Barubaru
JF-Expert Member
- Apr 6, 2009
- 7,161
- 2,323
Madaktari wa jeshi wameandaliwa kuwatibu majeruhi wa vita kwenye uwanja wa mapambano na kuwaandaa ili wasafirishwe kwenda kwa hawa wa kiraia waliogoma kwa matibabu zaidi. So kwa ufupi hawa waliogoma wanaanzia pale wale wa jeshi wanapoishia. Sasa unapowatoa hawa wa kiraia halafu unaleta wa jeshi unatarajia wafanye nini kama sio kuwaonea tu?
Labda tu nikujuze kidogo.
Kumbuka kuwa duniani kooote hospital za jeshi ndio hospital kuu na mara zote zinakuwa na kila kitu na wataalamu wengi sana na wenye uwezo mkubwa na zinakuwa ni za rufaa. Hata viongozi wa nchi wakiumwa mara zote wanatibiwa katika hospital za kijeshi kutokana na usalama na weledi wa maDr wao.
Nakumbuka hata Tz , Jeshi lilisomesha sana madaktari wake enzi hizo na kuiimarisha hospital yao ya lugalo.
Pasi na shaka yoyote huko Tz lugalo ni hospital ya rufaa pia kijeshi. Hakuna mtu anayeweza kupewa uhamisho toka lugalo kwenda muhimbili kwa matibabu zaidi.
Hata mgomo wa 2003 wa madaktari hao hao wa Lugalo walishika muhimbili na kuiendesha mpaka mgogoro ulipoisha
Chunguza hilo.