Updates kutoka Sahara - Mwanza mkutano wa CHADEMA

Kila kukicha mikutano sijui watanzania tunaelekea wapi

Tunaelekea kwenye Ukombozi, kama baba au mama yako ni Fisadi mjitaarishe kufilisiwa na kusekwa ndani. Mtaiogopa sana mikutano kwani somo la uraia linawaingia Walalahoi sasa kazi kwenu Mafisadi, mkae mkao wa kuliwa
 
Kwa hiyo hotuba ya Lema huko Sahara Mwanza ndio hiyo...sasa inahusu watu Mwanza ukawambie habari za mapenzi tena ulivyokuwa mahabusu Arusha.

Hakuongelea mfumuko wa bei na kuanguka kwa uchumi duniani.

Kasemaje kuhusu kuwainua wana Mwanza kiuchumi?

Mpigie akueleze zaidi.
 
Kwa nini usiulize Serikaki yako sikivu kuhusu mfumuko wa bei na kuwasaidia wana mwanza kiuchumi?Lema yeye atawasaidia wana mwanza kiuchumi kwa madaraka gani aliyo nayo?anachoweka wazi ni jinsi sheria za nchi zisivyoheshimiwa,na jinsi mashetani wachache walivyojipa umungu watu na kuwaumiza raia wengine wasio na hatia kwa kuwabambikia kesi za kukomoana!wewe haujuhh kama kesi za kubambikiwa ni nyingi sana nchi hii?au hauoni kama ilo ni tatizo kwa kua wewe haujawa muathirika wa ilo!
 
Mkuu kwani Chadema hawana sera uchumi ambazo wanaweza kuzielezea kwenye mikutano yao zaidi ya ufisadi.
 
Mkuu kwani Chadema hawana sera uchumi ambazo wanaweza kuzielezea kwenye mikutano yao zaidi ya ufisadi.

Unataka waelezee uchumi wakati wakizalisha Mafisadi wanachukua. Kumbuka CHADEMA siyo chama tawala.

:target:
 
Wenje hakuwepo, kwa mujibu wa Slaa, Wenje alikuwa ktk majukumu mengine ya kichama ikiwa ni pamoja na kwenda Dodoma kusaidia harakati za Zitto dhidi ya Serikali
 
imetosha kwa mwanza na arusha, sasa slaa na lema nguvu ielekezwe mikoa mingine
 
Kwa hiyo hotuba ya Lema huko Sahara Mwanza ndio hiyo...sasa inahusu watu Mwanza ukawambie habari za mapenzi tena ulivyokuwa mahabusu Arusha.Hakuongelea mfumuko wa bei na kuanguka kwa uchumi duniani.Kasemaje kuhusu kuwainua wana Mwanza kiuchumi?
hoja yake ya msingi ilijikita katka uonevu usababishwao na serikali ya magamba, na akihusianisha hoja yake na kuvuliwa ubunge. Pia maandalizi ya wanamwanza kujiletea ukombozi wa kweli wakati utakapotimu
 
Mikutano kila siku Mwanza? Hebu waacheni wananchi wafanye kazi/wapumzike this w.end. Acheni kuwachosha na upuuzi wenu usio na manufaa kwa wananchi. Kama mmekosa cha kufanya niambieni nitawaapatia.

ovyoooooo!bado haujavua gamba?
 
Further Updates: Dr. Slaa akihutubia umati mkubwa uliojitokeza ktk viwanja vya Sahara jijini Mwanza, amewataka wanamwanza kujiandaa kutia sahihi ktk zoezi la kumwondoa JK madarakani iwapo hatachukua hatua madhubuti dhidi ya ubadhirifu wa mawaziri na kuongezeka kwa hali ngumu ya maisha. Dr. Slaa ameelezea zoezi hilo kuwa linahitaji sahih za wapiga kura 8,000,000 kitaifa yaan theruthi moja ya wapiga kura wote walioshiriki uchaguzi mkuu ulopita. Akasisitiza kuwa rais hana budi kuachia madaraka kidemokrasia iwapo wapigakura wataridhia kusaini, hata kabla muda wa uchaguzi mkuu ujao kwa kuwa rais hautekelezi vema mkataba kati yake na wapigakura wake
 
Mikutano kila siku Mwanza? Hebu waacheni wananchi wafanye kazi/wapumzike this w.end. Acheni kuwachosha na upuuzi wenu usio na manufaa kwa wananchi. Kama mmekosa cha kufanya niambieni nitawaapatia.

Kinavyokuuma,kinavyokunyongorota,utaisomamwaka hùu,mtu na akili yako ukajivisha akili ya maiti kuitetea ccm,fimbo tuliyowachapia arumeru tunaisambaza nchi nzima,CCM TOO DESPERATE,mwenyekiti wenu aliyaona mapeema ndo maana hataki kushinda nyumbani,kiti cha moto anaogopa tu kusema,MTAKOMA MWAKA HUU
 
Mkuu kwani Chadema hawana sera uchumi ambazo wanaweza kuzielezea kwenye mikutano yao zaidi ya ufisadi.

sera za uchumi zinaanza na kuondoa ufisadi kwanza. watu wajuwe kama serikali ya m_kwere ni ya kifisadi, imejaa mafisadi, na kwa hiyo watanzania wanapojiandaa kuleta mabadiliko, wajuwe tuna adui wa kupambana naye kabla ya kufikiria kujenga uchumi imara kwa vitendo.
 
Akihutubia Dr. Slaa na kuwashangaa wabunge wa CCM kwa unafiki wao hasa wanapopiga kelele lakini amesema waliotia saini kwa ZITTO ni 7 tu.
watu wamejiunga Chadema na kutupa kofia na nguo za CCM.

Kiukweli CCM hawana chao tena hapa nchini kuanzia 2015 kwa aliyeona ile habari awe shahidi mwema kilichotokea huko Sengerema.

SOURCE: ITV HABARI USIKU HUU
 
Mikutano kila siku Mwanza? Hebu waacheni wananchi wafanye kazi/wapumzike this w.end. Acheni kuwachosha na upuuzi wenu usio na manufaa kwa wananchi. Kama mmekosa cha kufanya niambieni nitawaapatia.

Rejao ni ajira ngapi mmetengeneza? watu hawana kazi. Wapumzike wapi wakati hawana hata huduma za msingi sana kama chakula, malazi, maji & mavazi?
 
kujibishana na Rejao na Ritz ni sawa na kujaribu kufanya conversation na kondoo wa sufi kuhusu hali ya hewa!
 
georgemotika ni hovyo kabisa. huna mbele wala nyuma yaani hueleweki kama sigara kali. utaanzishaje thread halafu ushindwe kuupdate? Ujue jf ipo kimataifa so dunia yote inakutegemea wewe, wewe na e unaingia mitini. hatuko serious na tukifanyacho ndo maana hatuendelei. nyie jf member wa mwanza hamna kitu mnazidiwa na jf wa Kahama. Hii ni aibu yenu nyote mlioshindwa kuchangia. kwanini msijifunze kwa wenzenu wa arusha, mbeya na dar es salaam? mumezoea kutafuniwa tu, mnashindwa hata kupiga picha moja!..ptuu..!
 
Mikutano kila siku Mwanza? Hebu waacheni wananchi wafanye kazi/wapumzike this w.end. Acheni kuwachosha na upuuzi wenu usio na manufaa kwa wananchi. Kama mmekosa cha kufanya niambieni nitawaapatia.

hata unavosema hiv huon aibu,ndo nyie magamba msiotufaa hum kwenye javi.ukiwa huwa la kuchangia ni vema usiseme kitu
 
Back
Top Bottom