waziri2020
Senior Member
- May 31, 2019
- 190
- 451
Shule ya Sekondari ya Ngarenaro iliyopo kata ya Ngarenaro jiji la Arusha, imetia aibu ya Mwaka kwa kuongoza kuibuka na sifuri nyingi zipatazo 54 katika matokeo ya kidato cha Nne , yaliyotangazwa kitaifa jana.
Kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya elimu wamebaini kuwa taizo la anguko la shule hiyo ni diwani wa kata husika ,Isaya Doita ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya elimu jiji la Arusha ambaye amejikita kutafuta maslahi binafsi kutoka kwa wakuu wa shule na walimu wa kawaida jambo linalosababisha walimu kubadilishwa kila kukicha wanaposhindwa kumpatia chochote.
Diwani huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo anadaiwa pia kujipangia utaratibu wa kulipwa posho pindi anapoenda kwenye vikao mbalimbali shuleni hapo,kinyume na utaratibu.
"Huyo diwani amekuwa kero sana kwenye maendeleo ya kitaaluma katika jiji la Arusha, maana anapenda pesa kuliko utendaji ndio maana hata walimu hawana morari wa kufundisha"
Katika hatua nyingine wazazi wa shule ya msingi Mwangaza na Ngarenaro zilizopo katika kata hiyo,wamemlalamikia afisa elimu wa jiji,BAKARI HUSEIN na Diwani DOITA,kuwalazimisha wazazi kulipa kiasi cha sh,5000 kupitia lipa namba kwa ajili ya kuni za kupikia chakula kinachotolewa na mfadhili ,Mount Meru Millers ambaye amekuwa akihudumia chakula kwa zaidi ya miaka mitatu bila kuwepo na usumbufu wowote huku wazazi wakishiriki kununua viamba upishi kupitia kamati zao za shule.
Hata hivyo hadi sasa wanafunzi hawajawahi kupatiwa chakula shuleni jambo ambalo linaoneshwa wazi ni dili la viongozi hao wawili kujipatia asilimia 10 ya fedha hizo .
Suala hilo limekuwa kero kubwa kwa walimu wakuu wa shule zote 49 za msingi jiji la Arusha, kushurutishwa kuhamasisha wazazi kulipa pesa hizo kupitia lipa namba ndipo wapewe chakula na mfadhili ,na kuacha majukumu yao ya kufundisha watoto wakifuatilia usajiri wa lipa namba tofauti tofatu.
Baadhi ya walimu wamelalamikia usumbufu wanaoupata kutoka kwa afisa elimu Bakari,wakidai huo utaratibu ni mpya na umelenga kuwanufaisha wao pindi wanapowalazimisha wazazi kulipa pesa kinyume na utaratibu.
Mmoja ya walimu wakuu alidai kuwa Afisa elimu huyo aliwahi kufanya ziara akiwa na Isaya Doita ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya elimu,katika shule ya Arusha,Ambapo waliomba pesa ya mafuta lakini mkuu wa shule hiyo aliyefahamika kwa jina la Njololoi aligoma kutoa pesa hiyo jambo lililowakasirisha kiasi cha kumhamisha kituo cha kazi kwenda shule ya msingi Salei iliyopo kata ya Ungalimited.