Uraia Pacha Tanzania: Siasa ya Bernard Membe na hatma yake

The problem ya hii issue ni ufinyu wa knowledge kwa ccm hasa kikwete na kundi lake juu ya benefits za dual citizenship. The truth is more true wealth Tanzanians live abroad na facts zipo. Fact moja wapo ni kwamba most of Tanzanians abroad work really hard and save their money for future/retirement investments.

Why Tanzanians abroad support dual citizenship ni sababu moja kubwa wanaweza kuja Tanzania na ku-invest na kurudi wanapoishi ili kuendelea na maisha huko. Hii ni benefit kubwa kwa nchi na kwa sisi economist tunaita low cost stimulus kwa ajili ya uchumi wa nchi na politically itasaidia hata chama kilichopo madarakani, lakini jk anaonekana kutojua hili. The truth ni kwamba Watanzania wengi walio na massive cash in foreign banks hawataki tu kurudi Tanzania na kufungua biashara kubwa kama banks au ku-invest viwanda bila ya kuwa na legal/power to protect them, hii inamaanisha ukiwa na uraia wa US mfano na ukarudi Tanzania kufanya biashara ni kwamba huna power kama ukiwa na both citizenships. Serikali ya Tanzania itaendelea kudharau umuhimu wa kuwa na dual citizenship mpaka hapo watakapofunguka macho na kuona losses zilizotokea kwa muda mrefu, blind can really see...?

Hili swala tunalolifuatilia zaidi tunaona kikwete na membe wanacheza nalo kwa sababu tu wanataka kuwakomesha Watanzania wengi walio nje ya nchi mbao kiukweli wana knowledge ya politics na wameelimika na kamwe hawata vote ccm na this is true and facts about the issue I don't think anything else. Kwa kifupi taifa litaendelea kuchukua hii loss kwa muda mrefu ujao. The other facts here tusisahahu jinsi gani millions Watanzania walio nje ya inchi wanatuma kwa ndugu zao Tanzania kwa ajili ya matumizi ya elimu, afya, vyakula, kilimo na huduma zingine inchini (from US alone estimate $50,000,000 = TZ shil. 80 trillion yearly), bado hujagusa UK. Hii ndio free stimulus kwa serikali ya Tanzania na sio mkopo wala negotiations za deals. Haya ccm hawayaoni ila ni ku-block for political benefits.

Taifa litaendelea ku-lose talents, investments, best skills, leaders, technologies and many more solutions

ccm keep up na itikadi zenu tunajua jinsi gani Taifa lina suffer. Who will rather be Tanzanian national in this kind of circumstances?
 
Haiki upo hapo. haya ndiyo majadiliano ninayotaka yaani intelligent discussion with facts and data. Mimi kama kweli una sababu substantiable ningependa kujifunza kutoka kwako mimi nafili niweze ametufundisha zaidi.
 
Mimi ni Mtanzania ambaye nitachukua passport ya Marekani mwaka huu. Naomba ufahamu yafuatayo ndugu yangu

1. Hakuna kipengele Chochote kwenye application ya passport ya hapa inayosema unatakiwa kukana uraia wa nchi yako. Nimefanya application sijaona sehemu hiyo. Hii ni kwasababu Marekani wanaruhusu watu kuwa na uraia wa nchi mbili.
2. Uenyeji: Huku marekani watu wengi wamekuja kutafuta maisha kwenye kazi masomo na mambo mengineyo mengi.

