CHAMA cha UPDP kimefanya mabadiliko ya uongozi kwa kumwondoa aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Abdallah Ally.
Mwenyekiti wa chama hicho, Fahmi Dovutwa, alisema mabadiliko hayo yalifanyika katika kikao cha halmashauri kuu ya chama kilichofanyika mwishoni mwa wiki.
Kwa mujibu wa Dovutwa, kutokana na hali hiyo, Hamad Ibrahimu, ameteuliwa kushika nafasi ya katibu aliyepita na kwamba Ally atapangiwa shughuli nyingine.
Kikatiba halmashauri kuu ndiyo inapitisha na kuchagua katibu mkuu, hivyo tumefanya mabadiliko hayo na Ally tumempangia majukumu mengine ya kujenga chama pia, alisema Dovutwa.
Dovutwa alisema kwa sasa chama chake kimejipanga kuhakikisha kinafanya kazi na kuvutia wanachama wengi zaidi na kujipanga na na uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
Source: Tanzania Daima