Upungufu wa wingi wa damu kwa Watoto (Anaemia)

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
anaemia.jpg


Upungufu wa damu hutokea pale mtu anapokuwa na kiwango kidogo cha seli nyekundu za damu au ikiwa mtu na kiwango kidogo cha himoglobini. Himoglobini au protini ni sehemu muhimu katika kuongeza kiwango cha seli nyekundu za damu kwa sababu ndio hubeba hewa ya oksijeni na kusambaza sehemu mbalimbali za mwili.

Mtoto mwenye upungufu wa damu hawezi kujua kwa sababu anaweza hasionyeshe dalili yoyote.Kupauka kwenye sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo viganyani inaweza kuwa dalili ya upungufu wa damu kwa sababu damu kidogo inasambaa kwenye mishipa ya damu.

Moyo kwenda mbio inaweza kuwa dalii nyingine ya upungufu wa damu kwa sababu unapokuwa na kiwango kidogo cha seli nyekundu za damu, moyo hufanya kazi ya ziada kupata kiwango kilekile cha damu na oksijeni mwilni.

Hali inapozidi kuwa mbaya mtoto ambaye alikuwa mchangamfu anaweza kuanza kulegea haraka. Anaweza kujisikia dhaifu au mchovu kirahisi.

Kwa nini watoto hupata upungufu wa damu?
Uroto kwenye mifupa(bone marrow) katika mwili wa binadamu hutengeneza seli mpya nyekundu za damu kufidia zie za zamani zinazokufa baada ya takribani siku 120.

Mtu anaweza kupata upungufu wa damu kama
seli nyekundu za damu hazitengenezwi za kutosha.
seli nyekundu za damu nyingi zinaharibiwa(Hemolysis).
Seli nyekundu za damu zinapotea (kwa sababu ya kutokwa na damu).

Mwili kutengeneza kiwango kidogo cha seli nyekundu za damu:
Kuna sababu mbalimbali zinazomfanya mwili kushindwa kutengeneza seli nyekundu za damu za kutosha, mara nyingi inaatokana na kukosa madini ya chuma ya kutosha,Madini ya chuma hupatikana katika vyakula Kama nyama, maharage yaliyokaushwa na mboga za majani zenye rangi ya kijani. Bila madini ya chuma mwili hauwezi kutengeneza himoglobini, sehemu ambayo hubeba oksijeni katika seli nyekundu za damu.

Mbali na madini ya chuma, mwili wako unahitaji vitamini B12 na asidi ya foliki ili kutengeneza seli nyekundu za damu. Vitamini B12 hizi hutazipata katika vyakula unavyokula. Vitamini B12 hupatikana katika vyakula vinavyotokana na wanyama, hivyo watu wasiokula nyama(vegeterians), mayai, au maziwa wanatakiwa kuwa na njia nyingine za kupata kiwango kikubwa cha aina hii muhimu ya vitamini. Asidi ya foliki hupatikana katika aina mbalimbali za vyakula kama vile matunda (ndimu, machungwa, zabibu, limao), mboga za majani zenye rangi ya kijani na nafaka zilizoboreshwa.

Upungufu wa damu pia hutokea endapo uroto kwenye mifupa(bone marrow) haufanyi kazi vizuri. Hii inaweza kutokea kutokana na maambukizi au magonjwa yasiyotibika haraka au magonjwa wa figo. Wakati mwingine ingawa ni mara chache sana mtu kuzaliwa bila uwezo wa kutengeneza seli nyekundu za damu za kutosha.

Baadhi ya dawa kama zile zinazotumika kutibu Kansa zinaweza kusababisha uroto kwenye mifupa kushindwa kutengeneza kiwango kikubwa cha seli nyekundu za damu.

Seli nyingi nyekundu za damu Kuharibiwa:Kama itatokea urefu wa maisha ya seli nyekundu za damu kufupishwa kwa sababu yoyote ile,uroto kwenye mifupa(bone marrow) ambapo ndipo zinatengenezwa hautoweza kufidia hicho kiwango kinachopotea.Kuna magonjwa/hali nyingi zinazoaweza kusababisha seli nyekundu za damu kuharibiwa mojawapo ni ugonjwa wa Sicke cell na Malaria.

Kupoteza Kiwango Kikubwa cha Damu: Unapopoteza kiwango kidogo cha damu, kwa mfano unapojikata na kitu chenye ncha kali, au unapotokwa na damu puani uroto mwekundu unaweza kutengeneza damu ya kutosha zaidi hivyo huwezi kupata tatizo a upungufu wa damu(Anemia). Lakini unapopoteza kiwango kikubwa cha damu, kwa mfano katika ajali mbaya, uroto mwekundu hushindwa kutengeneza seli nyekundu za damu haraka kwa ajili ya kufidia.

