Upigaji:Mama KANUMBA aambulia "chenchi" ya 4 m kati ya 52 m!

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,139
[h=3]MAMA KANUMBA AAMBULIA MIL.4 KATI YA MIL.52 ZILIZOCHANGWA KWA AJILI YA MSIBA WA MWANAWE[/h]
SOURCE:MAMAPIPIRO BLOG

WAKATI kamati ya Mazishi ya msanii wa Filamu nchini Steven Kanumba ikikanusha kuwepo ubadhirifu Fedha za Mapato na Matumizi zilizokusanywa tangu kifo cha msanii huyo, leo imeanika mchanganuo wa Mapato na Matumizi ya fedha zilizokusanywa.

Mwenyekiti wa Kamati Hiyo Gabriel Mtitu amewaambia waandishi wa Habari jijini Dar es salaam jumla ya shilingi mil.52,352,000 tu ndizo zilikusanywa.

Alisema katika fedha hizo zilizopatikana zilitumika shilingi milioni 52,102,000, hivyo kubaki shingi milioni nne tu ambazo tayari amekabidhiwa mama mzazi wa marehemu.

Aidha Mtitu amesema pesa zilizopatikana kwenye M Pesa ni shilingi 300,000 wakati kwenye Tigo Pesa ni shilingi 150,000.

Katika hatua nyingine Mtitu ametoa shukrani kwa wale wote ambao wameweza kutoa michango yao ya hali na mali katika kufanikisha msiba huo.
 
mbona serikali ilisema itagarimia mazishi yake ?? imekuaje tena hizo pesa zikatumika tena ????????????????????????/
 
Nakumbuka niliandika kitu kama hicho mahali fulani, hawa watu njaa kali, angalau SK Alikuwa amejaribu, waliobaki hamna kitu, Jana nilinunua CD ya SK Magomeni, cha Ajbu nilipokwenda kuiangalia nikakuta ni tofauti na kile nilichotarajia, nilijiuliza maswali mengi sana, Nani anasimamia kazi za Steven baada ya kifo chake??? Kama huyu Mtitu? Sidhani kama anaaminika.
 
MAMA KANUMBA AAMBULIA MIL.4 KATI YA MIL.52 ZILIZOCHANGWA KWA AJILI YA MSIBA WA MWANAWE

SOURCE:MAMAPIPIRO BLOG

WAKATI kamati ya Mazishi ya msanii wa Filamu nchini Steven Kanumba ikikanusha kuwepo ubadhirifu Fedha za Mapato na Matumizi zilizokusanywa tangu kifo cha msanii huyo, leo imeanika mchanganuo wa Mapato na Matumizi ya fedha zilizokusanywa.

Mwenyekiti wa Kamati Hiyo Gabriel Mtitu amewaambia waandishi wa Habari jijini Dar es salaam jumla ya shilingi mil.52,352,000 tu ndizo zilikusanywa.

Alisema katika fedha hizo zilizopatikana zilitumika shilingi milioni 52,102,000, hivyo kubaki shingi milioni nne tu ambazo tayari amekabidhiwa mama mzazi wa marehemu.

Aidha Mtitu amesema pesa zilizopatikana kwenye M Pesa ni shilingi 300,000 wakati kwenye Tigo Pesa ni shilingi 150,000.

Katika hatua nyingine Mtitu ametoa shukrani kwa wale wote ambao wameweza kutoa michango yao ya hali na mali katika kufanikisha msiba huo.

Ruge Mutahaba ni shetani mtu !
 
Ruge naye msanii?
Jamani hamuoni mashada hayoyawezekana yalinunuliwa 1 m kila moja?
 
Kwani pesa ilikusanywa ya nini? Si ilikua ya maziko. Basi kama ndo hivyo basi wameshaizika. Bi mkubwa si anahitaji nauli tu.
 
Back
Top Bottom