Updates:Wabunge wa CCM hatarini kukwamisha Mswada wa marekebisho ya sheria ya Katiba mpya

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
WanaJF,

Niliwaahidi kuendelea kuwapa updates kuhusiana na tishio la wabunge wa CCM kukataa kuridhia marekebisho ya sheria ya Katiba mpya.Katika mazungumzo yangu na wabunge kadhaa wa CCM nimegundua kitu kingine kipya kabisa, kwamba vita hii ya wabunge wa CCM ni mpambano wa makundi ndani ya chama hicho.

Nimeelezwa waziwazi kwamba kundi la mwanasiasa mashuhuri anayetuhumiwa kwa ufisadi linataka kuonyesha jeuri yake ndani ya CCM.


Mbunge mmoja nisingependa kumtaja kwa sasa alinieleza waziwazi kwamba haiingii akilini kwamba Rais ameridhia marekebisho kadhaa kwenye sheria hii halafu eti wajitokeze wabunge ambao wanaonyesha kiburi cha hali ya juu si kwa Rais tu bali hata kwa mwenyekiti wa Taifa wa chama chao.

Inadaiwa wabunge kadhaa walioko katika kambi ya mwanasiasa huyo mashuhuri aliyepania kumrithi Rais Kikwete ndio waliosimama kidete na kukosoa marekebisho haya yaliyoletwa kwa idhini ya Rais na wengine hata wakaenda mbali zaidi na kutishia kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais.


Inadaiwa hata Yule aliyetoa hoja ya kukataa wabunge wa CCM wasikutane na Rais ni mtu kutoka kambi hiyohiyo. Baada ya kikao cha wabunge wa CCM niliwashuhudia wabunge kadhaa walioko kwenye kambi hiyo wakijipongeza kwa kile walichodai ni ushindi mkubwa kwao kwani wameonyesha nguvu waliyo nayo ndani ya CCM.

Mbunge mmoja wa CCM ambaye hayuko kambi yoyote anayetokea mkoa wa Morogoro alinieleza kwa masikitiko makubwa baada ya kikao hicho kwamba hii ni aibu kubwa kwa CCM,alidai ni jeuri ya hali ya juu na utovu mkubwa wa nidhamu kuonyesha dharau kwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa nchi kama walivyofanya.

Pili alisema kwamba hata kama ni watu wawili wanataka kuonyeshana ni nani zaidi basi wasitumie kitu kikubwa kama Katiba ya wananchi kuonyeshana ubabe wao.

Mbunge huyo alienda mbali zaidi na kusema kwamba kwa kujua ama kutokujua basi Rais Kikwete ataungwa Mkono na wananchi katika hili kwani mapendekezo aliyowasilisha bungeni ni kwa maslahi ya Taifa na si binafsi.

Hii ni tofauti na mwenzake anayetaka kuonyesha nguvu zake binafsi kwa kukwamisha nia njema ya Rais na kuwatumia wabunge vibaraka wake.


Nitaendelea kuwapa updates zaidi kila nitakapozipata kuhusiana na suala hili la Marekebisho ya sheria ya Katiba mpya.
 
Kwa kweli inaniuma sana.Hapa Rais Kikwete inatakiwa atumie mamlaka yake ya Kiutawala aliyo nayo
 
Hapa we dare not to hid names, we sema kama huyo mbunge toka kanda ya ziwa ni Chenge
 
Tatizo watu walikurupuka enzi zakupotisha mswada kwa nia yakuwashinda wapinzani sasa inakula kwao sisi CHADEMA tunapeta tu wamalizane wenyewe, tena napenda sana jk avunje bunge ili twende uchaguz mwingine naamini itakula kwao sana tu
!!!
 
r.i.p ccm,sitakulilia kwa sababu kwa miaka 50 umembaka mama yangu tanzania bila maendeleo yoyote pamoja na rasilimali kibao.
kuchelewa kufa kwako ni mauti kwetu,naomba mgomee huo muswada ili muwahi huko walipo kanu na rafiki yake zanupf.
 
r.i.p ccm,sitakulilia kwa sababu kwa miaka 50 umembaka mama yangu tanzania bila maendeleo yoyote pamoja na rasilimali kibao.
kuchelewa kufa kwako ni mauti kwetu,naomba mgomee huo muswada ili muwahi huko walipo kanu na rafiki yake zanupf.

Ningelukuwa Rais ningelivunja bunge hili la porojo
 
Back
Top Bottom