Upeo wa Maige watia mashaka makubwa!

Eddie mkono wa mjinga kama huu wa kwako huandika popote pale..............haitoshi kusema ni utumbo mtupu bila ya kuonyesha sababu ya kwanini umeona hivyo........kwa wewe ambaye umo humu ndani ya JF kuanzia 2008 na huna michango yoyote ile....inapendeza kama ukiendelea kuufyata tu kama ulivyokuwa umejizoeleza.........uko kama vile haupo.............though living but you are a dead man walking............
Kuna wimbo ulikuwa maarufu sana miaka ya themanini na sehemu ya mashairi yake ilikuwa hivi: Wape, wape--eee vidonge vyao. wakitema, wakimeza shauri yao.
 
Mkuu ruta upeo wake hautofautiani na yule aliyemteua na kumpa Uwaziri na ndio sababu kubwa ya nchi yetu kuyumba sana. Kwa maoni yangu sasa hivi si ajabu tungetakiwa kuwa na Waziri Mkuu wa tatu au hata zaidi baada ya Lowassa, Pinda ambaye naye kazi imemshinda...Katiba mpya ni lazima kuwepo na kipengele ambacho kitaruhusu Bunge kumuengua madarakani Rais pale ambapo utendaji wake ni wa kiwango cha chini.

Kipengele kama hiki kingekuwepo katika katiba ya sasa na Wabunge hata kama ni wa Magamba wana mapenzi ya kweli na nchi yetu badi Kikwete alistahili kutemwa 2007/2008 maana kulikuwa na ushahidi wa kutosha kwamba uongozi wa nchi umemshinda.
 
Last edited by a moderator:
Wakati akisulubiwa na Kamati ya Bunge ya Maliasili na Mazingira, aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Maige alikimbilia kwenye vyombo vya khabari na akawasagia Kamati husika akidai imehongwa na yeye ni mtu mwadilifu sana. Akiwa Bungeni aliishutumu Kamati tajwa chini ya uenyekiti wa Mhe. James Lembeli imwogope Mungu na ya kuwa inamwandama kwa kumwonea gere, chuki na fitina.

Mhe. Lembeli alimkumbusha Maige ya kuwa asilitaje jina la Mungu bure kwa kuwa Mungu siyo wa Maige tu bali ni wa wote viumbe vyake..........................La ajabu na kushangaza sana, jana wakati akimkabidhi wizara tajwa mrithi wake Balozi Kagasheki, Mhe. Maige alisahau kauli zake za awali za ya kuwa yeye ni mwadilifu
na akakiri ya kuwa alishindwa kuwasimamia watendaji ndani ya wizara yake na hata akatolewa kafara........Hivi kafara hutolewa kwa mtu aliyeshindwa majukumu yake au kwa yule aliyeonewa?.....Maige kwa kukiri huku kunafanya kauli zake bungeni na kwenye vyombo vya khabari kuwa hakuwa mkweli hata kidogo na ya kuwa utetezi wake ulikuwa kwa masilahi yake binafsi na wala siyo ya taifa............na ubinafsi wake ulichanuka pale alipomshukuru JK badala ya Mwenyezi Mungu kwa kumpa ugali na kumnufaisha yeye binafsi............Hili kweli linatisha sana!.......Maige safari hii baada ya kutenguliwa hakumkumbuka Mungu kama alivyokuwa Bungeni na hata kumshukuru angalau kwa kumwachia kuwa hai hadi jana hiyo huku akiwa kinara wa ufisadi au hata kuishukuru familia yake kwa kumruhusu na kumvumilia kuwepo kwake kwenye ulingo wa siasa..................au basi hata kuwashukuru wapigakura wajimbo lake ambao ndiyo waliomweka kwenye chati za siasa hata huyo JK akamwona angeliweza kumfaa kwenye cabinet yake...................Ingawaje hata JK mwenyewe anaonekana ni bomu kwa kuteua watu ambao uwezo wao wa kufikiri ni finyu kama huyu............

Mhe. Maige hakujilaumu yeye binafsi kwa kuelezea umma yawaje baada ya kuwa waziri ndiyo aligundua
kumbe yeye ni mjasiria mali nguli na hata angeliweza kujirundikia mabilioni ya mapesa na kuwa na mali nyingi zisizohamishika ambazo kama bila ya kufanya biashara ya siasa hayo yasingeliwezekana.................

