Updates: Zoezi la kupiga kura - Arumeru East

Status
Not open for further replies.

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,039
2,199
Wakuu nimeona ni vema kuwa na thread moja itakayotumika kuleta updates za uchaguzi huko arumeru east.

Uchaguzi huu wa mbunge wa arumeru east unahusisha jumla ya kata 17 na vituo 327 vya kupigia kura.
Jumla ya wapiga kura 127456 wanatarajiwa kupiga kura.
Majina ya kata ni kama ifuatavyo;

KINGORI
LEGURUKI
NGARENANYUKI
MARORONI
KIKATITI
MAKIBA
MBUGUNI
KIKWE
MAJI YA CHAI
USA RIVER
NKUARANGA
SONGORO
POLI
SINGISI
NKOARISAMBO
AKHERI
NKOARUA

mkurugenzi wa uchaguzi ndg Trasias Kagenzi amewahakikishia wananchi usalama upo wa kutosha.vituo vitafungwa mida ya saa kumi jioni.na anatarajia mpaka kufikia saa saba usiku masanduku yote ya kura kutoka kata zote yatawasilishwa ofisi za halmashauri.

Ametoa namba ya sms kwa wale wanaotaka kujua vituo vyao vya kupigia kura-15540

DOSARI
mgombea wa cdm alimpigia simu kulalamika juu ya mawakala wa cdm kuzuiliwa nje ya vituo vya kura kwa kukosa
fomu za kiapo,hata hivyo amewaelekeza wasimamizi wote kuwa kitambulisho cha wakala kinatosha

mwenyekiti wa ccm kijiji cha akeri anapotoka Siyoi akamatwa akiwaelekeza watu kumpigia kura Siyoi.amesema maelekezo haya amepewa na chama chake.

Mwigulu mchemba akamatwa na polisi baada ya kuhusishwa na kampeni/rushwa kanisani.

TENDWA:jukumu la mpiga kura ni kupiga kura na sio kulinda kura.

UPDATES.....
JOSHUA NASARI ;mgombea wa chadema ameshapiga kura.yapata dk 45 zilizopita.

Watu wameanza kujitokeza kwa wingi kulinganisha na asubuhi wakitokea makanisani.

Vijana wametikia wito wa kulinda kura.maeneo ya patandi,usa,makumira,maji ya chai...kuna makundi makubwa ya watu wakiwa kwenye hali ya utulivu.

Kuna taarifa kuwa kuna wafuasi wanaosadikiwa kuwa wa ccm wamezingira maeneo ya hospitali ya wilaya.haijajulikana kumetokea nini.

Matokeo yanaendelea kubandikwa kwenye vituo mbalimbali; fuatilia thread hii > [h=2]MATOKEO kutoka vituo mbalimbali, Arumeru Mashariki[/h]
 
@Jackbour hetu kwa kata zote kumi na saba ni kata gani ambayo kwa tadhini ndogo cdm wanaweza kuibuka kidedea
 
@Jackbour hetu kwa kata zote kumi na saba ni kata gani ambayo kwa tadhini ndogo cdm wanaweza kuibuka kidedea
ccm wanaweza kujivunia kata mbili tu kwa sasa ambazo ni nkuarisambu na maroroni
ingawa kata hizi zina watu wachache sana.
 
Ni vyema kila kata kukawa na timu inayoratibu matokeo kwa karibu na kutoa taarifa mapema!! Vipi utaratibu wa kuhesabu unafanyika hapo hapo kituoni au mpaka mabox yapelekwe kwa mkurungezi wa kupiga kura. All the best East Arumeru, mkirudia kufanya kile kile mkitegemea kitu tofauti basi majuto ni mjukuu.
 
Haya wakuu mliopo hilo tupeni taarifa zaidi hali ya watu kujitokeza ipo vp,hali ya utulivu kwa kila kituo
 
ccm wanaweza kujivunia kata mbili tu kwa sasa ambazo ni nkuarisambu na maroroni
ingawa kata hizi zina watu wachache sana.

Mkuu mbona nasikia kuanzia Kikatii, USA mpaka Tengeru nako hali si mbaya sana.
 
Vipi kuhusu watu kutoona majina yao kwenye orodha au safari hii hili halipo?
 
Pia mtujuze na matukio yanayaoendelea huko kama vile muamko wa wananchi kulinda kura zao zisiibiwe kwani mbele ya ccm ya Kikwete wako radhi kumwaga damu ili mradi wapate ushindi kwa kauli mbiu ya Ushindi Lazima
 
@Jackbour hetu kwa kata zote kumi na saba ni kata gani ambayo kwa tadhini ndogo cdm wanaweza kuibuka kidedea

Hizi ni ngome za CDM
1.kikatiti
2.Usa river
3.maji ya chai
4.leguruki
5.Maroroni
6. MBuguni
7.Sing'isi/seela
8.Songoro
9. Ngarenanyuki
10. King'ori
11. Poli
Haya mengine 50%
1. Akheri
2.kikwe
3. Makiba
4.nkoanrua
5. Nkoarisambu
6.Nkoaranga
 
Status
Not open for further replies.
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom