Mshindo
JF-Expert Member
- Mar 5, 2009
- 478
- 186
Umesema ukweli katika namna ya ukweli sana! Kila siku nazidi kuelewa conviction iliyo ndani ya watu kama mzee Kitine, Ulimwengu, Prof Shivji, Butiku, Warioba na wafananao na hao katika kupigana huku wakiwa ndani ya CCM. Wameelewa kuwa chama chao kimetekwa na genge la maharamia. Dr. Lwaitama wakati fulani aliliweka vizuri hili, "Natamani wananchi waiweke CCM pembeni ili iweze kujipanga upya (kama chama cha upinzani) na hatimaye irudi kama CCM ile ya awali,chama cha wakulima na wafanyakazi".
Nawashauri die-hards wa CCM. Piganieni chama chenu na Historia yenu. Wanyang'anyi mliowaachia chama kwa kujua au kutokujua kwenu, wamedhamiria kabisa kukibadili "jina"! Wameanza na hili la kumfuta kabisa mwasisi wenu kwenye historia na jitihada hizi ni kubwa sana nyakati hizi!

Mkuu Jasusi, sijui kama umeligundua kuwa hawa wapenzi na watetezi wa CCM ya sasa ndio wenye chuki kubwa na Mwalimu Nyerere wakati hicho chama wakiteteacho yeye ndio mwanzilishi wake.
Ila ukiangalia kwa darubini kali, CCM hii ya Kikwete sio ile ya Nyerere ila inatumia usajili wa CCM ya Nyerere ambayo ilishakufa pamoja na mwanzilishi wake.