Kwa kifupi kauli tatanishi za Maige na kukwepa kujilaumu mwenyewe huku akilaumu washirika wake wa karibu ndani ya wizara aliyokuwa akiiongoza ni dalili ya upeo wake ni finyu............................sioni utetezi mwingine.....................na kwa khali hii baada ya Takukuru kumweka kibindoni usishangae kuona anapatwa na kiharusi au jirani ya balaa za namna hiyo.......................sioni kama ana uwezo wa kuhimili mikikimikiki ya namna hizo hata chembe maana mwenyewe hajui anasimamia nini..........
Acha majungu dogo!
 
Kama kichwani ni sifuri learn to learn in silence......................usijitutumue bahari hii siyo kwa vijidagaa kama wewe

achana nae mkuu watu wengine wapo humu jf kuongeza idadi ya member lakini ni ziro , kama watu hawana mchango wowote bora basi wawe wasomaji wa mada za wanajamvi wenzao kama wenzetu sisi sio kubwabwaja pasipo na haja ya hoja
 
Mkuu Ruta..."wanaolazimisha kutokukuelewa" ni wachache kuliko waliokuelewa...piga konde! Una mengi ya kufanya
 
bdo inabidi umwelewe Eddie kazi yake ni kutuvuruga tuache kujadili maige tuanze kumjadili yeye..........jambo ambalo hatutalikubalia abadilishe somo kwa kuingiza upumbavu wake humu kwa kujidai kuna kitu anajua kumbe hakuna ajuacho hata chembe ile.......


Ndugu, mimi nafikiri hapa JF kuna tatizo kubwa sana la focus kuhusiana na topic zinazojadiliwa maana kuna watu kwa makusudi kabisa wanaamuaga kuingilia topic na kuleta hoja zisizo na misingi na watu wote kwa hasira wakaacha kujadili topic iliyopo na kuanza kushambuliana kwa kujibizana mambo yasio na msingi kabisa, sasa tunatakiwa kujifunza kubaki ndani ya topic na kuwa-ignore hawa wanaoleta mizaha, sasa muda wote mnaobishana na huyu Eddie badala yake mngekua mnatoa hoja ya kuhusiana na mada hata kama anaandika (utumbo) kuhusiana na mchango wa mtu yeyote sioni haja ya kumjibu maana hajatoa hoja watu wachangie hoja na wajingawajinga kama huyu Eddie watakosa mashiko lakini kwa kujibizana nao mpaka mwisho wa siku hakuna kitakacho badilika, kwamaana hiyo sisi tujifunze kuachana na kupelekwapelekwa na watu wa aina hii ambao wapo wengi tunawajua.
 
Huyu Maige kwa kauli zake za kujitetea alizotoa leo kupitia taarifa kwenye Blog kama ya Michuzii, zimeweka wazi kwamba cheo cha Uwaziri Tanzania ya leo ni cheap sana ukilinganisha na pale ilipokuwa zamani.

Kama ni matokeo ya maendeleo ya teknolojia ya Habari na Utandawazi au vingininevyo, hiyo itakuwa kwako Mhusika kutafakari na kufikia uamuzi. Lakini kwa ujumla, inabidi wafuatiliaji mambo tusherehekee kwa jambo hili: kwa maana kwamba, ni nadra kwa Waziri mzima kudiriki kutumia jukwaa la utandawazi aka internet kujitetea na kujisafisha baada ya kuhusishwa na tuhuma za ufisadi.
 
Inatosha kuhusu Eddie na mtoa mada - tunaonaje tukiendelea na mada sasa?

Nafikiri tatizo la kina Maige ni kukosekana chombo cha kushughulikia maadili ya viongozi - najua kipo chombo chenye jina hili LAKINI kila Mtanzania anajua haifanyi chochote kinachofana na kazi yake-kipo tu.
Nawaza : ni kwa vipi hili litarekebishwa katika katiba ili tuondokane na vyombo vya majina?
 
Inatosha kuhusu Eddie na mtoa mada - tunaonaje tukiendelea na mada sasa?

Nafikiri tatizo la kina Maige ni kukosekana chombo cha kushughulikia maadili ya viongozi - najua kipo chombo chenye jina hili LAKINI kila Mtanzania anajua haifanyi chochote kinachofana na kazi yake-kipo tu.
Nawaza : ni kwa vipi hili litarekebishwa katika katiba ili tuondokane na vyombo vya majina?
Nitarudi na uzi huu karibuni ukiwahi ruksa!
 
Mkuu I would expect you to analyse critical this thread and come out with counter-arguments and not abusive language.
 
Back
Top Bottom