Uraia Pacha Tanzania: Siasa ya Bernard Membe na hatma yake

Ubumuntu

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,316
10,782
Salaam wanaJF!

Katika kipindi kirefu sana kumekuwa na mjadala juu ya kuruhusu uraia wa nchi mbili 'dual citizenship' katika taifa letu. Mjadala huu umepamba moto sana haswa katika uongozi wa waziri Bernard Membe. Hata katika hotuba ya bajeti ya wizara mwaka 2011/2012, ndugu Membe alizungumzia na kusisitizia suala hili. Kabla sijaenda mbele zaidi, naomba niulize, hivi ni sahihi kwa suala hili kujadiliwa na wizara inayoongozwa na ndugu Membe? Suala linaluhusu uraia kwanini lijadiliwe na wizara ya mambi ya nje, badala ya wizara ya mambo ya ndani?!

Naendelea na mjadala. Mimi binafsi kama raia wa Tanzania sijaweza kuelewa hoja zote zinazotolewa katika kujustify dual citizenship. Hususani juu ya suala la kuongeza kuongeza uwekezaji kutoka na wanaoitwa watanzania walio nje. Hapa pia kuna maswali ya kujiuliza. Hivi mtanzania anatambulikaje? Kwa passport? Kwa kadi ya kupigia kura? Au? Kama mtu (alie na miaka zaidi ya 18) hana vyote hivi anaweza kutambulika kama mtanzania? Je, mtu aliekua na passport ya Tanzania, halafu akaikana kwa kuchukua passport ya nchi nyingine, huyu ataendelea kutambulika kama mtanzania au?

Kama nia kuongeza uwekezaji, kwani hao watanzania walio nje wanakatazwa kuja kuwekeza? Tena hao wanakua na added advantage kwavile wanaifahamu nchi kuliko wawekezaji ambao hawana trace ya utanzania. Tena wakija kama wageni ndio watapokelewa vizuri zaidi kuliko wakija kama wazawa, kutokana na hali ya urasimu uliopo katika suala la uwekezaji wa wazawa. Katika hili, bado sijaona hoja nzito.

Pia kuna suala la rasilimali watu. Kwamba kuna watanzania walio nje ya nchi ambao wana elimu na utaalamu wa mambo mbalimbali ambao pengine ni adimu au ungeweza kuongeza nguvu kazi katika taifa letu. Sawa. Je, hawezi kuja kama expatriates? Mbona tunao wengi tu katika sekta mbalimbali, kuanzia taasisi za elimu, mashirika ya umma, idara za serikali na taasisi za serikali na binafsi. Sasa hapa hao watanzania walio nje wanashindwa nini mpaka wapewe uraia mwingine?! Tena wakija kama expatriates watapata employment benefits nzuri zaidi kuliko wazawa. Hapa pia sijaona hoja nzito ya kupelekea uwepo wa dual citizenship.


Sasa kama hizo ndio hoja za Membe, napatwa na wasiwasi kama dual citizenship ipo kwa maslahi ya umma au maslahi ya watu binafsi (nimesikia ndugu Membe ana watoto aliowazaa nje ya nchi!)

Huu ni mtazamo wangu, kukosoana kwa manufaa ya kuelimishana kunakaribishwa.

Asante.

----------------------

The right to dual citizenship in Tanzania is a must


Dual Citizenship is a status in which a person is concurently regarded as a citizen under the laws of more than one state. Dual citizens have two passports and live and travel freely within their native and naturalized contries without immigration constraints. The Tanzania citizenship is governed by the Citizenship Act, 1995. This Act proscribes the right to dual citizenship. S. 7(4) provides"Any Citizen of Tanzania shall cease to be a citizen if having attained the age of 18 years, he acquires the citizenshp of some country other than Tanzania by a voluntary act other than marriage".

The Tanzanian Constitution, 1977 unlike Constitutions of other countries eg Kenya and Uganda, is silent on the right to dual citizenship. Generally, citizenship in our Constitution is merely mentioned en passant.

