Umekosea kuhusu Kassanga Tumbo. Aliwekwa kizuizini 1966 baada ya kurudi kutoka Uingereza alikokuwa balozi wetu na kuyaambia magazeti kuwa amepewa hela na Uingereza kupindua serikali ya Nyerere. He was a fool as far as I can see.Christopher Kassanga Tumbo was arrested in Kenya in 1963 for opposing the East African Federation proposal. He was returned to Tanganyika and held in detention for four years.
Kuhusu Joseph Kasella Bantu ninachokumbuka mimi ni kuwa alikuwa anampinga Nyerere na aliwekwa ndani kwa kuamrisha mapigano ya watu kuibiana ng'ombe kule Nzega. Bahati mbaya taarifa zake hazijaandikwa, lakini hili nalikumbuka.
Ukweli ni kuwa Nyerere alikuwa hapendi sana kubishiwa kitu. Alikuwa anawaadabisha wale waliompinga kwa kutumia sheria ile ile ya Preventative Detention Act waliyokuwa wanatumia wakoloni. Pamoja na mabaya yake yote Nyerere hakumuua yeyote wala kumuacha mtu aozee detention na wala hakuwa na lukuki ya watu walioswekwa detention.