Upungufu wa damu

chokambayaa

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
543
69
Aslam aleykum ma dokta wote wa humu ndani!
naomben ushauri wenu mke wangu amepata tatizo mwili hauna nguvu na anakuwa mchovu sana kapimwa na imeonekana damu imepungua ipo ml 8. Nn kinasababisha damu kupungua? Hosp. Gani naweza kupata matibabu ya kujua chanzo? Nn afanye damu iongezeke kwa haraka?
ahsanten wana JF nategemea msaada toka kwenu
 
juice ya rosela
chemsha matembele anywe
maganda ya mti wa parachichi twanga loweka au chemsha anywe
 
Ale maini yaliyochemshwa kidogo yasiive sana,juice ya ribena,alovera,na maua
 
Damu inaweza kupungua bila hata ya ugonjwa. Kwa mfano:
¤ uzalishwaji duni wa chembe nyekundu za damu, ikiwa mtu hakula mboga mboga na matunda;
¤ mwanamke kupoteza madini ya chuma mwilini kupitia hedhi, hususani kama alitoa damu nyingi;
¤ kuharibika kwa chembe nyekundu za damu kutokana na matatizo ya kurithi, au madhara ya utumiaji wa baadhi ya dawa, dawa zinazoathiri sehemu laini ya mifupa (borne marrow);
¤ kupoteza damu kwa sababu ya minyoo (Hookworms);
¤ mwanamke kuwa mjamzito. Ujaurito unapelekea mabadiliko makumbwa mwilini, ikiwamo kuongezeka kwa maji na kupungua kwa haemoglobini;
¤ N.K
 
Achemshe mashona nguo yanaongeza damu vibaya sana pia matembele, lozera,matunda na mbogamboga nyinine
 
nafikil si 8ml. hata panya ana zaidi ya 8ml za damu. binadamu ana karibia litter 5 amabzo ni 5000ml za damu katika mwili. nafikiri unaongelea haemoglobin 8g/dl. mpeleke kwa daktari akamchunguze then utapata jibu kiurahisi. katika mtandao hu damu haitaongezeka. mpende mkeo.
 
Damu inaweza kupungua bila hata ya ugonjwa. Kwa mfano:
¤ uzalishwaji duni wa chembe nyekundu za damu, ikiwa mtu hakula mboga mboga na matunda;
¤ mwanamke kupoteza madini ya chuma mwilini kupitia hedhi, hususani kama alitoa damu nyingi;
¤ kuharibika kwa chembe nyekundu za damu kutokana na matatizo ya kurithi, au madhara ya utumiaji wa baadhi ya dawa, dawa zinazoathiri sehemu laini ya mifupa (borne marrow);
¤ kupoteza damu kwa sababu ya minyoo (Hookworms);
¤ mwanamke kuwa mjamzito. Ujaurito unapelekea mabadiliko makumbwa mwilini, ikiwamo kuongezeka kwa maji na kupungua kwa haemoglobini;
¤ N.K

ahsante mkuu, matunda anakula na mgonjwa anadai hedhi yake ya kawaida
 
nafikil si 8ml. hata panya ana zaidi ya 8ml za damu. binadamu ana karibia litter 5 amabzo ni 5000ml za damu katika mwili. nafikiri unaongelea haemoglobin 8g/dl. mpeleke kwa daktari akamchunguze then utapata jibu kiurahisi. katika mtandao hu damu haitaongezeka. mpende mkeo.[/QUOTE

nampenda kuliko unavyofikiria na kuuliza huku haina maana kuwa sijaenda hosp. Ndo maana ktk JF kuna JF Dokta
kama huna majibu potezea!!!
 
kama hana appetite ina weza likawa tatizo, mtafutie vyakula vyenye madini ya chuma na folic acid kwa wingi
(google that!). nakushauri usimlishe maini yasiyoiva vizuri utamletea magonjwa mengine
 
kama hana appetite ina weza likawa tatizo, mtafutie vyakula vyenye madini ya chuma na folic acid kwa wingi
(google that!). nakushauri usimlishe maini yasiyoiva vizuri utamletea magonjwa mengine

Pamoja mkuu!
 
Yawezekana anaugua pia malaria mara kwa mara, kama ndiyo yaweza ikawa pia ni sababu
 
Aslam aleykum ma dokta wote wa humu ndani!
naomben ushauri wenu mke wangu amepata tatizo mwili hauna nguvu na anakuwa mchovu sana kapimwa na imeonekana damu imepungua ipo ml 8. Nn kinasababisha damu kupungua? Hosp. Gani naweza kupata matibabu ya kujua chanzo? Nn afanye damu
iongezeke kwa haraka?
ahsanten wana JF nategemea msaada toka kwenu
pole sana mkuu,niende moja kwa moja namna ya kulizuia,ukiweza tafuta vifuatavyo
1.pomesteen power,ni juice,atumie kifuniko kimoja akichanganya na juice ya aloevera au juice yoyote anayoipenda kutwa mara 2.
2.vitamin b12 plus fortified with folic acid ameze vidonge viwili kutwa mara mbili kabla ya kula or nusu saa baada ya kula
3.bery necta.atumie 60mls twice daily for 10 days
kama hali yake siyo zuri mpeleke hospital akiwa na vigezo na kuongezewa dam watamuongezea.
 
@chokambayaa Dawa ya Kuongeza Damu mwilini awe anakunywa maji ya mchicha uliochemshwa Asubuhi kikombe kimoja na jioni kikombe pamoja na kula mchicha wenyewe kwa kufanya hivo damu itarudi Inshaallah.

Upungufu wa Damu Mwilini – Anemia

Ni hali inayompata mtu na kumfanya apungukiwe na chembechembe nyekundu zilizo katika damu ama hizi chembechembe zinaposhindwa kupata hewa inayotosha ya oksigeni kutoka ndani ya mwili wake. Ugonjwa huu sana sana huwashika wanawake kwa sababu kwa kawaida, wao hupoteza madini ya chuma katika miili yao wakati wa hedhi hasa iwapo mtu hutokwa na damu nyingi.

Ni nini baadhi ya dalili?

  • Kuhisi ukiwa mchovu sana au hata kuishiwa kabisa na nguvu
  • Kusikia ukiwa mdhoofu mno
  • Kuhemahema na kupumua haraka haraka
  • Kuwa na mpigo wa moyo wa kasi unapojaribu kujisukuma na kujilazimisha
  • kutembea haraka ama kupanda ngazi.
  • Kuwa na maumivu ya kifua
  • Kushindwa kuweka akili yako pamoja unaposhughulikia jambo
Utajuaje kuwa una upungufu wa damu mwilini?

Ukiona dalili za ugonjwa huu, muone daktari mara moja. Huyo daktari au mhudumu wako wa kiafya atakupima damu yako kubainisha iwapo una huo ugonjwa kwa hakika au la.

Utatabuaje na kuzuia upungufu wa damu mwilini?

Daktari wako atakupa ushauri akwambie iwapo utatumia dawa au umeze tembe badala ya madini ya kukabiliana na hali hii.

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom