Upeo wa Maige watia mashaka makubwa!

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,424
911,172
Wakati akisulubiwa na Kamati ya Bunge ya Maliasili na Mazingira, aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Maige alikimbilia kwenye vyombo vya khabari na akawasagia Kamati husika akidai imehongwa na yeye ni mtu mwadilifu sana. Akiwa Bungeni aliishutumu Kamati tajwa chini ya uenyekiti wa Mhe. James Lembeli imwogope Mungu na ya kuwa inamwandama kwa kumwonea gere, chuki na fitina.

Mhe. Lembeli alimkumbusha Maige ya kuwa asilitaje jina la Mungu bure kwa kuwa Mungu siyo wa Maige tu bali ni wa wote viumbe vyake..........................La ajabu na kushangaza sana, jana wakati akimkabidhi wizara tajwa mrithi wake Balozi Kagasheki, Mhe. Maige alisahau kauli zake za awali za ya kuwa yeye ni mwadilifu
na akakiri ya kuwa alishindwa kuwasimamia watendaji ndani ya wizara yake na hata akatolewa kafara........Hivi kafara hutolewa kwa mtu aliyeshindwa majukumu yake au kwa yule aliyeonewa?.....Maige kwa kukiri huku kunafanya kauli zake bungeni na kwenye vyombo vya khabari kuwa hakuwa mkweli hata kidogo na ya kuwa utetezi wake ulikuwa kwa masilahi yake binafsi na wala siyo ya taifa............na ubinafsi wake ulichanuka pale alipomshukuru JK badala ya Mwenyezi Mungu kwa kumpa ugali na kumnufaisha yeye binafsi............Hili kweli linatisha sana!.......Maige safari hii baada ya kutenguliwa hakumkumbuka Mungu kama alivyokuwa Bungeni na hata kumshukuru angalau kwa kumwachia kuwa hai hadi jana hiyo huku akiwa kinara wa ufisadi au hata kuishukuru familia yake kwa kumruhusu na kumvumilia kuwepo kwake kwenye ulingo wa siasa..................au basi hata kuwashukuru wapigakura wajimbo lake ambao ndiyo waliomweka kwenye chati za siasa hata huyo JK akamwona angeliweza kumfaa kwenye cabinet yake...................Ingawaje hata JK mwenyewe anaonekana ni bomu kwa kuteua watu ambao uwezo wao wa kufikiri ni finyu kama huyu............

Mhe. Maige hakujilaumu yeye binafsi kwa kuelezea umma yawaje baada ya kuwa waziri ndiyo aligundua
kumbe yeye ni mjasiria mali nguli na hata angeliweza kujirundikia mabilioni ya mapesa na kuwa na mali nyingi zisizohamishika ambazo kama bila ya kufanya biashara ya siasa hayo yasingeliwezekana.................

Kwa kifupi kauli tatanishi za Maige na kukwepa kujilaumu mwenyewe huku akilaumu washirika wake wa karibu ndani ya wizara aliyokuwa akiiongoza ni dalili ya upeo wake ni finyu............................sioni utetezi mwingine.....................na kwa khali hii baada ya Takukuru kumweka kibindoni usishangae kuona anapatwa na kiharusi au jirani ya balaa za namna hiyo.......................sioni kama ana uwezo wa kuhimili mikikimikiki ya namna hizo hata chembe maana mwenyewe hajui anasimamia nini..........
 
Huyu jamaa wakati anasoma plae IFM hakuwai kuwa kiongozi,alikuwa msongo wakupenda kusoma kwa mashindano,alikuwa ni anti social kabisa,na shangaa sana siasa kaijulia wapi,labda ukubwani au...maana wanasiasa wazuri huwa waanzia mashule,ila ndio kashapotea tena arudi kwa Msasila akafundishe masomo ya jioni......ila kwake kama kijana ni msikitiko sana ndani ya mwaka mmoja kama full minister kachemsha vibaya mmno....
 
