Hata mimi nimeishtukia, hii ni habari njema kwani hivi ni vita vya panzi!. Kiukweli tukubali tukatae, angesimama Sioi, Chadema ingekuwa na kazi ya ziada!. Akipitishwa mwingine yoyote ni ushindi wa kiulani kama kumsukuma mlevi!.Fitina ni kawaida ya CCM, Huyu yupo karibu na EL wakati huo huo kiukweli Lowassa hatakiwi na fungu fulani ndani ya CCM, kwa kifupi ngoma inayotaka kuchezwa hapa ni ile ile type ya Bashe-Nzega
Jamaa kazaliwa Kenya na inasemekana hakuwahi kuukana uraia wake mpaka leo.. This was a technical error kwa Sioi..
Habari za uhakika kutoka kwa wazito wa NEC ya CCM ni kuwa SIOI SUMARI atapigwa chini na mgombea aliyemfuata Bw. Sarakikya atateuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi wa Arumeru Mashariki.
Hata hivyo mpango huo umeendelea kuwa mgumu kufuatia mashambulizi mapya ya nguvu ambayo mgombea mwingine Elishilia Kaaya ameyaanza. Habari ni kuwa Elishilia amekwaza na jinsi mpango ulivosukwa wa kumzunguka kiasi kwamba watu aliokuwa nao karibu ndio walioshiriki kummaliza ili kumjengea mazingira mazuri SIOI. Hata hivyo SIOI SUMARI inaelezwa na NEC kuwa hana mvuto wa kisiasa kabisa ila kwa nguvu ya koo na washili ana nafasi kubwa ya kushinda kwenye kunyang'anyiro.
NEC imejiridhisha kuwa Sarakikya ana uwezo na mvuto wa kisiasa kuweza kupeperusha bendera ya ccm dhidi ya mgombea wa CHADEMA.
Hata mimi nimeishtukia, hii ni habari njema kwani hivi ni vita vya panzi!. Kiukweli tukubali tukatae, angesimama Sioi, Chadema ingekuwa na kazi ya ziada!. Akipitishwa mwingine yoyote ni ushindi wa kiulani kama kumsukuma mlevi!.