Waungwana,
Kwanza nipige hodi kuingia kwenye ukumbi maana nilipotea kwa miezi kibao. Ni busara kuwasalimia wenye kijiwe kila urudipo toka safarini. Nimefurahi kusoma
hoja zenu na hii ni dalili nzuri kwamba wote mu wazima.
Nikija kwenye hii hoja hasa kuhusiana na Mwanakijiji. Anasema uraia wa nchi
mbili unafaidi kwa watu husika lakini hauna faida kwa taifa. Hapo ndipo tunapotofautiana sana.
Katika maendeleo yoyote hapa duniani yanakuja kutokana na juhudi ya mwanadamu kujiendeleza yeye mwenyewe na matokeo yake analeta maendeleo kwa yeye, familia yake na jamii yake nzima.
Kama uraia wa nchi mbili una faidi kwa kundi kubwa la Watanzania wanaoishi nji za nchi na hakuna madhara makubwa kwa taifa naona ni jambo zuri kulikubali hata kama halitabadilisha maishi ya watanzania milioni 30 wengine.
Ni sawa na shule, nchi inasomesha watu wachache kwa mamilioni na mara nyingi faida kubwa inaenda kwa wahusika ingawaje hata wengine wanafaidika indirectly.
Watanzania walioko nje kwasasa wanasaidia familia na jamii zao kwa njia mbalimbali kuanzia kusomesha, matibabu, maendeleo kwenye jamii nk. Kama hawa Watanzania wanaona neema yao hiyo itaongezeka kwa kuwa na uraia wa nchi mbili, naona ni jambo zuri kulitazama suala zima na kama hakutakuwa na matatizo mengine makubwa basi tuwakubalia.
Kitu cha msingi ni kwamba mpaka sasa Tanzania inaruhusu uraia wa nchi mbili kwenye baadhi ya makundi. Inaelekea hili wachangiaji wengi hawalijui. Kama wewe ni Mtanzania na umemuoa mgeni kwa mfano Mcanada na mkaamua kuishi Tanzania, baada ya muda mkeo anaweza kupata uraia wa TZ bila kuambiwa apoteze uraia wa nchi yake ya mwanzo. Naamini kuna mawaziri pia
wana wake zao ambao wana uraia wa nchi mbili. Sina uhakika lakini nadhani hata profesa Mwandosya ambaye alitaka kuwa rais ana mke kutoka Uganda. Huenda huyo mama bado ana magamba yake mawili na sheria inaruhusu hivyo. Lakini kama mwanamke kaolewa na mgeni na wamerudi kuishi TZ, basi huyo bwana hawezi kupata uraia wa TZ mpaka aukane uraia wa nchi alikotoka. Hapo kuna kaubauguzi ka aina fulani.
Pia kuna kundi la watoto, watoto mpaka miaka 18 wanaruhusiwa kuwa na uraia wa nchi mbili. Mfano mtoto akizaliwa UK kwa wazazi ambao wana permanent residence hapa basi moja kwa moja anakuwa na uraia wa UK hata kama wazazi wake wanakuwa sio raia. Wakati huo huo pia anakuwa raia wa TZ kutokana na wazazi wake kuwa Watanzania. Akifikisha miaka 18 inatakiwa aukane uraia wa UK ama sivyo anapoteza uraia wa TZ. Hapa pia ndio kwenye
kasheshe, baadhi ya hawa watoto wameishi miaka yote huku nje lakini pia wanataka kuendelea kuwa na uhusiano na nchi walikotoka wazazi wao. Ukiwaambia sio raia kwasababu una uraia wa nchi nyingine, tayari unawatupa
wananchi kwenye maelfu ambao huenda wangesaidia kuiendeleza nchi yetu huko mbele.
Hapa Europe kuna mifano mingi sana, kuna raia wengi wa nchi kama Italy na Poland waliondoka baada ya vita kuu ya pili kutokana na mambo ya kisiasa. Wengi walikuja UK na USA. Baada ya mabadiliko ya siasa ni watoto zao ndio
wanaongoza kupeleka vitega uchumi kwenye nchi walizotka wazazi wao.
Kwanini sisi tunataka tujifungie na kuwanyima kizazi chetu kijacho nafasi ya kushiriki kwenye maendeleo ya TZ?
Kama alivyosema Lowassa, wananchi wengi walioko nyumbani hawaelewi hili
jambo ni nini na ni moja kati ya masuala ambayo ukifuata wingi wa watu wanaopinga bila kuangalia matakwa ya kundi husika unaweza kujikuta unatunga sheria mbovu kwa maendeleo ya taifa.
Mtanzania.