Unaweza kutusaidia CV ya Rais wa ANC hapa?
Manufaa kwa nani? Mi naongelea awanufaishe wanafunzi wa kitanzania.
Kabisaa! Hasira ni ukilaza wa namna ya kuchangia mijadara wa watu wanaotoa hoja za msingi. Mtu ashinde kwa hoja nzito na siyo mahasira yake. Issue hapa ni uprofesa wa lipumba unatusaidiaje watanzania? Siyo mpaka tumruhusu kwenda ikulu.1. Punguza jazba.
2. Naheshimu uprofesa wake na nadhani taaluma yake itatusaidia kama akirudi nchini na kuwa mchumi mkuu au labda afundishe vijana waje kutusaidia katika nyanja hiyo.
3. Situmii mdomo hapa. Naandika kwa mikono!
4. Kama unashindwa kuheshimu uhuru wa maoni wa wenzio hustahili kuchangia hapa. Hujalazimishwa.
5. Nina uhuru wa kupost chochote ili mradi sijavunja sheria za JF.
6. Ahsante kwa kusoma. Ok,bye!
Hizo publications tu, ni tosha bila kuonesha shahada zake. Ni msomi wa haja.
Tunaomba na za Mwenyekiti wa CHADEMA. kwi kwi kwi kwi, teh teh teh!
Kwa jinsi ambavyo ndugu zangu, wanachama na washabiki wa CUF wanavyoupamba uprofesa wa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF napatwa na shaka.
Sitaki kuamini kwamba uprofesa wa mtu ndio unampa kigezo cha kuwa na uwezo wa kuongoza watu au nchi. Lakini wenzetu wanataka tuamini hivyo.
Wanataka tuamini hakuna sifa nyingine inayoweza kumpiku mtu aliyebobea katika uchumi na pengine kufanya kazi na IMF.
Hii dhana inatuambia kitu kuhusu watu ama viongozi waliomo katika chama cha CUF. Inatuambia kitu kuhusu wanachama na washabiki wake. Ng'amua.
Jambo moja la msingi: UONGOZI HAUSOMEWI!
Kwahivyo ndugu zangu, kama mnataka kunishawishi nimchague Prof. Lipumba kwenye kinyang'anyiro cha Urais mwaka 2015, naomba mnipe hoja nzito zaidi ya uprofesa wake katika uchumi. Nawasilisha.
Huyu yupo profesional zaidi, kwenye siasa anatumiwa tu na wanasiasa kama Maalim Seif, huyu anapaswa arudi kwenye fani yake PERIOD.
Kwa jinsi ambavyo ndugu zangu, wanachama na washabiki wa CUF wanavyoupamba uprofesa wa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF napatwa na shaka.
Sitaki kuamini kwamba uprofesa wa mtu ndio unampa kigezo cha kuwa na uwezo wa kuongoza watu au nchi. Lakini wenzetu wanataka tuamini hivyo.
Wanataka tuamini hakuna sifa nyingine inayoweza kumpiku mtu aliyebobea katika uchumi na pengine kufanya kazi na IMF.
Hii dhana inatuambia kitu kuhusu watu ama viongozi waliomo katika chama cha CUF. Inatuambia kitu kuhusu wanachama na washabiki wake. Ng'amua.
Jambo moja la msingi: UONGOZI HAUSOMEWI!
Kwahivyo ndugu zangu, kama mnataka kunishawishi nimchague Prof. Lipumba kwenye kinyang'anyiro cha Urais mwaka 2015, naomba mnipe hoja nzito zaidi ya uprofesa wake katika uchumi. Nawasilisha.
Mbona unachanganya mambo mengi kiasi hicho?
Jaribu kuwa na mpangilio. Lipumba anaweza kuwa hakufurahishi lakini shule yake muachie kabisa. Usimuchukie ukajikuta unaondoa hata sifa zake halali!
Una hakika Uongozi haosomewi?
Mbona hata hapa Tz tuna watu wamesomea uongozi? Tunavyo vyuo vya uongozi na digrii za uongozi zipo.
Utagundua uwezo na elimu ya member kwa comments zake, comment kama hii eti anasimamia wachumi wote wa duniani dah!, anatumia ujinga wa watanzania kujijengea jina, inawezekana ndio maana wengi walijitokeza kumpokea, mara kumi kumpokea anayekwenda kutembeza bakuli kuliko huyu.Wanafunzi wa Kitanzania wanafaidika kwa sana tu na wengine zaidi wanaweza kufaidika kwa sana wakimfata. Ulishaenda kwake au ulimwandikia ukataka ushauri wa kiuchumi akakutolea nje?
Anasaidia wanafunzi wa dunia nzima na anasimamia thesis nyingi tu za wanafunzi wa duniani na kwa sasa anasimamia wachumi wote wa duniani. Huoni kuwa ni sifa hiyo kuwa na mtanzania mwenye kipaji hicho?
Utagundua uwezo na elimu ya member kwa comments zake, comment kama hii eti anasimamia wachumi wote wa duniani dah!, anatumia ujinga wa watanzania kujijengea jina, inawezekana ndio maana wengi walijitokeza kumpokea, mara kumi kumpokea anayekwenda kutembeza bakuli kuliko huyu.