A significant number of Tanzanians are now living abroad and are scattered all over the world. They are now commonly known as THE DIASPORA COMMUNITY. Mean estimate is putting the number of Tanzanians in Diaspora at 2Million. This group, thus, account for 5% of our total population. This is an important constituency which has to be represented in the new constitution, in my humble view.

There are many factors obtaining in Tanzania which have contributed to the exodus of skilled talent. They include poor conditions of service, potential human rights abuses, nepotism and favoratism, disregard for local talent, scarcirty of jobs, poor salaries, limited access to education, the 2001 Zanzibar chaos etc.

African natives who are resident in industrialized nations have been prodding their home countries to provide for dual citizenship to make it possible to make them citizens of a second country. A lot of Tanzanians who are currently in the Diaspora have been agitating for the same. At the beginning, the issue of citizenship was resented but now it was beginning to be understood.

Tanzania has been benefitting from people living abroad through remittances. Apart from tha,t Tanzanians living abroad have different professions and are experienced in several sectors of the economy, hence they would make immense contribution if they came back to work here. Some of them command respect the world over hence if properly utilized they could greatly contribute to their mother country development.

The role of the Tanzanian Diaspora community has been, inter aia, to provide socio-economic support for some Tanzanians back home. Due to the extended family system, most of Tanzanians living abroad find themselves being regarded as crucial breadwinners of not only their immediate families but also their close family relatives.

They normally pay for most of the financial needs of their dependants back at home such as medical and education fees, accomodations rentals and social events such as religious gatherings, funerals, birthday and wedding parties.

in 2006, the Law Reform Commission of TZ under the Chairmanship of Judge A. Bahati recommended introduction of Dual Citizenship. The Commission stated that the issue deserved " a possitive and foward- looking consideration and that it was high time Tanzania adopted dual citizenship because in a globalized world, the country could not develop without interraction with other nations". More importantly, many developing nations scuch as Ghana have made significant economic strides after allowing dual citizenship a few years ago.Furthermore, Hon. B. Member, Minister for Foreign Affairs, a distingushed Diplomat stated the following in the National Assembly when responding to a question from one Vicky Kamata (CCM)
"African countries have been benefitting from people living abroad through remittances. For the past year,
a total of USD 40 Billion entered Africa through remittances out of which Tanzania received USD 250M.
We are creating a good environment that will enable Tanzanians living abroad work in the country. We
recognize them and respect their contribution to the country economic development. In the newly launched
5 year develoment plan (2011-2015) the issue of Diaspora has been highlighted and given priority. This dual
citizenship issue will also be included in the Constitutional debate..."

Thus, in my view, Dual citizenship MUST be enshrined in our new Constitution.
Great Thinkers, hii imekaaje?
 
tukiruhusu uraia wa nchi mbili basi tumekwisha maana wanaolilia hili ndo wale wale tunaowapigia kelele kuwa wanatuibia.sasa wanataka pa kukimbilia wakishaiba vya kutosha.
 
Jaribu kujenga vizuri hoja yako kwa mwainisho wenye kueleweka, maana hapa bado sijakuelewa unachoongelea. Naomba jaribu kutoa mada kwa kutuliza kidogo........
 
tukiruhusu uraia wa nchi mbili basi tumekwisha maana wanaolilia hili ndo wale wale tunaowapigia kelele kuwa wanatuibia.sasa wanataka pa kukimbilia wakishaiba vya kutosha.

Waruhusu wasiruhusu wanaotaka kuiba kwa kutumia njia hiyo watakuepo tu! Na kunawatu wana ppt za nchi nyingi tu hapa tz (illegally) kwa mfano nasikia RA anauraia wa TZ na nchi nyingine (source Mtikila), akitaka kusafiri huko..anatoka bongo na ppt ya Tanzania anashuka Nairobi, Nairobi anatumia ppt ya nchi nyingine (sijui Iran!!) anaenda!! Kwahiyo hoja hainamaana sana!!!

Watanzania wengi waliochukua urai za nchi nyengine ni kwajili ya maslai ya kiuchumi zaidi kwenye nchi walizofikia (which is a valid reason)....same applies to wahindi waliochukulia urai wa Tanzania (Ili waweze kumiliki ardhi etc)....

