Hivi kwa nini akina VODACOM na wenzao hawatoi misaada kwenye Mahospitali ambapo pana upungufu wa madawa, vifaa vya kazi? Sponsorship zao mkwenye michezo mimi hazinigusi sana kwani mwannchi wakawaida hafaidiki na misaada hiyo. Waache cheap popularity!HATIMAYE mbio za miezi saba ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara, zinaanza leo kwa miamba 12 kushuka dimbani huku bingwa mtetezi, Yanga akianza na wageni, African Lyon kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Yanga, mabingwa mara 22 tangu kuanza kwa Ligi hiyo mwaka 1965, leo wanakuwa wa kwanza kuikaribisha Lyon kwenye ligi hiyo ambao ni msimu wa kwanza kwao.
Hata hivyo, ni mechi inayotarajiwa kuwa ya ushindani mkubwa kutokana na ubora wa vikosi vyao, ingawa Lyon wanazidiwa kwa uzoefu.
Katibu Mkuu wa Lyon, Jeshi Zacharia, amesema pamoja na ugeni wao katika Ligi Kuu, lakini ubora wa kikosi chao, unawapa kiburi cha kujiamini dhidi ya Yanga.
Ni kweli Yanga ni wazoefu zaidi yetu, lakini kwa ubora wa kikosi au kiuchezaji, hilo ni suala jingine nasi tunajivunia kwa hilo, tutajitahidi kuwajengea vijana hali ya kujiamini, alisema Zacharia.
Naye Mwenyekiti wa Yanga, Imani Mahugila Madega, kwa upande wake ameifananisha Yanga kama kinara wa mchezo, ambaye kadiri itakavyokuwa, hauawi.
Alichomaanisha Madega ni kuwa, kadiri itakavyokuwa, Yanga leo itaibuka na ushindi dhidi ya Lyon, hivyo kutwaa pointi zote tatu na kuanza vizuri ligi hiyo itakayofikia tamati Machi 27, mwakani.
Vita nyingine ya ligi hiyo, itakuwa kwenye Uwanja wa Majimaji, mjini Songea, Ruvuma kwa wenyeji Majimaji kuwakaribisha Simba.
Ni mechi ngumu kwani wakati Simba wakitaka kushinda ili kuanza vema ligi hiyo, wenyeji Majimaji watakuwa wakipigana vilivyo kushinda katika uwanja wao wa nyumbani.
Majimaji, timu yenye historia katika soka ya Tanzania, leo watakuwa na kazi moja ya kudhihirisha kuwa hawakupanda Ligi Kuu kwa kubahatisha baada ya kuikosa kwa misimu kadhaa.
Hata hivyo, Simba walio chini ya Kocha Mzambia, Patrick Phiri, safari hii wamejipanga kutwaa ubingwa baada ya kuukosa kwa misimu miwili, ukitwaliwa na watani wao Yanga.
Hata hivyo, vita ya ligi hiyo safari hii inaonekana itakuwa na radha ya aina yake, kwani wakati Yanga wakiwania kutwaa ubingwa wa 23, Simba wamekamia kufanya hivyo kwa mara ya 16.
Aidha, Mtibwa Sugar wenye rekodi ya kutwaa ubingwa huo mara mbili, leo watakuwa katika Uwanja wao wa Manungu, Turiani kuwakaribisha Manyema Rangers.
Mtibwa Sugar, wanaingia katika kampeni ya kuwania ubingwa wa mara ya tatu wakiwa na kiburi cha ubingwa wa Kombe la Tusker na Ngao ya Jamii.
Kivumbi kingine cha ligi hiyo, kitakuwa kwenye Uwanja wa CCM-Kirumba, jijini Mwanza kwa wenyeji Toto Africa kuwakaribisha Moro United ya Dar es Salaam.
Aidha, katika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, wenyeji Kagera Sugar wanaonolewa na Kocha Mganda, George Ssemogerere, watakuwa wenyeji wa Azam FC.
