Upweke

Habari za Jumapili ndugu zangu wapendwa, nimekuwa najiuliza hili swala,
kila mtu akiwa na upweke ana njia yake ya kuondoa upweke alionao
na mimi pia huwa nina njia zangu za kuondoa upweke nilio nao,lakini kwa
sasa nahisi nafeli, tangu juzi najiona mpweke sana,huwa wa kwanza kuwashauri
marafiki zangu wanapopatwa na hali hii, lakini inaonekana kwangu nimeshindwa
embu marafiki zangu niambieni ni njia gani rahisi ya kuondoa upweke na
kuwa na furaha kama siku nyingine???

Pole..Huwa inatokea. Hata mimi leo siku nzima nimekuwa mpweke sana. Halafu ukiniuliza ni kwanini wala sina jibu! Inatokea, lakini inapita!
 
Habari za Jumapili ndugu zangu wapendwa, nimekuwa najiuliza hili swala,
kila mtu akiwa na upweke ana njia yake ya kuondoa upweke alionao
na mimi pia huwa nina njia zangu za kuondoa upweke nilio nao,lakini kwa
sasa nahisi nafeli, tangu juzi najiona mpweke sana,huwa wa kwanza kuwashauri
marafiki zangu wanapopatwa na hali hii, lakini inaonekana kwangu nimeshindwa
embu marafiki zangu niambieni ni njia gani rahisi ya kuondoa upweke na
kuwa na furaha kama siku nyingine???

Niambie jinsia yako haraka! Ushauri sometimes depends on sex.
 
Pole sana,...
binafsi nikiwa mpweke nalala,....
kama haisaidii nasikiza praise and worship songs,...then
nakaa katika ukimya
maana naamini ni ishara ya Mungu kutaka kusema nawe jambo fulani.
(sio principle kwa wote lakini,that's true for me)
 
Kuhusu namna ya kuwa na furaha, nakumbuka mwanandishi mmoja wa Kiyahudi (jina nimesahau), alisema "Kitu pekee cha kukufanya uwe na furaha ni kazi na marafiki". Hakutaja wapenzi wala familia. Nadhani kwa sababu wapenzi na familia mara nyengine wanaweza kutusaliti, watoto na wapenzi wanaweza kukutoka, ama kwa sababu wana maisha yao, wanaweza kuwa mbali nasi na si kila kitu tunapaswa kuwaeleza wao; Mungu anaweza kuwahitaji au wakaamua kutuwacha. Wanaokuwepo karibu yako siku zote ni rafiki zako na kazi au amali yako.

Ushauri wangu kwa hivyo ni kuwa kukimbilia kwa rafiki mkweli na mwaminifu wa kuongea naye, angalau kwa kutoa dukuduku lako. Huyu atakushauri na kukupa moyo. Si pombe, wala ngono kama walivyoshauri wengi.
Lakini hata kazi zina mwisho wake, unaweza kuachishwa, kufukuzwa au hata kupata redundant, na hata hao marafiki nao ututoka, kutusaliti au kuhama na kuendelea na maisha yao... Ndio maana Waswahili tuna msemo mmoja ...Rafiki mkia wa fisi ukiufuata utakufilisi. Maana marafiki nao ni wanafiki.
 
Back
Top Bottom