In-short kama mtu anahulka ya wizi ataiba tu haijalishi ana uraia wa nchi moja au mbili au hata tatu!!
 
Rasimu ya uraia wa nchi mbili wanaopinga ni wale wenye mtazamo hasi badala ya mtazamo chanya. Angalia mataifa yaliyopiga hatua za kimaendelea katika bara la Asia na Amerika kusini, halikadhalika baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ni kutokana na kuruhusu mfumo huo ambao hufanya raia wachume nje na kuwekeza kwao ili kukuza uchumi wa nchi.

Tunafurahia makampuni mengi ya kigeni kama ya simu za mobile nk. hao wanawekeza bongo na kuchukua faida kuirudisha kwao. Wewe huoni hasara hiyo unayoliwa na wawekezaji ila unachofikiria nafasi kama hiyo watanzania wasiipate?

Watanzania tuache tabia zenye mweleko wa wivu tufikirie zaidi ya manufaa ya uchumi kitaifa si mtu binafsi.
 
Rasimu ya uraia wa nchi mbili wanaopinga ni wale wenye mtazamo hasi badala ya mtazamo chanya. Angalia mataifa yaliyopiga hatua za kimaendelea katika bara la Asia na Amerika kusini, halikadhalika baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ni kutokana na kuruhusu mfumo huo ambao hufanya raia wachume nje na kuwekeza kwao ili kukuza uchumi wa nchi.

Tunafurahia makampuni mengi ya kigeni kama ya simu za mobile nk. hao wanawekeza bongo na kuchukua faida kuirudisha kwao. Wewe huoni hasara hiyo unayoliwa na wawekezaji ila unachofikiria nafasi kama hiyo watanzania wasiipate? Watanzania tuache tabia zenye mweleko wa wivu tufikirie zaidi ya manufaa ya uchumi kitaifa si mtu binafsi.

Binafsi bado napinga uraia wa nchi mbili na ninazo sababu muhimu. Uraia wa nchi mbili pekee hauwezi kutuletea maendeleo kama bado Watanzania hatujajifunza uwajibikaji. Hizo nchi za Asia unazozisema hawana mchezo na maslahi ya nchi zao, watu wake hawana ubabaishaji kama tulionao wabongo. Ni watu ambao teyari walishapevuka kifikra kama nchi kabla hata ya kuleta mambo ya uraia wa nchi mbili.

Kunamambo mengi ya msingi yametushinda vitu kama umeme ambao ni muhimu (tunashindwa kuwa nao wa uhakika) sasa unafikiri kukubali uraia wa nchi mbili pekee ndo utaleta maendeleo?

Ni kweli uraia wa nchi mbili unafaida zake lakini kwasasa bado hatuuitaji kwakuwa mfumo mzima wa uwajibikaji Tanzania hauridhishi. Mfumo wetu ni mbovu sana na kama tutaingia kichwa kichwa tutakuja kuumia sana. Kuna mambo mengi tuliyo ingia kichwa kichwa mfano uchimbaji wa madini ambayo wengi walisema yanafaida lakini hizo faida zake hatuzioni.

Tanzania tunahitaji kufanya mambo muhimu kwanza kama kuuondo ufisadi, ubabaishaji (ujanja ujanja) na kurudisha uwajibikaji. Tukisha fanya hayo ndiyo tufikirie mambo ya uraia wa nchi mbili.
 
Jamani jamani jamani, Watanzania tuko zaidi ya millioni 40 ambao karibu wote ni masikini, ni wachache tu wenye uhitaji/uwezo wa kuwa na uraia wa nchi mbili. Hawa wachache wenye uraia wa nchi mbili kimagendo (kwa sasa sheria hairuhusu) makusudi yao ya kuwa na uraia wa nchi mbili ni maendeleo ya kibinafsi zaidi kuliko maendeleo ya Watanzania walio wengi.