Uraia unasaidia mambo yafuatayo
a) Huna sababu ya kuomba vibali vya kusafiria hasa kwenye kazi- Wamerakani wengi hawahitaji vibali vya kusafiria kwenye kwenye nchi nyingi za nje hivyo inapunguza usumbufu na gharama kubwa za visa hasa kama kampuni yako inahitaji wewe usafiri.
b) Vilevile unaweza ku vote
c) Kuna kazi ambazo zinahitaji raia tu hasa kwenye IT au research kama Nasa, Petagon n.k. Kuna kitu kinaitwa Goverment Clearance ambayo ni ngumu kupata kama huna uraia.
d) Sheria- Kuna sheria nyingi za immigration zinabadilika hivyo watu wengi wanapenda kutoa pressure ya kuishi kwa woga woga hasa kama wana familia mfano ukipata kesi hata kama ndogo lakini huna uraia unaweza kuwa deported/kurudishwa nyumbani bila kujali ukubwa wa kesi au familia yako.
e) Ukiwa na Uraia unaweza kuwaleta wazazi wako huku kwenye vitu kama matibabu n.k bila kuingia gharama za internation. Healthcare ya Tanzania kwa mfano ni ya chini sana hivyo ki afya unaweza kuwaleta wazazi wakapata matibabu au screening za afya kwa bei nafuu sana
f) Biashara- Kuna mikopo inayohitaji uwe raia kama small Business administration loans.

Umuhimu wa uraia wa Tanzania:
Tanzania kwasababu ndiyo ulikotokea hakuna mtu anayependa kupoteza uraia kwasababu ya familia mfano watu wengi wangependa kwenda kuzikwa na ndugu zao, mirathi pia iko nyumbani Tanzania. Ndugu wengi pia wako nyumbani Tanzania hivyo watu wakienda kusalimia ndugu hawataki kupewa siku na serikali za kukaa nchini au serikali kukuambia huna haki ya kumiliki ardhi hata kama ni ya baba yako. Nchi nyingi wanaelewa hili na ndiyo maana kuna Dual Citizenship kama isingekuwa muhimu USA, Canada, UK, Nigeria, India, China, Brazil, Mexico, n.k wasingeruhusu!!

Uoga wa Tanzania:
Tanzania inasema inaogopa hawa watu wanaweza kukimbia nchi!!?

Je hii inafada gani kwa Mtanzania wa Kawaida? Kama wewe ni Mtanzania na unaishi Tanzania basi Mtanzania mwingine kuchukua uraia wa nchi nyingine hutabadilisha maisha yako hivyo hili siyo swali la msingi. Lakini kama wewe ni Mtanzania mwenye uraia wa nchi unayoishi basi itakusaidia hivyo wanaosema itamsaidia vipi Mtanzania wa kawaida huu si msaada bali ni haki tu ambazo huyu Mtanzania anazipata kwasasa! na hataki kuzipoteza kwasababu hizo hapo juu!

Je hawa watakuja kuchukua ardhi yetu! Hawa watu wanaomba uraia wa nchi mbili ni wa Tanzania kwa sasa na kama wanataka kuchua kitu basi wangeweza kuchukuwa kabla ya kuchukua uraia wa nchi nyingine hivyo hili nalo si la msingi!

Wataiba pesa ka kukimbia nje? Kwanza hili siyo la kweli kwani uraia wa nchi mbili hauzuii mtu kukimbia! au kuiba pesa. Ukweli vilevile Watanzania walioko nje wanapeleka nyumbani pesa nyingi kuliko pesa inayotoka nyumbani kwenda nje hivyo kama ni uizi badi ni kwa nchi wanazoishi na sio Tanzania.

Tatizo lingine Watanzania wanaona kama kunakitu cha kuiba Tanzania je ni nini cha kuiba hapo! Kama kuna vitu vingi vya kuiba je ni kwanini Watanzania wanapigania ubalozini kwenda nje kwenye vyuo na kutafuta maisha? Je kama una ndugu nje kwasasa ni Mfisadi? amawahi kukuomba hata pesa? Tanzania imemsadia nini kumlipia chuo? Tuacheni kuwachukia Watanzania wenzetu walio nje hawa si wafisadi ni vijana wanaotafuta maisha kama wengine.
 
