Upendo wa Mungu utaleta mabadiliko Tanzania, kila Mtanzania karibu

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,928
3,225
Upendo ni uvumilivu, upendo ni kusaidiana katika mahitaji muhimu.

Sasa kama upendo ni kusaidiana katika mahitaji muhimu, inakuwaje viongozi wa Chama la magamba wanakuwa wabinafsi?

Wanakuwa wezi, wanajiwekea hazina katika benki za nje,Wanauza nchi kwa bei chee ili wapate 10% na wanakula kusaza?

Mungu hapendi dhuluma, Mungu hapendi Hila (Kama za CsM) Mungu anapenda watenda haki.

Daima Nguvu ya Umma itashinda.

Hawa watawala (Chama la magamba) wanatumia Divide and Rule yaani kuwachonganisha watanzania wakose umoja ili wao waendelee kutawala.

Mfano propaganda za udini na ukabila,na ukanda. Chama la mafisadi wanajaribu kutugawanya watanzania ili waendelee kututatawala ili wao waendelee kufaidi rasilimali za Tanzania na kutafuna kodi zetu.

Chama tawala kimetunyima watanzania huduma za afya, Elimu duni, akina mama wanakosa huduma nzuri za uzazi, watoto wetu hawana vifaa shuleni, hawana waalimu. Watoto wa Vigogo wanasoma shule za International Nje ya Tanzania.

Vigogo wa C.sM wanasoma nje na wanatibiwa nje pamoja na watoto wao.

Mungu hapendi, tabia kama hizi za uchoyo na ubinafsi.

Watanzania sasa tuache woga,tuwemajarisi na tudai haki zetu, Mungu yupo pamoja nasi.

Wapo watanzania wanao amini kuwa ipo siku C.sM watakuwa wema. Hakuna siku Shetani amewahi kuwa Mwema. Tafadhali wananchi wenzangu, tusijekuingia mtegoni wa kudanganywa na hawa watawala. Tuepuke vishawishi vya Shetani (Rushwa na ahadi lukuki).

Wamepiga porojo miaka 50, inawatosha, sasa tuseme basi.

Hili Ndilo Neno langu kwa Hii Pasaka.

Nawatakia Watanzania wote Pasaka Njema.


Movement for Change, Tuikomboe Tanzania kwa Pamoja bila kujali itikadi za dini, kabila, rangi au ukanda.
 
Back
Top Bottom