Watanzania walio na uraia wa nchi mbili wengi wanaogopa kurudi kuishi nyumbani kwa sababu ya hali yetu ya uduni wa maisha, e.g miundo mbinu ya maji, barabara, umeme, matibabu n.k. Hata kama ni kuwekeza hawa ndugu wanaona kuwekeza nyumbani hakulipi kwa sababu ya matatizo yaliyotajwa. Wenzetu wazungu wao mazingira ya kwao ni magumu kuwekeza lakini ni mazingira mazuri ya kuishi kwa menye fedha, wao wanaona kwetu huku ni rahisi kuwekeza (kwa kutuibia) ili wapate fedha za kupeleka kwao kutumia.

Mimi ninamshauri bwana Bernad Membe asisumbuke na kupeleka malumbano bungeni ya uraia wa nchi mbili wakati bado tuna matatizo kibao ya elimu, miundo mbinu, magonjwa, na upungufu wa kuwajibika. Bwana Bernad wacha kupeleka hoja bungeni uliyotumwa na watu wachache, tengeneza mazingira yatakayowafanya watanzania wanaochuma nje warudi kutumia nyumbani, tengeneza utaifa wa kila Mtanzania kujivunia.
 
Mnaopinga uraia wa nchi mbili sababu kuu ni kuogopa mafisadi wataiba na kutoroka? mbona washaiba sana hata bila dual citizenship?

Kipi bora, watanzania waliopo abroad wachukue uraia wa nchi walizopo na kupoteza uraia wa tanzania (kunufaisha nchi walizopo) au kuwepo na sheria ya kuwawezesha kuwa na uraia wa nchi na kunufaisha nchi zote mbili?

Binafsi siwezi kuchukua uraia wa nchi yoyote ile na kupoteza utanzania wangu no matter what. Tutabanana hapa hapa kwa JK na shida zetu (umeme, maji, security, afya etc) hadi kieleweke.
 
BABA JUICE

Hivi mkuu nadhani haujui dunia inapoolekea, wewe unafikiri EU, UAE na EA community ni zipo kwa sababu gani? free movement of capital goods na human capital. sasa kuna watanzania milioni 3 ambao wanaishi nje ya nchi kwa sio maslahi yao tu bali na familia zao, na hao watanzania wengine wanawatoto na wake au waume wenye uraia wa nchi hizo walizokuwepo, nchi kama Mexico, India au China zimeendelea kwa sababu ya wananchi wao ambao wanaishi nje ya nchi, wanasajili mpaka vitukuu vya raia wao waliopo nchi za nje, na ndio hao hao wanaopeleka maendeleo kwao through technological, social and financial transfers.

Acheni siasa za kizamani kwamba watu wakiwa na raia mbili watahujumu uchumi.
 
Last edited by a moderator:
BABA JUICE

Mie nafikiri utoe factor za kupinga huo uraia na sio kupinga hewani. Unasema kuiba na kukimbia kwa RA,JK,Mbowe,Lowasa wameshakimbia?
 
Last edited by a moderator:
Binafsi bado napinga uraia wa nchi mbili na ninazo sababu muhimu. Uraia wa nchi mbili pekee hauwezi kutuletea maendeleo kama bado Watanzania hatujajifunza uwajibikaji. Hizo nchi za Asia unazozisema hawana mchezo na maslahi ya nchi zao, watu wake hawana ubabaishaji kama tulionao wabongo. Ni watu ambao teyari walishapevuka kifikra kama nchi kabla hata ya kuleta mambo ya uraia wa nchi mbili.

Kunamambo mengi ya msingi yametushinda vitu kama umeme ambao ni muhimu (tunashindwa kuwa nao wa uhakika) sasa unafikiri kukubali uraia wa nchi mbili pekee ndo utaleta maendeleo?

Ni kweli uraia wa nchi mbili unafaida zake lakini kwasasa bado hatuuitaji kwakuwa mfumo mzima wa uwajibikaji Tanzania hauridhishi. Mfumo wetu ni mbovu sana na kama tutaingia kichwa kichwa tutakuja kuumia sana. Kuna mambo mengi tuliyo ingia kichwa kichwa mfano uchimbaji wa madini ambayo wengi walisema yanafaida lakini hizo faida zake hatuzioni.