Naomba niongezee lingine hapa

Masilahi binafsi au ya umma

Maslahi binafsi ya mtanzania mara nyingi ndiyo maslahi ya umma Mfano. Mimi nikifanya kazi hapa nitatuma pesa kumsaidia mtoto wa kaka au dada kwenda shule ni maslahi ya binafsi na ni maslahi ya uma. Mimi nikituma pesa za matibabu kwa mzazi wangu Tanzania ni maslahi binafsi na maslahi ya uma. Mimi nikituna pesa ya kujenga nyumba ni maslahi binafsi na maslahi ya uma. Mimi nikija Tanzania kutembea na kutumia pesa ni maslahi binafsi na maslahi ya uma. Mimi nikipata elimu kwa pesa yangu mwenyewe bila ufisadi au kuiba kwenye kampuni ni maslahi ya nchi na maslahi ya uma. Mimi nikipata mwanga kwasababu ya kuishi nje na kukuelimisha hapa ni maslahi ya binafsi na maslahi ya uma. Kuna mengi hivyo hoja ya kusema kwamba kunatofauti ya maslahi ni potofu na isiyoangalia mbali. Maendeleo ya watu binafsi ndiyo yayoleta maendeleo ya nchi.
 
Sioni faida yake zaidi ya hasara,

Kwa sababu hauendani na mabadiliko ya dunia. Nikikwambia kuna mtanzania ambaye ni raia wa UK alinyimwa visa ya kuja TZ utaamini? unadhani huyo atawekeza TZ?

Hebu legeza ubongo wako na ufanye tathmini ya kina kwa nini Wachina, Wahindi na Wanageria wametapakaa duniani kote mpaka wamefungua mabenki yao na TV station zao? Usihitimishe kwa majibu mepesi kama vile population yao.

Umepata kujiuliza why mathalani wahindi faida zao hawaziweki TZ?

Ondokana na mawazo ya kipindi cha vita baridi pamoja na psychological effects za ukoloni.

Uraia wa nchi mbili ni muhimu sana kwa taifa lolote linalotaka kuondokana na umaskini.

Hivi unajua Tanzania inapoteza kiasi gani kwa mwaka kwa sababu ya watu wake kubanwa na uraia wa nchi moja?
 
nyandaigobeko

Swala ni Membe kutaka GF wake awe huru Tanzania na California pia. Swala la waaekazaji wazawa ni janja tu wa waziri kupitia hapa kwa masilahi binafsi.
 
Last edited by a moderator:
Naomba niongezee lingine hapa

Masilahi binafsi au ya umma

Maslahi binafsi ya mtanzania mara nyingi ndiyo maslahi ya umma Mfano. Mimi nikifanya kazi hapa nitatuma pesa kumsaidia mtoto wa kaka au dada kwenda shule ni maslahi ya binafsi na ni maslahi ya uma. Mimi nikituma pesa za matibabu kwa mzazi wangu Tanzania ni maslahi binafsi na maslahi ya uma. Mimi nikituna pesa ya kujenga nyumba ni maslahi binafsi na maslahi ya uma. Mimi nikija Tanzania kutembea na kutumia pesa ni maslahi binafsi na maslahi ya uma. Mimi nikipata elimu kwa pesa yangu mwenyewe bila ufisadi au kuiba kwenye kampuni ni maslahi ya nchi na maslahi ya uma. Mimi nikipata mwanga kwasababu ya kuishi nje na kukuelimisha hapa ni maslahi ya binafsi na maslahi ya uma. Kuna mengi hivyo hoja ya kusema kwamba kunatofauti ya maslahi ni potofu na isiyoangalia mbali. Maendeleo ya watu binafsi ndiyo yayoleta maendeleo ya nchi.

Ila je mkuu una hitaji uraia wa nchi mbili kufanya yote uliyo orodhesha hapo juu? Hilo ndilo swali.
 
Membe na viongozi wengine wengi CCM wana maslahi binafsi kwenye hili swala la uraia wa nchi mbili. Watoto wao wengi wako nje na wengine ameshachukuwa uraia wa huko, e.g Membe - Canada. Hiki wanachosema kuhusu kuwawezesha kuwekeza nchini ni kiini macho. Kwani ni kitu gani kinawashinda kufanya hivyo kwa sasa? Ni vizuri hili swala lisiangaliwe kinadharia kwa sababu litachochea kwa kasi ya ajabu kuhamisha 'capital' na rasilimali nyingi. Kwa sasa Rostam yuko wapi? Na yule dalali wa Rada yuko wapi? Watu watahujumu uchumi kwa kiwango cha juu na kutuweka! Dont tell me interpool maana hata sasa wapo lakini dalali wa rada bado anapeta!

Hawa wanasiasa wamekuwa waongo sana, hivi kuna watanzania wangapi nje ya nchi? na kati yao ni wangapi wana uwezo wa kuwekeza kiasi kwamba ni lazima tubadili kanuni za uraia.

Binafsi ningependa hili jambo la uraia liwe-implemented baada ya kuweka misingi imara ndani ya nchi kwa ajili ya kuzuia capital-outflow na pia kudhibiti watuhumiwa wa makosa mbalimbali makubwa kukimbia. Sidhani chini ya uongozi tulionao kwa sasa tuko tayari lakini kama ikatokea (and I hope it will happen -soon) tukawa na uongozi imara wa nchi na wenye uthubutu wa kusimamia sheria basi uraia wa nchi mbili utakuwa wa manufaa. but not now. SORRY.
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Kwa sababu hauendani na mabadiliko ya dunia. Nikikwambia kuna mtanzania ambaye ni raia wa UK alinyimwa visa ya kuja TZ utaamini? unadhani huyo atawekeza TZ?

Hebu legeza ubongo wako na ufanye tathmini ya kina kwa nini Wachina, Wahindi na Wanageria wametapakaa duniani kote mpaka wamefungua mabenki yao na TV station zao? Usihitimishe kwa majibu mepesi kama vile population yao.

Umepata kujiuliza why mathalani wahindi faida zao hawaziweki TZ?

Ondokana na mawazo ya kipindi cha vita baridi pamoja na psychological effects za ukoloni.

Uraia wa nchi mbili ni muhimu sana kwa taifa lolote linalotaka kuondokana na umaskini.

Hivi unajua Tanzania inapoteza kiasi gani kwa mwaka kwa sababu ya watu wake kubanwa na uraia wa nchi moja?

Je ni lazima kuwa na uraia wa nchi mbili kufanya yote hayo kama kufungua mabenki na T.v. stations? Na huyo Muingereza aliyenyimwa visa ya Tanzania kwani watu wengine wasio na uraia wa Tanzania wana kujaje kuwekeza?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Nadhani bado hujataka kunielewa. Aliyenyimwa Visa ni Mtanzania aishiye Uingereza ambaye alipata uraia wa Uingereza.

Kaka ukiweza kupitia vema hoja zangu na kuyajibu maswali yangu kama great thinker utauona ukweli.

Tufike mahali tuweke nyuma porojo, hisia na majungu yasiyo namaana, ndio maana mwingine anahoji why Membe aseme. Kama wote akili zao bado ni mgando je? Wewe ulitaka aseme nani?

Jana Mmoja kasema Leticia Nyerere anainterest zake sababu ana watoto wanasoma. Jamani haya mawazo yanaiua Tanzania.

Mmoja leo kasema Membe anataka GF wake afaidike, Hebu tuache tarabu katika mambo muhimu.

KUBALINI CHANGES. Nadhani taarabu za jinsi hii zinafaa kule kwa wale jamaa ---------- PIA KAMPEN ZIKIANZA IGUNGA huko kidogo ni uwanja wake
 
Nadhani bado hujataka kunielewa. Aliyenyimwa Visa ni Mtanzania aishiye Uingereza ambaye alipata uraia wa Uingereza.

Kaka ukiweza kupitia vema hoja zangu na kuyajibu maswali yangu kama great thinker utauona ukweli.

Tufike mahali tuweke nyuma porojo, hisia na majungu yasiyo namaana, ndio maana mwingine anahoji why Membe aseme. Kama wote akili zao bado ni mgando je? Wewe ulitaka aseme nani?

Jana Mmoja kasema Leticia Nyerere anainterest zake sababu ana watoto wanasoma. Jamani haya mawazo yanaiua Tanzania.