Utumbo mtupu! ndio umeandika nini sasa? unai aibisha JF

Eddie mkono wa mjinga kama huu wa kwako huandika popote pale..............haitoshi kusema ni utumbo mtupu bila ya kuonyesha sababu ya kwanini umeona hivyo........kwa wewe ambaye umo humu ndani ya JF kuanzia 2008 na huna michango yoyote ile....inapendeza kama ukiendelea kuufyata tu kama ulivyokuwa umejizoeleza.........uko kama vile haupo.............though living but you are a dead man walking............
 
Panga La Shaba.............subiria takukuru wamtie mkononi ndipo atajua kama kweli anavipaji au alivalia suti ya wengineo...........
 
Last edited by a moderator:
JK alisema hao jamaa watashughulikiwa ngoja tuvute subira. Mramba na Yona walishtakiwa kwa kutumia Madaraka vibya sana sasa cjui akina Maige na wenzake itakuwaje kwa hili.
 
Utumbo mtupu! ndio umeandika nini sasa? unai aibisha JF

Acha kuponda mawazo ya mwenzio, utumbo gani alioandika? yote aliyosema ni kweli! au hufuatilii matukio na taarifa mbali mbali? Kwani siku ana jitetea bungeni akitaja jina la Mungu hukumuona wala kumsikia? Aliye andika namsifu sababu ana kumbu kumbu nzuri. UTUMBO NI WEWE MNAO JAZA JF KWA MAWAZO MGANDO NA UWEZO FINYU WA KUFIKIRI KABLA HAMJA CHANGIA THREAD ZA WATU.
 
Eddie mkono wa mjinga kama huu wa kwako huandika popote pale..............haitoshi kusema ni utumbo mtupu bila ya kuonyesha sababu ya kwanini umeona hivyo........kwa wewe ambaye umo humu ndani ya JF kuanzia 2008 na huna michango yoyote ile....inapendeza kama ukiendelea kuufyata tu kama ulivyokuwa umejizoeleza.........uko kama vile haupo.............though living but you are a dead man walking............

Mkono wa **** kama wewe ndio unaandika utumbo huo hapo juu? kama mabandiko mengi ni "mchango" then no wonder unajaza utumbo tu humu.
 
We kilaza nyamaza kimya, naona tangu 2008 hujafanya lolote la maana, wakati mwingine bora kuufyata kuliko kutapika pumba kama ulizotoa hapa

Manyanza nchi hii ipo shida kubwa sana..................huyu anayejiita Eddie yupo JF kuanzia 2008 lakini huwa hana michango yoyote ile kazi kurushia wengineo matusi na bila hata ya kutoa maoni yake kama yapo...........it is very sad........
 
Last edited by a moderator:
Mkono wa **** kama wewe ndio unaandika utumbo huo hapo juu? kama mabandiko mengi ni "mchango" then no wonder unajaza utumbo tu humu.

Eddie hebu fafanua ni kwa nini unaona hizo khoja za kweli zilizotolewa bungeni na jana na zipo kwenye vyombo vya khabari hazifai kuandikwa humu JF?
 
Last edited by a moderator:
Mbona ameandika nyama! Usi "generalize" kuwa ameaibisha JF.

Eddie hebu mweleze Sometimes kwani yeye anaona nimeandkika minofu minono ya nyama lakini ni wewe pekee yako unaona ni utmbo?
 
Last edited by a moderator:
Acha kuponda mawazo ya mwenzio, utumbo gani alioandika? yote aliyosema ni kweli! au hufuatilii matukio na taarifa mbali mbali? Kwani siku ana jitetea bungeni akitaja jina la Mungu hukumuona wala kumsikia? Aliye andika namsifu sababu ana kumbu kumbu nzuri. UTUMBO NI WEWE MNAO JAZA JF KWA MAWAZO MGANDO NA UWEZO FINYU WA KUFIKIRI KABLA HAMJA CHANGIA THREAD ZA WATU.

Chaimaharage..........................shukrani kwa mchango mzuri sana...............na hiyo ya avatar iko mahali yake........LOL
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom