masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 17,882
- 13,171
Kupanga ni kuchagua! Kupanga kunategemea nguvu yako kiuchumi; utapanga kikubwa kama uchumi wako mkubwa na utapanga kidogo kama uchumi wako mdogo.
Duniani kote maji kwa matumizi mbalimbali yanatokana na vyanzo vifuatavyo:
- Surface water kwa maana ya mito na maziwa;
- Rainwater harvesting kwa maana ya mabwawa yaliyoko katika maeneo makame; na
- Groundwater kwa maana ya visima virefu na vifupi pia chemchem.
Maji kutoka katika vyanzo vyote hapo juu unaweza kuyapata kwa kuyafuata huko huko yaliko au kwa kutumia technolojia mbalimbali ukayapampu hadi unakotaka kuyafikisha. Technolojia zinazotumia ni pamoja na:
- Ku-pump kwa kutumia mafuta au umeme
- Ku-pump kwa kutumia upepo
- Kutumia nguvu ya mserereko (Gravity)
Ili uweze kutumia technolojia hizo kwa ufanisi huna budi na nguvu kubwa ya kiuchumi ili uweze kuukamilisha mradi na pia kuuendesha ili uwe endelevu.
Kwa kuwa wananchi wetu wengi ni maskini ambao kipato chao kwa siku ni chini ya dola moja technolojia nyepesi na rahisi kwa wao kuiendesha ni kuwa na kisima cha maji kilichofungwa pampu ya mkono au kutumia ndoo kwa visima vifupi.
Kwa maeneo ya mijini kwa kuwa watu wengi wana uchumi mkubwa pampu za umeme au dizeli hutumika na maji kusambazwa kwa mabomba hadi yanapohitajika (Nyumbani). Nchini kwetu kuna miji kama Arusha, Dodoma na Mtwara ambayo inategemea maji kwa 100% kutoka visimani na kusambazwa kwa mabomba.
Faida mojawapo ya maji ya visima kama vimechimbwa mbali ya makazi ya watu huwa ni safi na salama na kwa kiwango kikubwa hayahitaji tiba (Treatment) hivyo kuwa rahisi kwa miradi ya namna hii kuiendesha. Tofauti na maji ya mabwawa, mito na maziwa ambayo bila ya kufanyiwa tiba ni hatari kwa afya ya binadamu kwa kuwa huwa na tope jingi na vimelea vya magonjwa na hivyo uendeshaji wa miradi hii huwa ghali kwa kuwa na gharama za ziada za madawa ya kutibia maji.
Kwa kifupi serikali inapohamasisha watu kuchimba visima ni kwa sababu ya kuona kuwa wananchi wake wana uwezo mdogo wa kuiendesha. Hata hivyo lengo ni kuwa endapo hali ya uchumi wa wananchi itaimarika basi technolojia inaweza kubadilishwa na kusambaza maji kwa njia ya mabomba. Visima vilivyochmbwa kwa utaalam sahihi vinaweza kudumu kwa miaka mingi na mfano ni Dodoma ambako kuna visima vilichimbwa miaka ya 1930 mpaka leo vinatoa maji!
Safi sana mkuu Ileje kwa kutoa maelezo ya ufasaha katika mada hii.
Nakubaliana kabisa kuwa provision ya maji ni suala la uchumi na uhandisi, na fani hizo ndio zinaweza kutoa majibu sahihi juu ya utatuzi wa wananchi kupata au kutopata maji,of course mipango ikikaa sawa.