Tanzania tunahitaji kufanya mambo muhimu kwanza kama kuuondo ufisadi, ubabaishaji (ujanja ujanja) na kurudisha uwajibikaji. Tukisha fanya hayo ndiyo tufikirie mambo ya uraia wa nchi mbili.

Wababaishaji ni hao wabogo walio na uraia wa nchi moja walio bongo.Na ndio maana tunasema tuwaruhusu wezetu waliojifunza waje wahamasishe kutokuwa wababishaji.
 
Mzee wa Kaya

Maendeleo ya Taifa yanaanza na maendeleo binafsi. Harafu unaongea bila kushirikisha vizuri mfumo wako binafsi, unaongea wabongo walio na raia wa nchi mbili wanaogopa kurudi, kana kwamba tayari kuna uraia huo, ama unashindwa kuambatanisha vizuri kwamba mbongo aliyechukua uraia si raia tena wa tz, na akirudi bongo anakuja kama mwingireza lazima aombe viza na kwa nini na kwa nini na kwa nini. Kifupi sikuelewi.
 
Last edited by a moderator:
Bongo haendelei kwa sababu za choyo, chuki binafsi, ufitini, umimi na mambo ya namna hiyo.

Karne hii mtu anaongea kama yuko old stone age, eti ufanye uharifu ukimbie kwa sababu ya uraia wa nchi mbili, thubutuuuuuu. B
 
Mh Membe alitoa ufafanuzi Huu mjadala ulishajadiliwa tusubiri Bunge au tuwaambie wabunge wetu hoja zetu
 
Membe akaze buti ili watanzania walio na uraia wa nje warudi kuwekeza bongo. Unajua tena home is the best. Kuna wengine wana hata watoto lakini watoto hawana uraia wa Tanzania na wanakuja Tz kwa visa. Acheni mambo ya kizamani nafikiri TZ itanufaika zaidi kwa kuruhusu uraia wa nchi mbili.
 
watu naona hamuelewi tunakoelekea, nafikiri baadhi ya nchi za africa na UCHINA wanajua tunapoelekea na siyo kila sehemu inabidi tutumie nguvu ya hoja ya mmoja mmoja.

Ngoja nianze na hili MIMI binafsi na pinga kuwa na uraia wa nchi mbili japokuwa niko nje yanchi. Kuwa na uraia wa nchi mbili hakuna maana na wala hakuna faida unayoiita maendeleo ya uchumi, ngoja nikupe mfano nchi ya uchina uolewe au uoe hakutabadilisha uraia wako kuwa mchina na hakuna mtu kupewa uraia wachina hiyo ni mwiko, lakini tunaona inaendelea kiuchumi nahao wenye uraia wa nchi mbili wako nyumaa kwa uchina. Kwanini usiende kuomba work permit naufanye kazi kisha urudishe ujuzi na neema nyumbani? shida ndiyo zikufanye ukane nchi yako?

Kitukingine naona hata kutoa urahia kwa mtu ambaye siyo mtanzania nikosa kubwa sana, natukija kushtuka yanayotokea libya kwa mtutu wa bunduki hapa kwetu hao tunaowapa uraia eti wamekaa kwamuda mrefu tutakuja kujuta. unakuta mmarekani kisa kakaa miaka fulani tanzania basi aombe na apewe uraia kisha agombee uraisi awe raisi wa tanzania then mtasema mko safe dhidi ya nchi za magharibi? Jifunzeni mambo mengi kutoka nchi zinazo endelea kutokana na ujuzi na juhudi zao ndani ya nchi kuliko kutegemea kwenda kufanya kazi nje kuendeleza nchi yako .

TUWENI WABUNIFU TUJIFUZE KUTOKA KWAWATU TUSIMAMISHE KUTOA URAIA TUFUTE FIKIRA ZA URAIA WA NCHI MBILI TUFANYE KAZI KWABIDII TUTAFIKA MBALI. NINAFUU KUWAPA WATU WORK PERMIT YA MUDA MREFU 10YRS -20TRS LAKINI KIUKWELI SIYO RAIA WA TANZANIA.
 
