Upinzani MSIENDE Arumeru bila kuboreshwa daftari la wapiga kura!

Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,813
11,126
Akijibu hoja hiyo, kamishina wa NEC Profesa Chaligha alisema,"Kuhusu uandikishaji mpya wa wapigakura alisema jambo hilo haliwezekani kwa sasa na kusisitiza kuwa watakaoruhusiwa kupiga kura ni wale tu waliomo kwenye Daftari la mwaka 2010 na kusisitiza kuwa jambo hilo ni la kisheria"(Mwisho wa kunukuru)

Serikali ya CCM iliruhusu uandikishaji wa wapiga wapya Igunga na vijana wengi wakajiandikisha waliokuja kuwaadhibu vibaya kwenye sanduku la kura na toka wakati ule wakawa wamejua jinsi ya kuiminya demokrasia-KUTORUHUSU VIJANA WAPYA WASAJILIWE KWENYE DAFTARI WAKATI WA CHAGUZI NDOGO.Serikali inajua inachokifanya na nashangaa kwa nn uongozi wa kitaifa wa vyama vya upinzani hawatolei msimamo suala hili!

Upinzani sio mpaka mshindwe kwenye uchaguzi ndiyo mchachamae!Kuruhusu uchaguzi huu uendelee ni sawa na janga la kitaifa na eleweni kuwa kama mtakaa kimywa basi mnazikosa kura maelfu kwa maelfu ya vijana waliokuwa na umri wa miaka 16 na 17 mwaka 2010 na ambao sasa wana haki ya kupiga kura!Simamieni demokrasia na ndipo mtaongeza viti bungeni kwa urahisi zaidi!Mkiwakosa vijana hawa likely CCM ikashinda Arumeru-Mashariki kwani base yao ya wapiga kura hasa wanawake na wazee itakuwa ipo haijatingishwa!

kama NEC itazidi ng'ang'ania kuwa daftari la wapiga kura halitaboreshwa Arumeru-Mashariki nawashauri kwa umoja wenu tangazeni kujitoa kwenye uchaguzi halafu mnakwenda Mahakamani kufungua kesi ili Mahakama itamke"kupiga na kupigiwa kura kwa mtu mwenye miaka kuanzia 18 jimboni Arumeru-Mashariki hakuwezi zuiliwa kwa sababu tu ni gharama kubwa kuwaandikisha kwani ni haki yao msingi ndani ya katiba"
 
Malafyale naunga mkono hoja lazima timbili litengenezwe kuhakikisha daftari linaboreshwa CCM na upuuuzi wao hawawezi kuwa ndio vinara wa kupindisha sheria hicho kibabu Jaji Lubuva kama anataka kufa kwa presha acheze na sisi ,hakuna uchaguzi mpaka daftari liboreshwe
 
Ndio imetoka hiyo....hivi hawa wanasiasa wa upinzani wanafanya nini wasilione hili?
 
Jamani kama mpo humu viongoz wetu wa cdm plzzzzz, fanyieni kazi ujumbe huu kwani ni muhimu sana kwa harakati za mbadiliko ktk jimbo la arumeru also sio wa chadema 2 bali hata kama mpo viongozi wa vyama vingine vya upinzani lakini sio CUF.
 
Hizo ni njama za wazi za Ccm, za kulazimisha ushindi. Huyu Profesa Chaligha, alichokitamka ni uropokaji
wa maneno tu, hususani yeye inabidi atekeleze kazi inayomuhusu ya kuboresha Daftari la wapiga kura
mfumo, kanuni na sheria za uchaguzi kama zinavyohitajika, Kabla uchaguzi haujaanza.
Kwa upande wa CDM. kunahitajika kuwa makini zaidi, katika huu uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru.
Umakini zaidi uwepo kwa mawakala wa CDM, katika kulinda kura. Meneja wa kampeni na team yake
iongezwe maradufu ili kuwe na nguvu zaidi ya upinzani, nasema hivyo kwa sababu meneja na team yake
wote wanafaa kama ilivyoongozwa uzini, na hamna swala la huyu anafaa au huyu hafai, swala
hapo ni kutafakari kwa kuongeza nguvu zaidi, kwa sababu mimi nahamini Vijana wote CDM ni watu makini
ikiwa watajumiika pamoja, kwenye lengo letu la ushindi. Katika siku ya nyuma kulikuwa na uchangiaji
humu wa swala huyu anafaa na huyu hafai, nafikiri wazo ilo tuliondoe na umuhimu ni kuunganisha
nguvu zetu wote kwa pamoja. Na njia pekee ya kuleta ushindi na kumwondoa adui wa Taifa letu
Ccm pamoja na Serikali yake. NEC mjitayarishe kutuletea Transparent ballot box kunzia uchaguzi huu
mdogo wa Arumeru. Na kuendelea kuepusha uchakachuaji. Muhusika Kamishna wa NEC haya ndio
yanayokuhusu ufanye zaidi ya kuboresha Daftari la wapiga kura. Picha ya mfano katika post nyingine,
sasa hivi kumeshakuwa na virus siwezi ku upload.
 
Nafikiri wakienda itakuwa bora zaidi, mkazo uwe kwa kamishna wa Nec kuboresha Daftari la wapiga kura.
Na kuongezea Transparent ballot box, ili kuwe na uwazi zaidi.
mfano ndio huo hapo kuepusha matatizo ya kuchakachua kura.

Click Here:
 

Attachments

  • 061_front_view_ballot_box.preview.jpg
    061_front_view_ballot_box.preview.jpg
    21 KB · Views: 32
Back
Top Bottom