Mechi nyingine, itakuwa katika Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya kwa maafande wa Prisons kuwakaribisha ndugu zao JKT Ruvu ya Pwani.
Source: Gazeti la Tanzania Daima
wakati jkt anapata bao lake moja simba alikuwa na mbili..Ni kweli JKT wamesawazisha mkuu....Mwenendo mzima wa mechi wapatikana hapa kwa Dullo: http://www.dullonet.com/
mwananchi wakawaida ni yupi..Hivi kwa nini akina VODACOM na wenzao hawatoi misaada kwenye Mahospitali ambapo pana upungufu wa madawa, vifaa vya kazi? Sponsorship zao mkwenye michezo mimi hazinigusi sana kwani mwannchi wakawaida hafaidiki na misaada hiyo. Waache cheap popularity!
Yanga ninavyo wajua huenda wasipeleke timu..Kwa Simba niliyoiona leo kama Yanga watatia mguu tarehe 31 Oktoba, lazima wanywe! Kocha wao mpya kutoka Serbia alikuwepo uwanjani na alikuwa anashangilia mabao ya Simba. Ila aliondoka kabla mchezo haujaisha na kusababisha kuzomewa na wana-Simba.
uwanjani au...maana kama ni kifedha nadhani yeye na manji wamechemka..Nasikia mnyama ashakula buti moja, 1-0 !! Mwaka huu labda Jk awasaidie YY ...
Yanga ninavyo wajua huenda wasipeleke timu..
Hivi kwa nini akina VODACOM na wenzao hawatoi misaada kwenye Mahospitali ambapo pana upungufu wa madawa, vifaa vya kazi? Sponsorship zao mkwenye michezo mimi hazinigusi sana kwani mwannchi wakawaida hafaidiki na misaada hiyo. Waache cheap popularity!
I like this actually. Simba ni timu kubwa sana na kwa maana hiyo inahitaji viongozi wenye nidhamu ya uongozi na siyo blah blah za Uswahilini na kushikiana bakora kila kuchapo. Simba ubingwa ni wa nyumbani msimu huuNajua mambo yakienda kama yalivyopangwa, December tutakuwa na presida, wa nguvu ambaye ana quality zote
I like this actually. Simba ni timu kubwa sana na kwa maana hiyo inahitaji viongozi wenye nidhamu ya uongozi na siyo blah blah za Uswahilini na kushikiana bakora kila kuchapo. Simba ubingwa ni wa nyumbani msimu huu
Hivi kwa nini akina VODACOM na wenzao hawatoi misaada kwenye Mahospitali ambapo pana upungufu wa madawa, vifaa vya kazi? Sponsorship zao mkwenye michezo mimi hazinigusi sana kwani mwannchi wakawaida hafaidiki na misaada hiyo. Waache cheap popularity!
SSC tupo mbioni kufungua web site ya uhakika. Mwaka flani, zamani enzi za Siang'a nilikuwa na utaratibu wa kununua viatu swafi vipya na kuzawadia player of the month, ambaye alikuwa anateuliwa na kocha kutokana displin, maudhurio ya mazoezi na kufuata maagizo ya kocha. Ilisaidia sana kuongeza motisha na kuwafanya players wawe na mori ya kutisha. Ofcourse zawadi hiyo ni ndogo, lakini kubwa pia kwa kule nyumbani hasa kupata viatu vya kisasa, leather na quality ya juu. Nashauri tuanze tena utaratibu huu, hasa kwa wale wapenzi wa kweli !!
Pia kwa wale ambao hawana forms za uanachama, huu ndo muda muafaka wa kujiunga. Najua mambo yakienda kama yalivyopangwa, December tutakuwa na presida, wa nguvu ambaye ana quality zote, na ambaye hata akienda kuongea na akina Blatter, basi watajua kweli kuna timu kubwa bongo- Simba. Stay tuned...