Mmoja leo kasema Membe anataka GF wake afaidike, Hebu tuache tarabu katika mambo muhimu.

KUBALINI CHANGES. Nadhani taarabu za jinsi hii zinafaa kule kwa wale jamaa ---------- PIA KAMPEN ZIKIANZA IGUNGA huko kidogo ni uwanja wake
'

Mkuu ushasema tayari ana uraia wa Uingereza sasa anakuaje Mtanzania tena? Yeye si alichukua uraia wa Uingereza akijua fika kwamba ina maanisha kupoteza sifa za kuwa Mtanzania? Kwa hiyo natumai alifanya cost benefit analysis na akaona kuna faida zaidi kwake kuwa raia wa Uingereza.

Lakini mkuu that first part is beyond the point. Hapa point ni faida au hasara za kuwa na dual citizenship kwa Tanzania. Ukaorodhesha vitu fulani na mimi nikasema mtu hahitaji uraia wa nchi mbili kufanya hivyo. Kwani mtu kama ni Mtanzania akaamua kuchukua uraia wa mfano Uingereza ni nini kitamfanya ashindwe kuwekeza Tanzania? Ni lazima kuwa na dual citizenshio kuwekeza Tanzania?

Hizo za Leticia Nyerere na Membe sijasema mimi kwa hiyo jibu hoja zangu kama mimi mkuu maana mawazo yangu si sawa na hayo ya hao ndugu yangu. Leticia Nyerere and Membe have nothing to do with me mkuu. Wewe umeorodhesha vitu unavyo ona ni faida ya kuw na dual citizenship. Nikauliza swali ya je hayo yote mtu hawezi kufanya bila kuwa na uraia wa nchi mbili. Bado hujanijibu.

Kuhusu changes mkuu mimi sija kataa wala kukubaliana na suala la dual citizenship. Nahoji nijue faida na hasara zake. Mpaka sasa sijaona kitu chochote kilicho orodheshwa kama faida ya dual citizenship ambavyo haviwezi kufanyika bila hiyo dual citizenship. Change haimaanishi kuiga sera za sehemu zingine bila kwanza kujua kwa nini tuna ziiga. So ukisha nijibu swali langu mkuu tutaendelea na hoja zaidi.

Asante kaka....
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Wakuu kama kuna mtu anafahamu baada ya maombi ya passport ya kimataifa, je huchukua muda gani kupata pass hiyo?
 
Nikiongezea tu pia ni kwamba watoto wengi wa vigogo wako nje ya nchi na wanauraia kwenye nchi hizo.

Kuwa na uraia Europe, US kunasaidia kupata benefits nyingi tofauti na mtu asiye raia (kama mchangiaji mwingine alivyosema). Sasa hawa hawa watoto wa vigogo (i believe na watanzania wengine wasio watoto wa vigogo) wanataka kuja nyumbani kupigania nafasi nyeti za uongozi, lakini hawawezi kufanya hivyo kama wana uraia wa nchi nyingine.

Kuwa na uraia wa nchi nyingine means your no longer raia wa TZ. Kuna mtu aliniambia kuwa sheria za uwekezaji pia ni tofauti (benefits/taxes zinazotakiwa kulipwa na wazawa ni tofauti na zinazotakiwa kulipwa na wageni kama haki ikizingatiwa (bila rushwa). Kenya wanaruhusu uraia zaidi ya mmoja, nafikiri ndio maana Wakenya walioko nje wanawekeza sana nyumbani.

Tujiulize pia kuna umuhimu gani waku-invest /waku-put all your effort kwenye nchi ambayo unajua legally wewe sio raia? Ukweli ni kwamba watu wengi wanatabia yaku-direct effort zao kuestablish uchumi wa nchi ambayo wanajua vizazi vyao vita-benefit from it.

Nilikuwa narafiki yangu alizaliwaga Canada lakini akiwa mdogo wazazi wake wakarudi bongo. Alipomaliza high school ali-apply chuo Canada na akaambatanisha cheti chake chakuzaliwa. Wao wakamu-accept kama raia na wakamshauri awe na current passport etc. Siku anaondoka TZ kwavile aliondokea na passport ya Canada uhamiaji ulimshikilia ukasema alikuwa anakaa nchini kinyume cha sheria.(I think alitakiwa aonyeshe documents fulani lakini yeye hakuwa nazo).