DOCTORMO

Hoja yako haileweki.

Saizi watanzania mko safe kwa sababu rais ana uraia wa nchi moja? wewe unaonyesha malengo yako na mitazamo yako ni ktk kuajiliwa na huu ndo mtizamo butu wa sisi watanzania wengi, unaotakiwa kurekebishwa.

Lazima utambue sahizi tuko ktk soko la ushindani soko huria na kwa bahati mbaya feather wieght(TZ) na heavy weight(weasten countries) mmewekwa ktk ulingo mmoja mzichape, japo ktk hali ya kawaida mabondia hawa hawaruhusiwi kuzichapa.

Uchumi hauwezi kusonga mbele kama hakuna nguvu ya kuingiza fedha yani watu wengine kununua kutoka kwenu. Na ni lazima muwafuate huko kwao muwauzie bidhaa yenu. Ndivyo china walivyo wanawafuata huko, kama hujui, serikali ya china inawapa watu/makapuni fedha ya kutosha kwenda kushindana huko nje. NK
 
Bongo haendelei kwa sababu za choyo, chuki binafsi, ufitini, umimi na mambo ya namna hiyo.

Karne hii mtu anaongea kama yuko old stone age, eti ufanye uharifu ukimbie kwa sababu ya uraia wa nchi mbili, thubutuuuuuu. B

Mpaka leo watu wana mawazo ya mgando wakati ulimwengu mzima unahaha kuunganishwa kuwa global village. Tuna Jumuiya ya Afrika Mashariki na sasa tutakataa kuruhusu uhuru wa kupenya kila nchi mpaka mtu awe na visa eti watakimbiza mali za kifisadi? Mawazo finyu mno. Tunawaza kuwa na pesa moja wakati huo huo tunaendelea kuwa na mawazo ya mgando (isolated) tutafika?
Kama nchi za ulaya zingekuwa na fikra hizo sidhani kama wangefikiwa kiwango cha umoja walio nao sasa.

Kuruhusu uraia wa nchi mbili una manufaa zaidi kiuchumi kwa taifa letu kuliko wanavyofikiria wengine kuhusu uchumi binafsi. Pesa za kigeni wanazoingiza nchini pamoja na njia nyingine za uwekezaji zinasaidia si kuinua uchumi tu wa nchi ila kupunguza pengo kubwa la umaskini kwa kiwango cha mfumo wa uchumi wa kimataifa. Utashangaa baada ya miaka michache tu kama mfumo huo utaruhusiwa utakuta Tanzania inapaa kiuchumi na kuongokana na umaskini.

Mataifa yaliyoendelea katika nchi za magharibi ni kutokana na mwingiliano wa watu, free market, na ndio unaona taifa kama marekani idara ya uhamiaji imelinua sana taifa hilo kiuchumi, kisiasa na kijeshi kwa sababu raia wako huru kushi nchi ye yote wakiwa na itikadi za taifa lao.

Angalia makampuni makubwa na wafanya biashara wengi tulio nao Tanzania ni Asian, na hao wana uraia wa nchini kwao na hapa. Tungekataa kuwapa urai kwa vile wana uraia wa nchi nyingine maana yake tungedhoofisha uchumi wa nchi kwa vile wafanyabiashara hao licha ya kuteka pesa toka Tanzania na kupeleka kwao vile vile nchi yetu inanufaika na uwepo wao kibiashara na kiuchumi.
Watanzania tusiwe nyuma kila mara, na sasa tusema basi turuhusu kwa uchumi wa nchi kukua na kutengamaa unategemea mengi hili la uraia wa nchi mbili ukiwa mmojawapo. Kale kawivu tuweke kando kwa kufikiria faida ya mtu binafsi ila nini nchi inapata advantage.
 
