Mparee2
JF-Expert Member
- Sep 2, 2012
- 2,572
- 4,241
Binafsi napenda sana jitihada za Waziri wetu Lukuvi ambaye amekuwa kati ya mawaziri wachapa kazi. Hata hivyo sikubaliani kabisa na hii kauli yake ya kupima ardhi nchi nzima.
Kimsingi hii nchi ina population ya kawaida, hapo inaongezeka kila siku. Kwa kauli yako watu wanajaa na hasa wenye uwezo watajichukulia mapori na kuyapatia hati. Mimi naona unatengeza tatizo lingine litakaloleta mgogoro mkubwa wa ardhi miaka ijayo, pale watoto watakokua wakute kila eneo lina mtu.
Natamani kujua hili umelipata wapi, nchi gani inayoendana na sisi na kama limewasaidia? Mimi sina Elimu ya mambo ya Ardhi ila naona hatari kubwa itakayotukumba baadae, kama hutabadilisha huu muelekeo.
Naomba uelekeze watu wapimiwe Ardhi kwenye yale maeneo wanavyoyamiliki na kuyaendeleza, na Mapori yetu ambayo hayajaendelezwa yaendelee kubaki wazi.
Kwa mtazamo wangu, hili ni la kupima nchi nzima, litatuletea ukabila kwa kila kabila kumiliki maeneo yanayowazunguka, na vijana wengi wajao hawatakuwa na maeneo.
Binafsi naona unaandaa bomu litakalolipuka kwenye miaka ishirini na kuendelea ijayo.
Nakushauri uombe Ushauri kwa wataalam, ila sio wapima Ardhi kwani wengi hatuwaamini hadi wajisafishe.