To make story short walimpiga fine then wakamuachilia. This and other stories itakuonyesha ni-kwa kiasi gani unaweza kusumbuliwa na system kama huelewi vizuri haya mambo ya uhamiaji. Lakini pia sijui kama Membe na wenzie wana-ajenda nyingine binafsi au vipi.

Nafahamu pia hawa viongozi wa matawi ya CCM nje ya nchi wengi wana-uraia kwenye hizo nchi; sasa wanataka kuja nyumbani kupigania nafasi kwenye chama lakini hawawezi wanakwamishwa na hii kitu.
 
Kunyima watu dual citizenship ni kujirudisha nyuma. Hao matajiri wenyewe kina Marekani na Uingereza wanajua umuhimu wa hiki kitu katika biashara ya kimataifa. Mara nyingine tunajifungia milango wenyewe halafu tunalaumu mvua hazinyeshi.

Wahindi kibao wamekuja kufanya kazi/ kusoma US, wameishi, wamechukua uraia, wameona India kuna maendeleo sasa yanayohitaji mchango wao, wamerudi kwao kuendeleza nchi. Wanaipeleka India katika mashindano ya kibiashara kwa benefit zote za raia wa Marekani.

Dual Citizenship ni kama vyama vingi vya siasa, ni trend ambayo utake usitake inakuja, sasa uamuzi ni wetu kama tunaamua kuikubali leo ili tupate a leg up on it's advantages au tuikubali miaka 50 ijayo wakati wenzetu hawaongelei dual citizenship tena, bali washachafua dunia wanataka kuikimbia waende kuhamia sayari nyingine.

Wakati sie tutakuwa tumebanana Kisarawe kwa kuwa hatutaki raia wawe na dual citizenship.

Hii habari ya kuwaminyia watu dual citizenship haina tofauti na ile habari ya kukataza watu kusafiri na kuwa na passport, baadaye tutakuja kuangalia nyuma na kusema "duh, hapa tuliboogie step sana" kama hatutaikubali.

Huwezi kuniambuia mei leo nije kuwekeza Tanzania kwa terms za foreigner eti kwa sababu nimechukua uraia wa Marekani. Na Marekani kuna mi ofshore investment siwezi kui explore kama naishi kwa green card.

Kwa hiyo hiyo dual citizenship ikija poa, isipokuja napo poa vile vile, tutakuja kwa visa tu au kuchukua permanent residency ya huko.
 
People with dual citizens enjoy many privileges, example of voting in both countries, owning property in both countries, and having government health care in both countries. These are just few exhibits.

To say the truth, dual citizenship is becoming more common in our increasingly interconnected, global economy. Many countries are now seeing the advantages of dual citizenship and are liberalizing their citizenship laws (India, the Phillippines, and Mexico are recent examples).

Dual citizenship has the advantages of broadening a country's economic base by promoting trade and investment between the dual citizen's two respective countries.

So, it is better for Tanzania to adopt and/or allow dual citizenship.
 
Mwanafastafa Je mimi nikichukua uraia wa USA na bongo nina kunyima au kukuzuia nini wewe kwenye maendeleo yako. Au je Mimi nitakuwa na hasara gani kwa jamii ya Tanzania?. Hivi mnavyosema hivyo je USA wangekuwa na mawazo kama hayo kungekuwa na Watanzania hapa kweli kwamba kila mtu akija huku ni kwasababu ya kutaka kuiba na sisi tunavyotuma pesa nyingi kutoka nchi hii ingekuwa Tanzania ingekuaje? Lakini ndiyo maana hii nchi ni tajiri. Watanzania bado tunafikiria kimasikini na kama msikokuwa makini tutaachwa sana na wenzetu kama wa Rwanda ambao wanawatumia sana ndugu zao walio nje
 
Back
Top Bottom