Binafsi bado napinga uraia wa nchi mbili na ninazo sababu muhimu. Uraia wa nchi mbili pekee hauwezi kutuletea maendeleo kama bado Watanzania hatujajifunza uwajibikaji. Hizo nchi za Asia unazozisema hawana mchezo na maslahi ya nchi zao, watu wake hawana ubabaishaji kama tulionao wabongo. Ni watu ambao teyari walishapevuka kifikra kama nchi kabla hata ya kuleta mambo ya uraia wa nchi mbili.

Kunamambo mengi ya msingi yametushinda vitu kama umeme ambao ni muhimu (tunashindwa kuwa nao wa uhakika) sasa unafikiri kukubali uraia wa nchi mbili pekee ndo utaleta maendeleo?

Ni kweli uraia wa nchi mbili unafaida zake lakini kwasasa bado hatuuitaji kwakuwa mfumo mzima wa uwajibikaji Tanzania hauridhishi. Mfumo wetu ni mbovu sana na kama tutaingia kichwa kichwa tutakuja kuumia sana. Kuna mambo mengi tuliyo ingia kichwa kichwa mfano uchimbaji wa madini ambayo wengi walisema yanafaida lakini hizo faida zake hatuzioni.

Tanzania tunahitaji kufanya mambo muhimu kwanza kama kuuondo ufisadi, ubabaishaji (ujanja ujanja) na kurudisha uwajibikaji. Tukisha fanya hayo ndiyo tufikirie mambo ya uraia wa nchi mbili.

Brother leo umeamua kuutangazia umma umbumbumbu wako kuhusu hii concept na wewe na baadhi yenu mna fikra kwamba hali hii tuliyonaoyo ndiyo itatusaidia. Wale wanaofanya ufisadi kwa nchii wote wana uraia na passport za nchi hii, na ndiyo wanaotorosha utajiri wa nchi hii kupeleka huko nje. Wengine tayari wana uraia wa nchi nyingine na huko wanatambuliwa kama raia.

Sheria hii inawalenga watanzania ambao walitoka hapa kwenda kuhemea nje na wakakuta mazingira yaliyowalazimisha kuukana uraia wa Tanzania ili wapate manufaa ambayo wasingeyapata kama wasingechukua uraia wa nchi hiyo. Hawa sasa wako comfortable na wanatama kurudi kuwekeza lakini wakija huku wanaonekana ni wageni na wanabanwa na masharti yanayowabana wageni wote. Vile vile wanabanwa na masharti ya nchi walikochukua uraia. Hawa wana nia ya kufanya remittance hapa nchini lakini bila kuwa na hadhi hii remittances zao zimekuwa ni za kinyemela na zisizotosha.

Sasa unaposema kwamba kuna vipaumbele kama kupambana na ufisadi, kwani hili litazuiaje mapambano hayo ya ufisadi kama dhamira ya kufanya hivyo ipo. Yote yanaweza kwenda na wanaopinga hilo ni wale ambao hawana uelewa hii concept au ni wale wanaochukizwa na hoja hii kwa sababu ya chuki zao kwa aliyeitoa.

Kilicho wazi ni kwamba nchi nyingi hivi sasa zikiwemo zile tunazopakana nazo na washirika wetu wa kiuchumi wameona kwamba wazo hili ni muafaka na wale walioanza utekelezaji matunda yake yameweza kujitokeza. Hali hii itaweza kuondoa hata dhana iliyojengeka ya kubabaikia watu wanaojiita wawekezaji na mfukoni wana dola elfu hamsini au dola laki moja. Membe aendelee na mpango huu na kinachohitajika sasa kuwaelimisha wale wasiouelewa lakini wenye mapenzi mema kwa nchi hii na wanaotambua utendaji mwema wa watu kama Membe.
 
Uraia wa nchi mbili una manufaa kwa watanzania walio nje ya nchi kwani wanakosa fursa kama wakiamua kuchukua uraia wa nchi wanayoishi na kuwafanya waje tanzania kama wageni.

Uraia wa nchi mbili utawapa fursa ya kuwekeza hapa nyumbani na kuja bila kufuata mlolomgo wa kuomba visa kama wafanyavyo wageni.
 
Back
Top Bottom