Kenya lakini hakuwahi kuwa Mkenya. Ni sawa na mtoto anayezaliwa Tanzania na wazazi wawili ambao sio Watanzania, huyo hawi Mtanzania.

Sioi hakuna haja ya ku declare uraia wake alipofikisha miaka 18 kwasababu yeye hakuwahi kuwa Mkenya.
 
Mkuu mbona unapingana na sheria? Kama hakuwa Mkenya then, he is a stateless person. Kama kweli alizaliwa Kenya, kwa mijibu wa sheria alitakiwa ahalalishe uraia wake alipofikisha umri wa miaka 18 kwa kuonyesha kuwa anakusudia kuwa raia wa Tanzania. Wakati akiwa na umri chini ya miaka 18 he was merely "DEEMED" to be a Tanzanian citizen.

Kuhusu katiba mpya ya Kenya wamebadili mambo mengi sana. Kwanza wameruhusu dual nationality. Pia sheria ya mpya ya Uraia na Uhamiaji ya mwaka 2011, kwa kiasi kikubwa imeondoa matatizo ambayo Sioi amekumbana nayo. The new law now inaruhusu citizenship by descent kwa kusema in section 7 that "A person born outside Kenya shall be a citizen by birth if on the date of birth that person's mother or father was or is a citizen by birth."
 
Pasco said:
Feedback, japo sina chama na Chadema naikubali sana tuu, ila kwenye uchaguzi wa Arumeru, nasimama na Sioi na machalii wote wa AR wako nyuma yake!. Asipopitishwa na CC leo, ile kambi yote ya Sioi, watashiriki kampeni za CCM, ila kura Chadema!. Kiuhakika bila Sioi, CCM itaangukia pua!.Igunga RA ni muoga kama kunguru siku za mwisho alijitokeza kuokoa jahazi, Sioi asipopitishwa Mmeru No. 1 hatatia mguu Arumeru!, CCM ni kifo cha mende straight away!.

Sijui ni lini umefika Arusha Pasco, ila kwa taarifa yako tu hiyo analysis uliyotoa sio sahihi. Huyu mtoto wabgemwacha aomboleze msiba wa baba yake. He is very young, 2015, sio mbali.

FJM, liangalie hili;
Sioi ni kijana wa Lowassa
Pasco ni kijana wa Lowassa
Unategemea Pasco kuwa kinyume cha Sioi?
 
Back
Top Bottom