Pia endapo mtu atapoteza damu kwa kiwango kidogo lakini kwa muda mrefu, anaweza kupata upungufu wa damu pia.Kwa sababu atazidi kupoteza madini ya chuma kwa njia ya damu zaidi ya yale yanayoingia mwilini kwa njia ya chakula. Mwili unapokosa madini ya chuma ya kutosha uroto mwekundu hauwezi kutengeneza seli nyekundu za damu za kutosha. Hai hii inaweza kuwapata wasichana wanaoingia hedhi kwa kipindi kirefu na kutokula vyakula vyenye madini ya chuma ya kutosha, au watu wenye matatizo katika njia ya mfumo wa chakula.

Daktari anaweza Kusaidia nini katika tatizo hili la Upungufu wa wingi wa Damu(Anemia)?
Unapokwenda kumuona daktari, atachukua vipimo na kukuuiza maswali juu ya jinsi ambavyo umekuwa ukijisikia, unakula nini na endapo unatumia dawa ya aina yoyote. Endapo daktari atahisi mtoto ana upungufu wa damu atachukua kipimo cha damu kinachoitwa hamatokriti.

Daktari atachukua ile damu na kuipeeka maabara kwa ajili ya uchunguzi ambapo atataka kujua kiwango cha seli nyekundu za damu, atapima pia kiwango cha himoglobini na kupima ukubwa na umbo la seli. Daktari anaweza pia kuchukua vipimo vingine zaidi kutegemeana na jinsi atakavyohisi nini hasa kinaweza kuwa chanzo cha tatizo, kwa hiyo ni muhimu sana kwenda Hospitalini kwa msaada wa matibabu.

Je, tatizo la upungufu wa damu linatibiwaje?
Tiba sahii ya tatizo hili hutegemeana na nini chanzo/sababu ya Tatizo. Sababu kubwa inayosababisha tatizo hili kwa watoto ni kukosa kiwango cha kutosha cha madini ya chuma katika chakula.Baadhi ya watoto wanatakiwa kupata dawa zenya madini ya chuma ii kusaidia miili yao kutengeneza seli nyekundu zadamu za kutosha. Pia ni muhimu kula vyakula vyenye madini ya chuma ya kutosha kama vile nyama, nafaka ziizoboreshwa, maharage yaliyokaushwa na soya.

Endapo tatizo hilo limesababishwa na maambukizi , tatizo hili itapona kama maambukizi hayo yatatibiwa na mwili utarudi katika hali yake ya kawaida. Endapo chanzo cha tatizo hili ni sababu nyingine, mtoto anaweza kulazimika kumuona mtaalamu maalumu na kupata vipimo zaidi kabla ya kuanza kutibiwa.

Bila kujali tatizo hii imetokana na nini kama kiwango kikubwa cha damu kimepungua, mgonjwa anatakiwa kuongezewa damu na baada ya hapo kuanza matibabu ya nini hasa cha upungufu mkubwa wa wingi wa Damu.

Upungufu wa wingi wa damu kwa Watoto (Anaemia)
 
thanks m.m,nimejifunza kitu.nilikuwa sijui maana ya bone marrow kwa kiswahili.ni uroto kwenye mifupa
 
OK mzizimkavu na shukuru kwa somo hili maana upungu wa damu kwa watoto ni tatizo kubwa sana haswa kwa nchi maskini ninaimani litasaidia sana kwa watakao pita hapa na kusoma kwa makini. Asante sana
 
lakini Mzizimkavu nilikuwa utusaidie kwenye ugonjwa wa sikoseli maana ni ugonjwa hatari sana nimeona kwenye jamii zetu kuna tatizo kubwa na watu wanaokuwa na watoto wenye tatizo hili huwa ni adhabu kuwatunza napengine huwa hawaishi muda mrefu
 
Mzizi mkavu,je matumizi ya antibiotic mara kwa mara kwa mtoto inaweza kuwa ni sababu ya upungufu wa damu kwa mtoto?
 
Usipende kutumia Dawa pasipo na ushauri wa Daktari, dawa zina madhara na zinatibu na kukuletea madhara mwilini uwe muangalifu sana na dawa za kizungu.
Ni kweli kabisa ila mtoto wangu anasumbuliwa na mafua mara kwa mara na daktari ndiye anamwandikiaga hizo dawa.je inaweza kusababisha kutokuongezeka kwa damu ya mtoto?
 
Mi mwanangu anaauka usoni nimeandikiwa folic je nisahihi na folic inasaidia nini?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom