Upepo mkali wavuma - Michuzi afungua milango kwa vyote vya siasa

Status
Not open for further replies.

Njele

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
275
121
38180_10150240987845125_4030115_n.jpg

Michuzi katika bandiko muhimu leo kwenye blog yake, amesema kumekuwepo na upungufu mkubwa wa picha zinazoingia kwenye mtiririko wa blog yake kila siku kutokana na vyama vya siasa kutopeleka picha na habari. Amesema wahusika na propaganda vyamani hawapeleki habari, na hivyo anawaasa wapeleke habari na picha kutangaza sera za vyama vyao for free.

Ninachojiuliza, kwa nini walisitisha kupeleka habari huko isipokuwa CCM?

Kuna blog nyingi tu kama Mjengwa, na wengine wana habari nyingi tu za vyama vya siasa, wahusika hupeleka au timu ya bloggers ndiyo inayohaha kupata habari hizo kupamba blog zao?
 
Ashaona mlango wa kuelekea kupewa uDC unazidi kuwa mwembamba!......kaamua kurudi nyuma na kupanga atoke vipi!
 
Ashaona mlango wa kuelekea kupewa uDC unazidi kuwa mwembamba!......kaamua kurudi nyuma na kupanga atoke vipi!

Miti aliyozoea nyani kujihifadhi inaanza kuteleza, na hifadhi inayobaki ni ardhi ambayo si salama kwa nyani.
 
Hovyo kabisa huyu jamaa..si alikuwa sehemu ya kampeni za ccm 2010 na alikuwa kwenye msafara wa jk toka day one ss kakumbuka nini!aendelee kuandika habari za wafu aone mwisho wa hicho ki blog chake...njaa mbaya sana michuzi
 
Gamba yule watu wameshamstukia sasa Blog inaanguka ndio anaanza kujibaraguza.
 
great thimkers huu sio muda wa kumnanga mtu! mkiona mtu anarudi nyuma na kutambua upepo unaelekea wapi, ni vizuri kumpokea na kufurahi kuongeza idadi ya watu kundini wananojielewa tena wana uwezo wakutoa msaaada kubwa! kikubwa ni kumpa support jamaa awe miongoni mwa wanavuguvugu tu.
 
umenena vyema mkuu, alielala anapoamka hachekwi bali kupokelewa ili aamshe wengine.
 
Aiseee baba yangu michuzi mambo magumu ehhhhh itakula kwako

ngoja nianzishe mbege blog
 
Sio peke yk anaehaha!Midia nyingi zimeshashituka haziuzi!

"Upepo tu unaovuma kwa muda utapita na kutulia wenyewe", alisema baba rizone aliyesema hapo awali vyama vya upinzani ni vya msimu tu wakati sasa natekeleza sera za vyama alivyoviita vya msimu.
 
great thimkers huu sio muda wa kumnanga mtu! mkiona mtu anarudi nyuma na kutambua upepo unaelekea wapi, ni vizuri kumpokea na kufurahi kuongeza idadi ya watu kundini wananojielewa tena wana uwezo wakutoa msaaada kubwa! kikubwa ni kumpa support jamaa awe miongoni mwa wanavuguvugu tu.

Mkuuu, hawa watu wengine kabla ya kuwapokea ni vizuri mka-wapa makav laiv watie adabu. ni wanafiki hawa mkiwapokea kwa tabasamu watawaona hamnazo, wanajali sana maslahi binafsi na kujipendekeza kwenye hili serikali lililopoteza mwelekeo, badala ya kusimama upande mmoja na wanaopinga dhuluma. mtu anayeshabikia serikali ya ccm kwangu huwa namuona haitakii mema Tanzania, HIVI UNAWEZA VIPI KULISHABIKIA LI SERIKALI BOVU KAMA HILI??? inatia kichefuchefu!!!!!!!!!
 
JK kamtosa, sasa ndo anasaka mlango wa kutokea... Hakuna cha UDC wala Mpiga Picha Mkuu wa Rais kama ulivyotegemea! Na hivi kimbunga cha M4C kinavyopuliza mpaka paa za vigae, mtahenya mwaka huu nyie CCM Masalia kama akina Michuzi!
 
Status
Not open for further replies.
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom